Mawizard kichizi hukoMabinti wa kule wamezoea kucheza kadogoli kwa hyo kwa viuno mmakonde akasome. Ukizingua kuna uchawi wa kuitiwa mamba yaan anakufata nchi kavu
Mkuu hebu elezea kidogo tu kuhusiana na MBUNYE za Ukerewe na huko Ukara, nina mpango wa kwenda kutalii huko soon.
Safari njema lakini kaa chonjo; Wakara ni mafundi sana kwenye tasnia ya usangoma!
HaaNatafuta fundi aliepo ukara
HaaMabinti wa kule wamezoea kucheza kadogoli kwa hyo kwa viuno mmakonde akasome. Ukizingua kuna uchawi wa kuitiwa mamba yaan anakufata nchi kavu
Nipo serious
Ukara, jina langu na huko ndiko kwetuLeo nasafiri kwenda katika kisiwa cha Ukara, nmeona ni vyema ningewajuza kuhusu kisiwa hiki kilichopo ndani ya mipaka ya Tanzania. Kabla sijaja Mwanza kikazi nlikuwa nasikia kuhusu kisiwa cha Ukerewe tu, kutokana na kazi yangu nimeweza fika katika visiwa nane tofuti na Ukerewe vyote vikiwa ndani ya mipaka ya Tanzania. Hivyo leo tutaiongelea Ukara tu.
Ukara ni kisiwa cha pili kwa ukubwa ndani ya ziwa Victoria kwa upande wa Tanzania, kisiwa kinachoongoza kwa ukubwa ndani ya ziwa ni kisiwa cha Ukerewe.
Wenyeji wa kisiwa cha Ukara wanaitwa Wakara, hawa wanaongea lugha inayoingiliana na wajita wa Musoma, pia wakerewe huongea lugha hiyo hiyo.
Kisiwa cha Ukara kina mawe yaliyopachikwa jina la "the dancing stones", kwamba mawe yanayocheza. Sijawahi kwenda yatembelea bado, japo ntajitahidi fika huko kwa siku za usoni. Pia inasemekana kuna mti ambao majani yake yakiingia ndani ya ziwa, yakitoka anatoka mamba na sio majani tena.
Kufika Ukara kwa kutokea Mwanza inakubidi upande ferry kutoka Mwanza hadi Nansio Ukerewe, baada ya hapo utapanda Tax kutoka Nansio hadi Bugorora, kutoka Bugorora utapanda tena ferry hadi Ukara, Ferry inafikia katika kijiji cha Bwisya.
Ntaendelea wajusa safari ya Ukara step kwa step.
View attachment 478574
Wewe utakuwa mvuvi wa samaki au mfanyabiashara wa samakiNishaenda Irugwa (Ukerewe), Rukuba (Musoma Rural), Maisome (Buchosa, zamani Sengerema), Kerebe (Muleba), Goziba (Muleba), Bumbure/Mahaiga (Muleba), Ikuza/Kasenyi (Muleba) na Iramba/Murumo (Muleba).
katika visiwa vyote hivyo, Goziba, Kerebe na Iramba vina mandhari nzuri sana.
Hii picha ndio wapi au ndio ukala
Sijaona pisi kali kwenye hii picha
yaani ziwa looote lile, wao tu ndio waonekane wanakula samani? wakurya pia hawapo mbali na samaki na wanakula ila utasikia mtu anakwambia wajaluo ndio wenye akili kwasababu ya samaki.Wazawa wa ukara ni watu wanaoongoza kwa usiri na wana IQ kubwa kuliko makabila mengine yapatikanayo Nchini mwetu.
Inasemekana wengi wao wanatumika sana na ''watu wa suti nyeusi''
Kwa utafiti wangu mwembamba kinacho wafanya wawe na uelewa mtambuka ni kutokana na ulaji wa vichwa vya sato na kamongo!
NYEHUNGE wa Ferry ndio huyu huyu wa Mabasi ya siku hizi(Moro - Mwanza)?Nmetoka Mwanza mchana na kufika Nansio Ukerewe jioni, hapa ntalala na kumalizia safari yangu kesho.
Kwa sasa Nyehunge kaleta ferry mpya, kaipa jina la Nyehunge II, ina class tatu, VIP, First Class na Second Class. Naona safari ya Nansio imefanywa ni ya kuvutia sasa tofauti na zamani.
Nyakalilo niliwahi kusikia ipo SengeremaKuna kijiji cha Kome kilichopo katika kisiwa cha Ukara na kuna kisiwa cha Kome kilichopo wilaya ya Sengerema.
Nyakalilo sina uhakika nacho.