La
Labda dini yakeWakuu amani iwe nanyi,
Jana Mh Rais ameteua baraza la mawaziri na miongoni wa mawaziri walioteuliwa ni aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania Mr Geoffrey Mwambe.
Geofrey Mwambe amekuwa mkutugenzi wa TIC kwa kipindi cha miaka mitatu na katika kipindi hicho Mr Mwambe alichemka sana. Katika kipindi chake TIC ilishutumiwa sana kuzungusha wawekezaji na kuwa na ukiritimba kwenye suala zima la uwekezaji nchini mpaka kupelekea wawekezaji wengi kukimbia na nchi kukosa pesa.
Hali hii ilipelekea mpaka TIC kuhamishiwa ofisi ya Rais kwa kile kilichodaiwa kuipa ufanisi zaidi.
Swali langu: Ni kipi kimembeba mchumi huyu mpaka kuwa waziri ilihali huko TIC alichemka?