Kinana asome alama za Nyakati, wana CCM hawamwelewi

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,398
3,907
KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WATENDAJI

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametaka viongozi na watenaji serikalini kuzingatia kanuni, sheria, utaratibu na Katiba wanapowakosoa watendaji.

Amesema ni vyema wakajifunza kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na kuwa na uwezo na mamaka lakini hajawahi kusimama hadharani na kuvunja haki ya utu wa mtu hususan watendaji katika ngazi mbalimbali.

Kinana aliyasema hayo jana Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM, viongozi na wananchi alipofungua jengo la ofisi za CCM la wlaya hiyo.

“Nataka kufafanua hili ambalo nimezungumza katika Mkutano Mkuu hapa Bukombe, ni kwamba viongozi wasimamie watendaji serikalini, wasimamie sheria, kanuni na utaratibu lakini si vizuri kuwasema hadharani na kuwafedhehesha watendaji wa serikali.

“Mfano mzuri wa kuigwa ni wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani hatujawahi kuona akisimama hadharani akmfedhehesha mtendaji serikalini, kwa sababu yeye ni muumini wa utawala bora, unaozingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu,” alisema.

Kinana alsisitiza watendaji wote wa serikali wanasimamiwa na kanuni, sheria, katiba na utendaji serikalini.

1702531140891.jpg
1702531059872.jpg
 
Hao njaa tu wakikosa buku tano lazima wafure....yani ukiitwa kwenye mikutano yao kengele ya kwanza kichwani leo nabadilisha Mboga

Chadema ndo imebaki na wafuasi wa KWELI yaani chama imo ndani ya moyo mpaka kwenye Damu....

Na nauli zimekayibong sasa ule wimbo wa fronti kwa fronti mtamujeee ....unaenda kula Mwaka mpyaa kwenu na maumivu bado maloope inawasubiri ...
 
KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WAT
Huo ndio ukweli!

Kwenye utendaji kuna kitu kinaitwa Proffessionalism.

Kisiasa unaweza ukadhani mtendaji ana makosa...lakini kumbe siyo!

Na Watendaji huchapwa na Kalamu na siyo kwenye podium!

Uko mtindo wa Mwanasiasa ili kuonekana anatenda vema ni Lazima amuumbue mtendaji...of course kwenye macho ya wapiga kura ni credit lakini kuanzia tu hapo morale ya Mtumishi ktk utendaji inakufa papo hapo!

Unakuwa na waigizaji tu kwenye maeneo ya kazi badala ya Watendaji..!

Makamu alikuwa very right!

By the way huyu mzee akiongea kitu usipoelewa basi tena!
 
Makamu kila mara akisimama lazima amuongelee msemaji.

Ngoja tuone panapoishia.

Tulisikia pia kule Arusha.
 
Msemaji anamambo ya kipuuzi sana ndio maana kila kitu kikawekewa utaratibu na kanuni ukutaka kufuata mihemko ya hawa raia ambao wengi wao ni wapenda majungu na chuki dhidi ya watumishi wa umma utaonea sana watumishi ambao hawana cha kukufanya ukiwa kwenye jukwaa.

Sio ustaarabu naheshima ya kiuongozi kupigia kelele watendaji kwenye majukwaa ya kisiasa, huo sio utaratibu, hata mke wako nyumban kuna mambo huwezi muuliza mbele ya watoto hata kama kakosea mbele yao
 
Kimepasuka Makonda Anataka Anachoagiza Watendaji Wafanye
Kinana Naye Anaponda Ngoja Tuone
Concern ya makonda ni nzuri ila utaratibu alio anza nao sio mzuri kabisa anajifichia kwenye mgongo wa chama kujiimarisha yeye binafsi kisiasa.
 
Msemaji anamambo ya kipuuzi sana ndio maana kila kitu kikawekewa utaratibu na kanuni ukutaka kufuata mihemko ya hawa raia ambao wengi wao ni wapenda majungu na chuki dhidi ya watumishi wa umma utaonea sana watumishi ambao hawana cha kukufanya ukiwa kwenye jukwaa.

