Kipande cha barabara usichokipenda ukisafiri

Kipande cha barabara usichokipenda ukisafiri

umeniwahi mkuu, Segera to Wami kwangu ni janga, ni kipande kirefu na chenye kuchosha sana, Sehemu nyingine ni Minjingu to Arusha, Longido to Arusha, Gairo to Dodoma.
Hicho kipande unatakiwa kulala tu njia nzima, ukiwa idle daah unachoka hakuna hata vionjo njiani
 
Makutano ya barakara ua Keko VETA mataa pale na Nyerere Toad kuingia Posta asubuhi ni jau
 
Mzee si Sawa au sijakuelewa..Barabara ya Mbeya Tunduma ni raha tupu lami nzuri kasoro foleni Za Tunduma ukifika.Barabara Dume Kigoma Kasulu mpaka Nyakanazi...Hii mpaka ushibe Ndio usafiri
Kigoma kasulu kuna lami, labda unazungumzia Kasulu - Kibondo - Nyakanazi.
 
mwaka juzi mwezi wa tatu nipo na new force la dar-songea,maeneo ya kifanya madaba huko tukashangaa limeanza kufyeka miti,hatujakaa sawa tukaskia kishindo kikubwa TIIIIIIIII,akili zinakuja kukaa sawa naning'inia kwny mkanda kichwa chini miguu juuu,zile kona acha tuuu
Bora ulifunga mkanda maana
 
Nzega - Igunga. Dah, sikipendi hiko kipande balaa.
Wasalaam

Najaribu kupata uzoefu toka kwa wadau!

Binafsi hufanya safari za Mara kwa Mara kwa barabara! Katika safari zangu za mkoa wa Rukwa safari yangu huwa inaingiwa na ukakasi nikishafika Mbeya Mjini nikianza kuitafuta Tunduma.

Sijui wewe mdau kipande gani kinakutesa kutokana na Barabara kutokuwa rafiki na hali ya safari kwa ujumla
 
Kuna barabara moja nilisikia ikijadiliwa bungeni(kutoka UBENA to NGERENGERE Huko vijijini tena walisema imejengwa kiwango cha lami.....Siku nilienda maeneo ya huko nikakuta Malori yale makubwa Yamenasa yaani Ina Tope balaaaa! Hata bodaboda walipandisha nauli ......Mungu anawaona mjueeee!!
 
Back
Top Bottom