Kipi kimemfanya Geofrey Mwambe aliyekuwa Mkurugenzi (Director) wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuteuliwa kuwa Waziri wa Biashara na Viwanda?

Je, jamaa ana exposure na dunia ya nje?!

Unajua kuna baadhi ya posts zinahitaji zaidi ya madgrii ya darasani na local experience bali exposure!!!

Hivi huyo Mwambwe anaweza kuinua simu na kumpigia Dangote na Dangote asiulie "Who? Mwambe??! Mwambe who? Come again?"

Anyway, nadhani nimeenda mbali sana!!! Hivi anaweza kuinua simu kumpigia hata Rostam Azizi?!

Ndo vile tu itakuwa ngumu lakini kama kuna Mtanzania anayeweza ku-fit hiyo position basi ni Mzee wa Msoga!!! Lakini ningekuwa JPM, hata watu kama Mwamvita Makamba wanaweza ku-fit compared na hao akina Mwambe!

Hawa watu wasio na exposure wanachoweza kufanya ni ku-attend Prospective Investors waliobisha hodi kwenye milango yao lakini sidhani kama wana ubavu wa kufanya "Investors Hunting" popote walipo duniani!!

JK pamoja na mapungufu yake mengi, alikuwa anafahamu sana nani akae wapi, na ndio maana akamvuta Julieth Kairuki ambae kabla ya uteuzi wake alikuwa kwenye banking sector huko South Africa na pia kuwa Project wa Private Public Partinership Capacity Building kwa nchi za SADC!

Kwa CV yake hiyo, tu tayari utaona Julieth kwenye mafaili yake alikuwa na orodha ya Wafanyabishara wa SADC ambao miongoni pengine alikuwa na uwezo wa kunyanyua simu na kuwapigia!

UPDATE:

Ukweli nilikuwa simfahamu kabisa huyo Mwambe lakini baada ya kuandika hayo hapo juu, nikalazimika kum-Google kidogo!!! Wallah JPM hayupo serious! Kumbe huyo jamaa kabla ya kuingia TIC alikuwa DC wa Manyoni?! Halafu ex-DC wa Manyoni ndie tulimpa dhamana ya kuvutia Foreign Direct Investment wakati hata akikutana na Diamond Platnumz tu lazima alikuwa anababaika!!!

Utani huu!!
Well said brother,..

I wish Meko angeisoma hii point yako....,,a very good point
 
Hayo pia nimeyaona lakini naona info kama bado chache mno! Kwa mfano hapo Foreign Affair, nimeona alikuwa Mkurugenzi wa Biashara BUT for ONLY one year... kabla ya hapo alikuwa anafanya nini... sijapata!!

Aidha, hapo BoT pamoja na TTCL nimeona akiwa tu Mjumbe wa Bodi!!! Matumaini yangu mtu kuwa Mjumbe wa Bodi, basi kawahi kufanya kazi hapa na pale... hicho ndicho sijaona kikijitosheleza; unless nami ni-conclude kama wengine kwamba inaweza jamaa ni Afisa Kipenyo!!

Lusungo
Kama nakuelewa, ni vigumu kwa sasa kumpata mtu unayemaanisha kwasababu wateule wengi wa sasa hawakuandaliwa kuwa viongozi kama ilivyokuwa hapo nyuma na waliojiandaa ambao huenda wako kwenye taaisi kubwa kubwa za kidunia si rahisi kukubali kuachia huko kwenda bongo kukutana na balaa la uteuzi. Jiulize mtu kama waziri wa madini au PST kabla ya kuibuka awamu hii walikuwa wapi? Mi naona wameibuka tu.
 
Akili mbovu za Kilumumba hizi manake huwa mnakurupuka tu na kuandika bila kuelewa!!

Hapa nimezungumzia suala la uwaziri au nimezungumzia Mwambe alivyokuwa TIC?!
Rudiaxkusoma ulichoandika inawezakana akili zako huwa zinahamahama.
 
Wakuu amani iwe nanyi,

Jana Mh Rais ameteua baraza la mawaziri na miongoni wa mawaziri walioteuliwa ni aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania Mr Geoffrey Mwambe.

Geofrey Mwambe amekuwa mkutugenzi wa TIC kwa kipindi cha miaka mitatu na katika kipindi hicho Mr Mwambe alichemka sana. Katika kipindi chake TIC ilishutumiwa sana kuzungusha wawekezaji na kuwa na ukiritimba kwenye suala zima la uwekezaji nchini mpaka kupelekea wawekezaji wengi kukimbia na nchi kukosa pesa.

Hali hii ilipelekea mpaka TIC kuhamishiwa ofisi ya Rais kwa kile kilichodaiwa kuipa ufanisi zaidi.