Sio ustaarabu naheshima ya kiuongozi kupigia kelele watendaji kwenye majukwaa ya kisiasa, huo sio utaratibu, hata mke wako nyumban kuna mambo huwezi muuliza mbele ya watoto hata kama kakosea mbele yao
Kinana akiwa katibu aliwaita mawaziri kuwa mizigo.

Mda wake huyu akalee wajukuu. tunahitaji mchaka mchaka.
 
KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WATENDAJI

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametaka viongozi na watenaji serikalini kuzingatia kanuni, sheria, utaratibu na Katiba wanapowakosoa watendaji.
Samia wa utawala bora ni yupi uyo,huyu aliyesema katiba ni kijitabu!!!!?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Kinana akiwa katibu aliwaita mawaziri kuwa mizigo.

Mda wake huyu akalee wajukuu. tunahitaji mchaka mchaka.
Mchakamchaka usio heshimu mamlaka ya wengine nao ni ujinga na upumbavu huwezi kuendesha nchi kwa kutegemea fikra za vijana aina ya makonda hiyo itabaki kuwa nchi ya kusadikika
 
Huo ndio ukweli!

Kwenye utendaji kuna kitu kinaitwa Proffessionalism.

Kisiasa unaweza ukadhani mtendaji ana makosa...lakini kumbe siyo!

Na Watendaji huchapwa na Kalamu na siyo kwenye podium!

Uko mtindo wa Mwanasiasa ili kuonekana anatenda vema ni Lazima amuumbue mtendaji...of course kwenye macho ya wapiga kura ni credit lakini kuanzia tu hapo morale ya Mtumishi ktk utendaji inakufa papo hapo!

Unakuwa na waigizaji tu kwenye maeneo ya kazi badala ya Watendaji..!

Makamu alikuwa very right!

By the way huyu mzee akiongea kitu usipoelewa basi tena!
Watendaji wepi hao,hawa wanaotujengea mapagale kwa Milioni 800!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Msemaji anamambo ya kipuuzi sana ndio maana kila kitu kikawekewa utaratibu na kanuni ukutaka kufuata mihemko ya hawa raia ambao wengi wao ni wapenda majungu na chuki dhidi ya watumishi wa umma utaonea sana watumishi ambao hawana cha kukufanya ukiwa kwenye jukwaa.

Sio ustaarabu naheshima ya kiuongozi kupigia kelele watendaji kwenye majukwaa ya kisiasa, huo sio utaratibu, hata mke wako nyumban kuna mambo huwezi muuliza mbele ya watoto hata kama kakosea mbele yao
Watumishi wepi hao,hawa wanaotujengea madaraja ya kamba na waya kwa Milioni 200?
Wacha wakaangwe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WATENDAJI

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametaka viongozi na watenaji serikalini kuzingatia kanuni, sheria, utaratibu na Katiba wanapowakosoa watendaji.
Ccm itaendelea kutawala mpaka pale watakapo anza kutoa elimu sahihi kwa raia ili watu wapate uelewa na utatari wa kupambania mageuzi na haki zao,........kwa elimu duni hi sidhani kama tutakua po na upinzani kwa miaka kaďha.
 
Basi tuwategemee vijana kama wakina Nape watuvushe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Tatizo ni usukuma ndio unao waletea shida, utaratibu ulio tumika na magufuli na ulianza kutumika na makonda sio uongozi bora bali ni udhalilishaji wa watumishi viongozi.

Huwezi kumuita mkuu wa mkoa "njoo hapa kimbia" hiyo sio heshima kwa sababu yeye ni kiongozi ana watu wanasubiri maelekezo yake huwezi kumuita kama mtoto wako ni udhalilisha ule ila wajinga wajinga ndio walikuwa wanapenda kutokana na kukosa kwao elimu na kupenda kwao majungu
 
Kinana ni mwana CCM kiongozi wa genge chafu ndani ya CCM.
Kinana ni mwizi na mbadhirifu kama wengine tuiowafahamu mfano wa Makamba Jr.
Vema Kinana akajitambua na kufunga Domo lake kabla hayajamkuta ya kumkuta.

Hii sio awamu ya ujinga!
 
Kinana pamoja na ufisadi wake ila ana AKILI, anayo yaongea yana mantiki kubwa sana ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom