Kisiwa cha Ukara (Ukara Island)

Kisiwa cha Ukara (Ukara Island)

Mh!! Sasa hayo majani naona bonge la dili na inabidi hiyo miti ipandwe mingi ili kuvutia watalii
 
Bwana safiri salama!

Kwenye majumuisho yako naamini kuna vitu vingi hutaweza kuvifaham! Usisite kutuomba msaada wenyeji wa huko tukujuze na jamii kwa ujumla
 
Kwa ujumla Ukerewe kama Wilaya ina visiwa jumuishi 11...kutia ndani kisiwa cha Ukara. Wenyeji wa ukara hudhaniwa kuwa washirikina sana kuliko wakaazi wengineo wa Ukerewe.. Pengine ndio sababu kubwa ya kusema kuna jiwe linacheza.
Hata hivyo, yapo mambo flani ambayo yakitangazwa vizuri yanaweza kuwa kivutio cha watalii, tofauti na hilo jiwe ambalo limehodhiwa na ukoo mmoja kwa madai kwamba ndio wenye nguvu za asili za kulichezesha hilo jiwe.
Mkuu umekosea ukerewe ina zaidi ya hivyo 11 ulivyosema, hebu hesabu hivi ambavyo mimi navikumbuka

Kweru
Kweru mto
Irugwa
Ukara
Sizu
Garinzila
Kamasi
Mafunke
Kibinda
Kiara
Burubi
Izinga
Siza
Ghana
Marerema
Lyamwenge
Bwiro
Kenfunezya
Furu mbisi

Hivyo ni baadhi tu!

Ukiongea hapa uwe na facts watu tusha declare huko ndo kwetu so tunajua mengi
 
Nishaenda Irugwa (Ukerewe), Rukuba (Musoma Rural), Maisome (Buchosa, zamani Sengerema), Kerebe (Muleba), Goziba (Muleba), Bumbure/Mahaiga (Muleba), Ikuza/Kasenyi (Muleba) na Iramba/Murumo (Muleba).

katika visiwa vyote hivyo, Goziba, Kerebe na Iramba vina mandhari nzuri sana.
Uje utembelee na kisiwa cha Ghana, hiki ndo kisiwa chenye starehe zaidi, wao hupenda kukiita Cape Town
 
Pale karibu na uwanja wa mpira kuna soko la samaki , zahanati pia kuna kanisa la kihistoria la roman ..babu yangu alikuwa ni padre hapo anaitwa father bwile alifariki miaka miwili iliyopita. Ndiye kwenye ukoo wetu mungu alimjalia kupata daraja takatifu..

Basi mpaka hapo wewe nindugu namimi hapo unapo pasemea ndio uwanja wetu wa nyumbani ukiulizia ukoo wa Nyabelo tu nimalamoja unafikishwa
 
safari iamalizika leo kwa kutoka Nansio hadi Bugorola saa 5 , na kutoka Bugorola hadi Bwisya (Ukara) saa sita.
 
Jamaa anaelichezesha huwa hataki msimame upande wake... Na watu kwa vile wameaminishwa ni miujiza, hukubali bila kuhoji.. Bahati mbaya wengine tumetokea kwenye Jamii ya watenda miujiza....kwetu kamati za ufundi ni kama Wacongo na muziki!!
ha haha sasa akilisukuma kwa nguvu zaidi itakuwaje
 
Pale karibu na uwanja wa mpira kuna soko la samaki , zahanati pia kuna kanisa la kihistoria la roman ..babu yangu alikuwa ni padre hapo anaitwa father bwile alifariki miaka miwili iliyopita. Ndiye kwenye ukoo wetu mungu alimjalia kupata daraja takatifu..
Father bwile yupi ndugu yangu? Alikuwa na kakake anaitwa sebastian machele? Usijekuta ndugu halafu hatujuani
 
ukara ndo naisikia leo.. endelea kutujuza kisiwa kilivyo.hali ya uchumi
hata mimi, ila nakumbuka hotuba ya Baba wa taifa mwalimu JKNY akisema MKARA!!!!! sasa nimejua hao watu wanapatikana wapi. endelea kutujuza mengi kutoka huko. kama walet bado ikosafi usisahau kupitia call me J. wakupe minofu ya Bashite jaribu kupiga stori 2,3 na majirani
 
Back
Top Bottom