Swali langu: Ni kipi kimembeba mchumi huyu mpaka kuwa waziri ilihali huko TIC alichemka?
Ungependa awekwe nani...?
 
Nanukuu"
Katika kipindi chake TIC ilishutumiwa sana kuzungusha wawekezaji na kuwa na ukiritimba kwenye suala zima la uwekezaji nchini mpaka kupelekea wawekezaji wengi kukimbia na nchi kukosa pesa.

Swali linakuja unauhakika mamlaka iliyomteua haijapendezwa na hicho nilichonukuu hapo?
Kuna mambo ya kujirudi, refer kwa andengenye.
 
Kwa mahitaji ya nchi yanayozingirwa na mabadiliko mengi kidunia hasa katika medani za teknolojia, uchumi na siasa...process ya uteuzi inapaswa ifanyiwe marekebisho, sikweli kabisa kuamini kuwa TISS ndio wanajua kila kitu cha nchi hii na wao wanastahili kudrive process za uteuzi, huko ni kujidanganya, pili, ni vyema sasa wanaopendekezwa uteuzi wapitie usaili wa namna moja au nyingine kuthibitisha uwezo wao, uelewa, elimu, maarifa, tabia, mahusiano na mambo gani mapya kama anayafahamu yanaweza ifaa nchi..tatu, nchi zote zenye mkakati imara wa maendeleo wanatumia sana uwepo wa diaspora kubuni na kuweka mikakati ya maendeleo inayotumia teknolojia na kusaili ushindani wa mataifa kwenye maendeleo uliopo, huwezi kuwa na Baraza la mawaziri 23 halafu hakuna diaspora hata mmoja!!!! tarajia total failure, wapo watanzania wengi wenye uwezo mkubwa sana kushape ajenda yetu ya maendeleo kwa sasa, ishu si kununua ndege, kuuza korosho, kukusanya mapato nk..NOOOO! tusiwe km bado tuko dunia ya mwaka 1980..mambo yale yale, traditions!kwamba kwenye baraza la mawaziri lazima iwepo wizara ya biashara na viwanda..bila hata kujiuliza hapa kwetu biashara tulizo nazo ni za aina gani, kubwa ndio nyingi au za kati na za chini ndio nyingi, viwanda gani tunahitaji na vijengwe wapi na wapi na kwa wakati gani...anyway ngoja tuone, sikutarajia mtu km Profesa Matambalya, mtanzania aliyefanya kazi UNIDO na kusimamia vizuri reform ajenda ya Industrialization kwa nchi za Africa, safari hii tena asiwemo kwenye cabinet kuisadia nchi yetu..nadhani pia nafasi ya chief secretary inahitaji mtu mpana sana na mjuzi mwenye maarifa mengi juu ya dunia ya sasa...sifa ya kuwa ulifanya vizuri ulipokuwa katibu mkuu wizara fulani hivyo unafaa kuwa chief secretary ni dhaifu sana..kwa kiwango kikubwa matokeo ya utendaji wa serikali kwa ujumla yanategemea sana uwezo wa mtu wa nafasi hii...haya mambo ya tumbua teua, tumbua teua ni kielelezo cha udhaifu wa mtu anayeshika nafasi hii..tukiwa wakweli kwa dhamira zetu na mbele ya mwenyezi Mungu km kweli tuna nia ya maendeleo kwa watanzania, nafasi hii inahitaji mtu wa kaliba ya Dr. Slaa..
kila la heri kwa wateuliwa!
 
Aisee! Kupitia michango humu nimeona kwa kiasi gani JF ina taarifa za uzushi. Nimesoma michango yote nimejiridhisha watu mlivyo wazushi wengi wenu. Namjua huyu bwana in and out. Itoshe kusema tusipende kuongea mambo tusiyoyajua.

Naandika kwa ufupi, mimi si muumini wa utawala huu, ila kwa uteuzi wa huyu bwana kwa nafasi hii ni jambo muafaka. Mwambe ana exposure, visionary na anaweza ku-offer kila kitu kinachohitajika. Ana mapungufu yake kama binadamu na mengine nisingependa niyaandike hapa- maana ni personal - hasa kati ya mimi, yeye na partnership ktk mambo binafsi. Kigezo cha mimi kuwa na tofauti naye si sababu ya kupindisha ukweli kumhusu. Ukweli lazima usemwe.
 
