Kisiwa cha Ukara (Ukara Island)

Kisiwa cha Ukara (Ukara Island)

Leo nasafiri kwenda katika kisiwa cha Ukara, nmeona ni vyema ningewajuza kuhusu kisiwa hiki kilichopo ndani ya mipaka ya Tanzania. Kabla sijaja Mwanza kikazi nlikuwa nasikia kuhusu kisiwa cha Ukerewe tu, kutokana na kazi yangu nimeweza fika katika visiwa nane tofuti na Ukerewe vyote vikiwa ndani ya mipaka ya Tanzania. Hivyo leo tutaiongelea Ukara tu.

Ukara ni kisiwa cha pili kwa ukubwa ndani ya ziwa Victoria kwa upande wa Tanzania, kisiwa kinachoongoza kwa ukubwa ndani ya ziwa ni kisiwa cha Ukerewe.

Wenyeji wa kisiwa cha Ukara wanaitwa Wakara, hawa wanaongea lugha inayoingiliana na wajita wa Musoma, pia wakerewe huongea lugha hiyo hiyo.

Kisiwa cha Ukara kina mawe yaliyopachikwa jina la "the dancing stones", kwamba mawe yanayocheza. Sijawahi kwenda yatembelea bado, japo ntajitahidi fika huko kwa siku za usoni. Pia inasemekana kuna mti ambao majani yake yakiingia ndani ya ziwa, yakitoka anatoka mamba na sio majani tena.

Kufika Ukara kwa kutokea Mwanza inakubidi upande ferry kutoka Mwanza hadi Nansio Ukerewe, baada ya hapo utapanda Tax kutoka Nansio hadi Bugorora, kutoka Bugorora utapanda tena ferry hadi Ukara, Ferry inafikia katika kijiji cha Bwisya.

Ntaendelea wajusa safari ya Ukara step kwa step.
View attachment 478574
Nasikia kuna gari moja tu aina ya Landrover ya mwaka 1966!,kwa anayekumbuka hotuba za Mwl Nyerere kuhusu hatima ya muungano na uraisi nadhani mnakumbuka alipotania kuwa ''ah nae Mkara anataka kumgombea uraisi''
 
Hongereni wakerewe&Wakala kwa Uzi wenu, nimewapenda bure akina chimenyane.
 
Kuna ndugu yangu kaolewa na mkara yani watoto wa wifi hawarudi kwao wakati wa likizo wakishafunga shule kisa watarogwa na wanakijiji wa huko
 
"Sidhani kama Kiongozi wa Nchi hii aliushawahi kutoka huko". (Azarel)


Azarel nakucheka kwa dharaaaaaaaaaahu
 
Uje utembelee na kisiwa cha Ghana, hiki ndo kisiwa chenye starehe zaidi, wao hupenda kukiita Cape Town
Kisiwa Chenye starehe ni "Mchangani" hapo Wanaishi Watu wazima pekee tena Wafanya Biashara hakuna Watoto wala Shule!! Na ni marufuku kuishi na familia kule!.
N/B Wanaishi Wafanya Biashara kwa sababu ni Hifadhi ya Misitu inayojumuishwa kwenye na HIFADHI YA MSITU WA BUHINDI. "Buhindi Forest and game Reserve"

Mchangani_Kome/ Jimbo la Buchosa
 
Back
Top Bottom