GE2025 Zitto Kabwe: Mkinichagua bei ya Simenti itashuka Kigoma

GE2025 Zitto Kabwe: Mkinichagua bei ya Simenti itashuka Kigoma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewaambia wanakigoma wakimchagua kuwa Mbunge atashusha bei ya Simenti ambayo inazalishwa katika Mkoa huo kutokana na bidhaa hiyo kuuzwa bei sawa na Simenti inayotoka Dar es salaam.

Zitto Kabwe amesema hayo wakati akiendelea kunadi sera zake Kata kwa Kata kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.

Yeye kama nani?

Pia Soma: GE2025 - Zitto nyumba kwa nyumba kuzisaka kura za ubunge
 
Duh........aise hii hapana atashusha vipi bei ya saruji kimazingara Dang'ote mwenyewe alipojaribu kuuza kwa 10,000/- kwa mfuko vita aliyokumbaba nayo ndo Zito aje kushusha jamani hebu wawe na huruma kwa wananchi maskini waache utapeli wa kisiasa.
 
Kiuhalisia cement bongo ilipaswa kuuza 10,000, hapo Nigeria cement ni tsh 11,000 sawa na naira 6800 tu

Walimwekea dangote urasimu tu, hii nchi kila mahala ni upigaji tu!
 
Kiuhalisia cement bongo ilipaswa kuuza 10,000, hapo Nigeria cement ni tsh 11,000 sawa na naira 6800 tu

Walimwekea dangote urasimu tu, hii nchi kila mahala ni upigaji tu!
Nashukuru kwa kuliweka sawa hili wanasiasa ndo chanzo cha yote haya fikiria watu wana hisa zao pale Twiga Heidelberg ( Wazo) Dang'ote alipoanza uzalishaji na bei zake kufikia Tshs 10,000/- kwa mfuko kulitokea mvurugano maana wengi walihamia kwenye saruji ya Dang'ote hata sasa mikoa ya Kusini wanatumia kwa wingi saruji hiyo akaanza kupigwa vita kubwa mpaka kumkatisha tamaa yeye mwenyewe maana uwekezaji wake ulikuwa mkubwa sana kwenye kile kiwanda. Nia yake saruji iuzwe kwa bei ya chini kabisa
 
Mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Mjini Kupitia chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameahidi kushughulikia bei ya simenti ili iweze kupungua na kusaidia jamii ya Wana Kigoma kujenga nyumba bora.


 
Maisha yanaenda kasi sana leo baba levo anamlaza na viatu ZZK
 
Back
Top Bottom