Mkuu umeongea point tupu, japo simjui sana jamaa lakini nahisi ni mtu wa kitengo maana licha ya madudu kaula, amekuwa TIC kutokea kwenye uDC na pia ni memba wa bodies za BOT Na ttcl mobile.
Hata BOT aliifanya iwe Bank kuu inayopora pesa za watu zinazotumwa tokea nje kuliko bank kuu zote Duniani, huku ikiongoza kwa kuwatishia wafanyabiashara wakubwa kuwabambikia kesi kesi uonevu utakatishaji fedha na uhujumu uchumi
 
Aisee! Kupitia michango humu nimeona kwa kiasi gani JF ina taarifa za uzushi. Nimesoma michango yote nimejiridhisha watu mlivyo wazushi wengi wenu. Namjua huyu bwana in and out. Itoshe kusema tusipende kuongea mambo tusiyoyajua.

Naandika kwa ufupi, mimi si muumini wa utawala huu, ila kwa uteuzi wa huyu bwana kwa nafasi hii ni jambo muafaka. Mwambe ana exposure, visionary na anaweza ku-offer kila kitu kinachohitajika. Ana mapungufu yake kama binadamu na mengine nisingependa niyaandike hapa- maana ni personal - hasa kati ya mimi, yeye na partnership ktk mambo binafsi. Kigezo cha mimi kuwa na tofauti naye si sababu ya kupindisha ukweli kumhusu. Ukweli lazima usemwe.
Wewe ni muumini wa utawala huu na ni mnufaika wa blackmail zote uonevu mbalimbali kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa na wadogo ndiyo maana umejitoa fahamu zote na kuona kila tuhuma za kweli ni uzushi, tofauti zipi kwake? Ukweli ukisemwa wewe unakuwa mnafiki mkubwa
 
Sidhani kama unaijua visiting TIC.
Godfrey Mwambe Amefanya reform kubwa sana pale TIC-Actually ataisaidia TIC akiwa Bungeni akishirikiana na Prof Mkumbo kwa sababu TIC ilionekana kama inakosesha TRA mapato kitu ambacho ni kunyume na Nia na sababu za uanzishwaji wa TIC.
Jamaa anaamini anachokijua na anakitetea.
Alipishana sana na TRA kuhusu kufunga makampuni kwa ajili ya kodi za zamani!

Huyu atasaidia kutengeneza mazingira Rafiki ya Biashara na viwanda.

He is a very right choice
TRA mpaka sasa wanaendelea kuwafungia wafanyabiashara Account zao kienyeji kwa njia haramu za kishetani kisha kuwabambikia kodi kubwa zisizo na kichwa wala miguu huku baadhi wakijitengenezea mazingira ya Rushwa au kuwakomoa wafanyabiashara kwa makusudi kwa wivu au fitna, yafaa TRA ifumuliwe isikwe upya au magufuli afuatilie wafanyabiashara wote waliofungiwa kampuni au Account zao awape nafasi za kuongea nao wampe vilio vyao dhidi ya mateso dhidi ya baadhi ya maafisa wa TRA na BOT
 
Alidhibiti vizuri uwekezaji kwa kuhakikisha wababaishaji na uwekezaji usiokua na tija kwa maendeleo haupati nafasi. Hao wababaishaji ndio wanaojidai wamekimbia.
Mbona hakuondoa kero ya TRA na BOT kuwapora wafanyabiashara na wawekezaji pesa zao? Kenya Uganda Zambia na sehemu zingine Duniani hukuti Bank kuu kuzuia pesa kuingia Nchini kwao na hata zikija zinaporwa kienyeji kama Tanzania
 
Rudiaxkusoma ulichoandika inawezakana akili zako huwa zinahamahama.
Mazuzu ya Lumumba ni mavivu ya kusoma ndo maana mnadanganywa danganywa kirahisi! Usingekuwa mvivu, ungeona conclusion niliyokitoa kwamba:-
Hawa watu wasio na exposure wanachoweza kufanya ni ku-attend Prospective Investors waliobisha hodi kwenye milango yao lakini sidhani kama wana ubavu wa kufanya "Investors Hunting" popote walipo duniani!!
Sasa kwa akili zako za ki-Lumumba, ni kazi ya waziri hiyo?!
JK pamoja na mapungufu yake mengi, alikuwa anafahamu sana nani akae wapi, na ndio maana akamvuta Julieth Kairuki ambae kabla ya uteuzi wake alikuwa kwenye banking sector huko South Africa na pia kuwa Project wa Private Public Partinership Capacity Building kwa nchi za SADC!
Julieth Kairuki alikuwa Waziri?

Na mwisho nikamalizia:-
Ukweli nilikuwa simfahamu kabisa huyo Mwambe lakini baada ya kuandika hayo hapo juu, nikalazimika kum-Google kidogo!!! Wallah JPM hayupo serious! Kumbe huyo jamaa kabla ya kuingia TIC alikuwa DC wa Manyoni?! Halafu ex-DC wa Manyoni ndie tulimpa dhamana ya kuvutia Foreign Direct Investment wakati hata akikutana na Diamond Platnumz tu lazima alikuwa anababaika!
Yaani kwa akili yako unaona hiyo hoja ni ya uwaziri hiyo wakati uwaziri wenyewe hajaanza kuutumikia?!

