Waziri Mkuu avinadi vivutio vya uwekezaji Italia. Ataja msimamo wa Rais Samia wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa nchini Italia kuja Tanzania kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kuwa Tanzania ina malighafi za kutosha pamoja na uwepo wa masoko ya uhakika kutokana na eneo la kijiografia.

“Msisitizo wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mkakati wa Serikali ni kuwahamasisha wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa mbalimbali nchini waje kuwekeza katika ujenzi na kuzalisha bidhaa hizo nchini ili zipatikane kwa wingi na kwa urahisi.”

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 19, 2023) wakati akizungumza katika Jukwaa la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia lilifanyika Palazzo Regione Lombardia, Milan nchini Italia. Waziri Mkuu yuko nchini Italia akimuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Jukwaa la Kimataifa la Chakula Duniani ulioanza Oktoba 16 hadi Oktoba 20, 2023, Rome nchini Italia.

Mheshimiwa Majaliwa ametaja baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji hao wanaweza kuja kuwekeza katika sekta za madini, kilimo, mawasiliano, mifugo, uvuvi, utalii na afya hivyo amewakaribisha wafanyabiashara hao na wawekezaji watumie fursa hiyo na kuwekeza nchini.

Aidha, Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa na maeneo na mazingira mazuri ya uwekezaji pia amesema nchi ina vivutio vingi vya utalii hivyo, amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara, pia Mheshimiwa Majaliwa ameyakaribisha makampuni na mawakala wa utalii waje nchini na kuwekeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii katika miji mbalimbali yakiwemo majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa sasa Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, viwanja vya ndege na nishati ya uhakika ili kurahisisha shughuli mbalimbali zikiwemo za uwekezaji.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo ametumia fursa hiyo kuwahakikishia ushirikiano wawekezaji na wafanyabiashara wote kutoka nchini Italia ambao watahitaji kuwekeza na kufanya biashara nchini Tanzania.

Jukwaa hilo la Tatu la Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Italia limehudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji zaidi ya 300 kutoka mataifa hayo. Pia, mbali na wafanyabiashara na wawekezaji pia limehidhuriwa na Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Taasisi hizo ni pamoja Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Kukuza ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ambao viongozi wake walipata fursa ya kutaja fursa za uwekezaji zilizopo nchini pamoja na namna ya kuwawezesha kuyafikia maeneo hayo.

Screenshot 2023-10-19 at 16.05.18.png
Screenshot 2023-10-19 at 16.05.28.png
 
- Ataja msimamo wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini

IMG-20231019-WA0160.jpg
IMG-20231019-WA0161.jpg
IMG-20231019-WA0159.jpg
IMG-20231019-WA0162.jpg
IMG-20231019-WA0163.jpg
 
View attachment 2786440View attachment 2786441
Ni ngumu sana kwa mwekezaji makini kuja kujenga kiwanda Tanzania.

Hakuna mwekezaji makini anayeweza kwenda kuwekeza katika nchi ambayo mifumo na sheria za kodi zipo ovyo kama zilivyo nchini Tanzania.

Kodi na tozo kwa kiwanda kwa nchi ya Tanzania, zipo zaidi ya 20, wakati nchi kama Botswana, idadi ya kodi na tozo kwa kiwanda, hazizidi 5. Sisi tutabakia kuwa wachuuzi wa bidhaa hafifu za China.
 
Back
Top Bottom