Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,435
8,254
Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Kinana anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzania ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.


View: https://www.youtube.com/live/3zH8m9Mt8ec?si=yGKfJn_tYKNShT0r

kinanaa.jpg

Abdulrahman Kinana-Makamu Mwenyekiti wa CCM


CHADEMA wametutuhumu CCM, Serikari na Rais kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa na kusahihishwa, lakini hatukubali kuzuliwa wala kushtumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ni ya kutunga. Kubwa walilofanya kwenye mizunguko yao ni kujenga chuki na mfarakano miongoni mwa Watanzania.

Hoja zao na ufafanuzi wa Chama cha Mapinduzi

1. Katiba na Sheria
Wanasema wanataka Katiba Mpya na kutushawishi katiba mpya ni muhimu - Mwaka jana 2023 tumekubali hoja ya katiba mpya, na wanatanzania wanaitaka katiba mpya, tunachobishania ni lini, wao wanataka ipatikane leo. Rais Samia wakati anandoa zuio la mikutano ya hadhara alikubali pia kuhusu suala la katiba. Haya mambo yanahitaji muda na tafakuri, lakini wenzetu wanasema hapana, katiba inahitajika sana.

Katiba yetu imepokea mabadiliko mara 14, na ukitazama madailiko hayo mara nyingi yalilenga siasa, madaraka na uchaguzi, hata msukumo wa sasa wa CHADEMA lengo lake ni uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi na Mamlaka ya Rais
Serikali imetunga sheria tatu za uchaguzi ambazo zimepita bungeni na Rais kutia saini, sheria ambazo zilitolewa maoni na wadau mbalimbali ikiwemo mpaka bungeni kwa siku nne, ambapo hoja za msingi zilikubaliwa lakini CHADEMA hawakuridhika, bado wasema Rais asihusishwe kwenye uchaguzi wa viongozi wa Tume, sijaona nchi ambayo Rais hahusishwi kwenye maamuzi mfano China, India, Kenya, Afrika Kusini kote Rais anakuwa na mamlaka fulani juu ya Tume. Hakuna Tume ya Uchaguzi Duniani ambayo Rais hana Mamlaka.


CHADEMA walitaka suala la Katiba liwe la CHADEMA na CCM kama chama kikuu cha upinzani na chama tawala, hili haliwezi kufanyika, sababu katiba sio suala la vyama hivi viwili pekee.


Kwa sheria hii nawahakikishia Tume hii itakuwa Huru na kufanya kazi kwa uadilifu, Mweyekiti, Makamu na watendaji watakula kiapo kufanya hiyo kazi, labda kama tunataka malaika kufanya hizo kazi, lakini kazi hizi lazima zifanywe na binadamu.


Katiba na Sheria ya Uchaguzi siyo njia pekee ya kushinda uchaguzi, Sera nzuri, Kukubalika kwa chama chako, Kukubalika wagombea wako na kujipanga ipasavyo kwenye uchaguzi kuna mchango mkubwa sana kwenye ushindi.



2. Muungano
CHADEMA wamekuja na hoja hizi;
  • Zanzibar ni ndogo wakati ina wabunge wengi
  • Rasi samia ni Mzanzibari hana nia njema na sisi - uongo ukirudiwa rudiwa usiposahihishwa unageuka kuwa ukweli, ndicho wanachotaka kuaminisha Watanzania, Watanznia kataeni sumu hiyo inayojaribu kujengwa miongoni mwenu. Kama zanzibar ingekuwa na wnanchi milioni 40 au 60 sawa na sisi je, swali hilo lingekuja? Jibu ni hapana, swali linakuja sababu wako 1,400,000!

Wabunge hawaendi bungeni sababu ya idadi ya watu, wanaenda kwa uzito wa hoja
Wanasahau muungao huu ni wa nchi huru, tumeunganisha nchi mbili, na huu Tunakubali na kukiri hizi ni nchi mbili tofauti zilizoamua kuungana kwa hiyari, zikiwa na ukubwa ardhi tofauti, ukubwa wa uchumi tofauti na ukubwa wa watu tofauti, tukiungana lazima tukubali kuwe na uwakilishi wa kutoka pande zote mbili. Usipime watu kwa udogo wao na ukubwa wao, wapime kwa walivyo, walikuwa huru tukaungana nao. Nchi ya Seychelles wako 100,007 wana wabunge 35, Lesotho ina watu 2,300,000 wana wabunge 130, lakini ndivyo walivyojipanga, Switzerland ina watu 1,700,000 wabunge wa 246 sawa na Tanzania ambapo sisi ni milini 60 na wabunge 300, ndivyo walivyokubaliana uwakilishi wao, Sweden 10,500,000 wana wabunge 349 kwanini hatuwaulizi? Kwahiyo hoja hii ya CHADEMA haina maana, ni hoja ya kuzua, kukotroga vichwa vya watu, kuchanganya watu, kuleta, uhasama, uchochezi. Haya yote wanayoongea hayaondoi umasikini wala kuleta maendeleo, basi tu tuvurugane, mimi naamini muungano huu utadumu.