Bure kabisa!!
 
Viwanda havipo haviwezekani, huyo naye atabatizwa kwa moto muda ukifika.
Wawekezaji kila walipotuma pesa zao toka nje kwa ajili ya kuwekeza zilizuiwa BOT mpaka wawekezaji wanakata tamaa kuna mfumo wa ajabu Tanzania ni vigumu kumudu uchumi wa kati mda si mrefu Tanzania inarejea kwenye uchumi wa chini mno
 
He is the right person kabisa kwenye hiyo Wizara na atafanya Mageuzi makubwa sana. Hata TIC alifanya Mageuzi makubwa ya kishujaa kuanzia staffing n.k. Na kule Wizarani kwa Viwanda na Biashara atafanya Mageuzi mazuri tu. Ni Mchumi na uchumi anaujua. Ujue pia BOT amefanya kazi kabla ya kuwa na political posts.

Aliandaliwa. Narudia aliandaliwa. Hata kugombea Ubunge ni maagizo pia.

Ni mtiifu narudia ni mtiifu. Anapenda nchi yake. Ni mzalendo mnywa maji ya bendera. Usalama wa nchi ni lazima uanze kwenye sector muhimu. Place the right leaders from the Oven. To undertake multiple responsibilities???!!!@ Why not!!!???
Habari ndo hiyo sasa; hint moja kuwajua hawa jamaa wanakuwa hawana Umahiri wala Ufanisi wowote kwenye nafasi wanazoshika lakini huwezi kuona waachwe kwenye nafasi za Utawala, sanasana wanakuwa wanahama tu mara hapa mara pale...

Na hata mwonekano wao, nguo wanazovaa nk. hawako presentable wanavaa kipolisipolisi tu, sura ngumu!

Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni....mara vuuuuuumpuuu, Mkurugenzi wa TIC; na hapo hakuna alilofanya zaidi ya kuspy Wawekezaji au Wafanyabiashara wanapata wapi mitaji yao,halaf anareport kwa Jiwe,hakuwekwa pale kurahisisha Uwekezaji bali kukusanya taarifa za kiintelejensia za Wawekezaji

Kwa hiyo Mkuu.....akili za kuambiwa changanya na zako!
Uko vizuri
 
Sasa kawa waziri ni mda wake kurekebisha hizo kasoro zote kuanzia BOT, TRA na sekita zingine zote zinazohusiana na uwekezaji, amalize usumbufu wa hizo taasisi kwa wafanyabiashara na pia apige marufuku maafisa kuwapiga mikwara ya kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha uhujumu uchumi wafanyabiashara kisha kuwachukulia pesa zao kienyeji kwa njia haramu za kishetani
 
Hayo pia nimeyaona lakini naona info kama bado chache mno! Kwa mfano hapo Foreign Affair, nimeona alikuwa Mkurugenzi wa Biashara BUT for ONLY one year... kabla ya hapo alikuwa anafanya nini... sijapata!!

Aidha, hapo BoT pamoja na TTCL nimeona akiwa tu Mjumbe wa Bodi!!! Matumaini yangu mtu kuwa Mjumbe wa Bodi, basi kawahi kufanya kazi hapa na pale... hicho ndicho sijaona kikijitosheleza; unless nami ni-conclude kama wengine kwamba inaweza jamaa ni Afisa Kipenyo!!

Lusungo
Alifanya pia NIDA kwa muda mfupi. Na mabomu yake yakalipuka🤣🤣🤣😂😂😂😂
 
He is the right person kabisa kwenye hiyo Wizara na atafanya Mageuzi makubwa sana. Hata TIC alifanya Mageuzi makubwa ya kishujaa kuanzia staffing n.k. Na kule Wizarani kwa Viwanda na Biashara atafanya Mageuzi mazuri tu. Ni Mchumi na uchumi anaujua. Ujue pia BOT amefanya kazi kabla ya kuwa na political posts.

Aliandaliwa. Narudia aliandaliwa. Hata kugombea Ubunge ni maagizo pia.

Ni mtiifu narudia ni mtiifu. Anapenda nchi yake. Ni mzalendo mnywa maji ya bendera. Usalama wa nchi ni lazima uanze kwenye sector muhimu. Place the right leaders from the Oven. To undertake multiple responsibilities???!!!@ Why not!!!???

Uko vizuri
Sasa amekuwa waziri aende kurekebisha mapungufu yote ya BOT na TRA ikibidi aitishe mkutano mkubwa wa wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wote asikilize kero zao kwa uwazi apate kujua pa kuanzia kumaliza kero zote zilizopo kwenye mfumo wa fedha kodi na biashara kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom