Kinana akemea makada wanaowadhalilisha watendaji wa Serikali majukwaani

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana amekemea tabia ya viongozi na makada wa CCM kuwadhalilisha watendaji wa Serikali kwenye majukwaa ya kisiasa.

Pamoja na kukiri kuwa chama tawala kinaisimamia Serikali na kuishauri, Kinana amesema si vyema viongozi na makada wa chama tawala kuwadhalilisha watendaji wa Serikali.

Kinana ameyasema hayo leo huko mkoani Geita na kuwataka viongozi na makada wa CCM kumuiga Rais Samia Suluhu Hassan ambaye hajawahi kuwadhalilisha watendaji wa Serikali majukwaani pamoja na kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa.
 
Katibu mwenezi ndugu Paul Makonda akiwa jukwaani

1702490965895.png

1702491168682.png
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Abdurahman Kinana amekemea tabia ya viongozi na makada wa CCM kuwadhalilisha watendaji wa Serikali kwenye majukwaa ya kisiasa.

Pamoja na kukiri kuwa chama tawala kinaisimamia Serikali na kuishauri, Kinana amesema si vyema viongozi na makada wa chama tawala kuwadhalilisha watendaji wa Serikali.

Kinana ameyasema hayo leo huko mkoani Geita na kuwataka viongozi na makada wa CCM kumuiga Rais Samia Suluhu Hassan ambaye hajawahi kuwadhalilisha watendaji wa Serikali majukwaani pamoja na kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Makada wamesikia, ila sijui kama wamejifahamu kama wanafunzwa kuwa na adabu.
 
Makamu mwenyekiti anakemea wakati mwenyekiti aliyemteua yupo kimya, ushauri wake usipofuatwa nae aanze kulalamika kama JK, hawa wazee wanateseka sana wangepisha huko chamani kwao damu changa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom