ila Zitto aliwahi kuchukua ela na cheki kwa CCM ili aimalize CHADEMA? Je Zitto anatishia kuua watu? Je, Zitto anauza utu wake? Je, Zitto ni mnafiki? kama ndivyo kwanini kamati kuu haikumvua nyadhifa zake na kumshitaki kwa makosa hayo? Kwanini makosa ya Zitto yaliyotangazwa na Lissu kwa niaba ya chama si hayo ya kutumika na CCM, kuchukua fedha toka CCM na TISS, na kuuza majimbo kwa CCM? Kwanini chama kiliendelea kukanusha kuwa sababu za kumvua nyadhifa Zitto si hizo hata mara baada ya Zitto kusema WARAKA haukumvua nyadhifa zake? Je, tukisema hizo ni propaganda zenye lengo la kuumpa mbwa jina baya ili mpate kuhalalisha kitendo cha kumuua huyo mbwa tutakosea?
Zitto atakuja kuonekana shujaa kama tuhuma za usaliti dhidi yake ni propaganda za kum-maliza kama vile uhaini kwa Mandera ulivyokuwa ni propaganda za Makaburu, na kitendo cha Lissu kukana hizo tuhuma kuwa si sababu za Zitto kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni kiashiria tosha kuwa hizo tuhuma ni propaganda za maadui wa Zitto, na tutasikia mengi kabla ya Zitto kufukuzwa chadema RASMI.
Hiki anachofanyiwa Zitto ni dhambi kama itakuwa ni njama za kummaliza, na haitawaacha salama wale walioifanya, ni sawa na kula nyama ya mtu, leo utakula familia za majirani, ukiwamaliza hao utaanza kuila familia yako. Utaanza na beki tatu, kisha watoto na utamalizia kwa mke. Hili likija kutokea nyinyi mabeki tatu mnaoshinnda mitandaoni mtatamani ardhi ipasuke muingie mjifiche, lakini ardhi haitapasuka na mtaliwa huku mwajiona.
Pia eleweni hadi sasa kuna baadhi ya watu wameshastuka, iweje kila mwenye kuhoji utendaji kazi wa Mbowe aitwe msaliti? Kwanini kila mwenye kuhoji matumizi ya fedha aonekane msaliti? Kwanini Chacha Wangwe aliandamwa ikiwa hoja zake hadi sasa hazijajibiwa? Kwanini watu wanaishiwa kuitwa wasaliti bila hoja zao kujibiwa au kufanyiwa kazi?
Tuache chuki na kuzushiana, kwani hazitujengi hata kidogo na tabia hizi zinafanya chama kuonekana mali ya watu badala ya mali ya wanachama. Tuhuma zisizothibitishwa ni uzushi, uzandiki na siasa chafu zenye lengo la kutimiza malengo binafsi badala ya chama.
Njano5.
0655345394