Ubunge hauwakilishi idadi ya watu, ubunge unawakilisha hoja, matakwa ya watu, maoni, na mahitaji ya wnanchi. Wabunge hawaendi bungeni sababu ya idadi ya watu, wanaenda kwa uzito wa hoja, kuzungumza matatizo ya wananchi, kuzungumza juu ya shida za nchi yetu sio idadi, idadi sawa itafikiriwa lakini sio msingi pekee. Tukatae kugawanywe, waje na hoja za mashiko kuondoa umasikini

3. Kuligawa taifa katika majimbo
Tukishakubali hilo baadaye watasema kila kabila lipate jimbo liwe mkoa, baadaye watasema waislamu na wakristo wawe na eneo lao, mambo huwa yaanza hivi hivi, kuwagawa watu, moja ya sifa ya nchi yetu ni ummoja wa kitaifa, watanzania endeleeni kuikataa hoja hii.

Duniani nchi nyingi hazina majimbo zina mfumo wa umoja, inaitwa unitary system of government, mfumo wa serikari ya umoja.

CHADEMA wanataka kujenga uhasama miongoni mwetu, Watanzania nawasihi tukatae mgawanyiko.

4. Hoja ya Rais Samia na Uzanzibari
Kila kitu kipo kwenye Katiba, mgombea mwenza lazima atoke Zanzibari, kipi cha ajabu? Rais ipo kwa Msingi wa Katiba, hakwenda mwenyewe. Tusisikilize hoja za reja reja, hoja za msimu zinazotaka kutugawa. Mkiwasikiliza sana hawasemi watafanya nini, wanasema kasoro zetu.


Rais Samia ameleta uhuru nchini
Rais huyu wanayemsema, Rais Samia na mtakubaliana na mimi ndiye aliyeleta uhuru ulioko sasa hivi nchini, uhuru wa kusema, kushutumu, kuandamana, uhuru wa mikutano ya hadhara, nina hakika watajibu watasema lakini ipo kwenye katiba, kwani huko nyuma waliponyimwa katiba haikuwepo? Walikwenda barabarani? Katiba ilikuwepo, uhuru huo ulikuwepo lakini ulipigwa marufuku na hawakwenda barabarani. Sasa amekuja kiongozi muungwana amesema katiba inaruhusu na mimi naondoa kifungo kile mlichokuwa mmefungwa kuzuiwa kutumia uhuru wenu halafu wanasema hapana, unajua hii ipo kwenye katiba siyo kwamba ameturuhusu. Leo hii akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?


Rais ametoa uhuru wa habari, kila mtu aandika leo, andika unachotaka, ukweli, uongo watu wanaandika, haki za raia sasa hivi zina nafasi kubwa kuliko wakati wowote, tume ya haki jinai juu ya kuboresha haki za watanzania na kuhakikisha watanzania wanatendewa ipasavyo, haya yote yanaitwa maendeleo ya watu na jambo la msingi ni uhuru. Rais amejenga madarasa 20,000 nchi nzima, bwawa la Mwl. Nyerere limekamilika kwa 96%, SGR treni imefika mpaka Dododma, viwanja vya ndege vikubwa vya kimataifa na hajafanya kitu hata kimoja Zanzibar lakini wanalalamika, hoja nyepesi lakini imejaa fitna.


Hitimisho la Kinana
Lazima tukubali, Rais wetu anajitolea sana, Rais anajituma, tukatae kugawanywa na kufarakanishwa, watu wanatafuta uongozi CCM, CHADEMA ACT, CUF, tutafute uongozi kwa hoja zinazosaidia wananchi, zinazoleta maendeleo, zinazopunguza umasikini, tusitafute hoja rahisi za kuchonganisha watu, kufarakanisha watu, za kuvunja umoja wetu.
 
Makala na Nchimbiwazee wa "kutatua kero kisayansi" wako wapi ...

Tulitegemea wao ndio wamjibu Lissu.
Hayo magarasa wewe ndiyo unayaamini! CCM hivi sasa haina watu imebaki na manyangarakasha tatizo walitegemea dola kuwa ndiyo inayojibu kupitia kesi za mchongo, vijitu vijanja kama Lucas Mwashambwa ndivyo vimekuwa vinanajibu tofauti na hoja kisha vinakimbilia eti wametukana!
 
Masikini Comrade amebaki peke yake kama kisiwa kisicho na wavuvi, CCM ni hivi sasa ni sawa na kasha tupu baada ya Mangula kuchoka na kukabidhi mitambo kwa Nape! Ukimuangalia Kinana unamuona kuwa hana mtu anayeweza kuongea naye lugha moja wakaelewana ndani ya chama.
Wale wanaojiita Watoto wa Mjini wao ni kupiga WANZUKI tu sasa Lumumba kimenuka
 
CHADEMA wametutuhumu CCM, Serikari na Rais kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa na kusahihishwa, lakini hatukubali kuzuliwa wala kushtumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ni ya kutunga. Kubwa walilofanya kwenye mizunguko yao ni kujenga chuki na mfarakano miongoni mwa Watanzania.
Kwani nani hajui kuwa tunaongozwa na mzanzibari?
Nani hajui kuwa nchi inauzwa kidogokidogo kwa waarabu?
 
Back
Top Bottom