Kinachoendelea Kigoma "KARIBU SHUJAA ZITTO KABWE".

Status
Not open for further replies.
Ikiwa bado siku moja kabla ya Zitto hajatua hapa Kigoma kuja kuzungumza na Wananchi wake,kutoa kile Wanakigoma wanakisubiria kwa hamu sana kusikia toka kwa Shujaa..Mwanao Zitto Zuberi Kabwe.

Hapa Kigoma Kasulu,Mwandinga na Kigoma Mjini Tax,Bodaboda zinapepea matangazo ya KARIBU SHUJAA ZITTO KABWE TAR.21.12.2013
Heka heka za hapa na Pale zinaendelea huku maandalizi ya Mikutano yote ikiwa imekamilika kwa hisani ya Wananchi wa Kigoma.
Moja ya Bango ni hili hapa.

attachment.php

Safi sana
 
Kama atawahusisha ccm kwenye mapokezi yake atajisababisha maadui zaidi ndani ya chama chake.kila la heri zitto huko kigoma. M4c daima!
 
teh teh, ndoa ya mbowe inawasaidia nini wanachadema na watanzania? Huu ni upofu wa fikra!

Teh teh teh teh teh sisi tunaongelea ukombozi wa pili lakin jamaa yeye anaongelea ndoa ya mbowe. Kwel jamaa ni kipofu wa fikra.

"Nothing is more terrible than to see ignorance in action"-( Von Goethe)
 
Wastage of time,tumeshawasikia CDM wanachosema juu ya zito,na tumesikia Zito anachosema juu ya CDM.wote wanatakiwa wabadilike,asiyeweza kufanya kazi na wenzie asipoteze muda wetu kujadili stori zake.shujaa gani anaenda kujenga chama peke yake kila siku?wenzie wanapigwa mabomu,wanaumizwa yeye anasubiri kugombea vyeo kila kona.oparesheni za chama haonekani,vikao hahudhurii,ccm ndio marafiki zake wakubwa.halafu anataka apewe UENYEKITI na AGOMBEE URAIS.Huyo ndio shujaa??Hizi ni tamaa,cdm wasimpe nafasi tena labda abadilike na jamii ione kwa vitendo.

Alishasema chama akijengwi na matukio
 
Kwa taarifa zaidi, Maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kurushwa live kwa mkutano huo na kituo cha startv huku uratibu mzuri ukiwa chini uv-ccm.

Taarifa Rasmi ni kwamba maandalizi yote yanafanywa na CCM.


Huyu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini anayetokana na chama cha Chadema, hivyo bila shaka hilo jimbo lina wana chadema ccm na wengineo. Kama baadhi ya wana ccm ni sehemu ya maandalizi kwa mbunge wao sioni ubaya wowote. Hata JK akitembelea jimbo linaloongozwa na Chadema wanaompokea si CCM pekee bali hata wana Chadema ikiwa pamoja na Mbunge. Tujifunze ukweli badala ya kuchochea mgawanyiko kila siku.
 
Kwa taarifa zaidi, Maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kurushwa live kwa mkutano huo na kituo cha startv huku uratibu mzuri ukiwa chini uv-ccm.
Brother ata wewe unachuki na Zitto,au sababu unaisiwa kuwa upande wake,kwahiyo unaandika kuwafurahisha Chadema chumbani
 
Huyu ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini anayetokana na chama cha Chadema, hivyo bila shaka hilo jimbo lina wana chadema ccm na wengineo. Kama baadhi ya wana ccm ni sehemu ya maandalizi kwa mbunge wao sioni ubaya wowote. Hata JK akitembelea jimbo linaloongozwa na Chadema wanaompokea si CCM pekee bali hata wana Chadema ikiwa pamoja na Mbunge. Tujifunze ukweli badala ya kuchochea mgawanyiko kila siku.

Tuendelee kuwatoa Utumwani
 
Kama zzk ni maarufu zaid ya CHADEMA CHAMA MAKIN yanin ang'ang'anie kuwa chadema si atoke naanzishe chama Chake, CHADEMA NI CHAMA KILICHOBEBA MATUMAIN YA WATANZANIA WOTE. CHADEMA NI MPANGO WA MUNGU.!
 
Pls usimtukane Mandela kiasi hiki.Muache apumzike kwa Amani

Mandela hajawahi kuchukua hela kwa makaburu.Hajawahi kuchukua cheki.Hajawahi kuwa na chuki na kutishia kuua watu.Hajawahi kuuza utu wake na watu wake.Hajawahi kuwa mnafiki

Please ,spare us with your ignorance!

ila Zitto aliwahi kuchukua ela na cheki kwa CCM ili aimalize CHADEMA? Je Zitto anatishia kuua watu? Je, Zitto anauza utu wake? Je, Zitto ni mnafiki? kama ndivyo kwanini kamati kuu haikumvua nyadhifa zake na kumshitaki kwa makosa hayo? Kwanini makosa ya Zitto yaliyotangazwa na Lissu kwa niaba ya chama si hayo ya kutumika na CCM, kuchukua fedha toka CCM na TISS, na kuuza majimbo kwa CCM? Kwanini chama kiliendelea kukanusha kuwa sababu za kumvua nyadhifa Zitto si hizo hata mara baada ya Zitto kusema WARAKA haukumvua nyadhifa zake? Je, tukisema hizo ni propaganda zenye lengo la kuumpa mbwa jina baya ili mpate kuhalalisha kitendo cha kumuua huyo mbwa tutakosea?


Zitto atakuja kuonekana shujaa kama tuhuma za usaliti dhidi yake ni propaganda za kum-maliza kama vile uhaini kwa Mandera ulivyokuwa ni propaganda za Makaburu, na kitendo cha Lissu kukana hizo tuhuma kuwa si sababu za Zitto kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni kiashiria tosha kuwa hizo tuhuma ni propaganda za maadui wa Zitto, na tutasikia mengi kabla ya Zitto kufukuzwa chadema RASMI.


Hiki anachofanyiwa Zitto ni dhambi kama itakuwa ni njama za kummaliza, na haitawaacha salama wale walioifanya, ni sawa na kula nyama ya mtu, leo utakula familia za majirani, ukiwamaliza hao utaanza kuila familia yako. Utaanza na beki tatu, kisha watoto na utamalizia kwa mke. Hili likija kutokea nyinyi mabeki tatu mnaoshinnda mitandaoni mtatamani ardhi ipasuke muingie mjifiche, lakini ardhi haitapasuka na mtaliwa huku mwajiona.

Pia eleweni hadi sasa kuna baadhi ya watu wameshastuka, iweje kila mwenye kuhoji utendaji kazi wa Mbowe aitwe msaliti? Kwanini kila mwenye kuhoji matumizi ya fedha aonekane msaliti? Kwanini Chacha Wangwe aliandamwa ikiwa hoja zake hadi sasa hazijajibiwa? Kwanini watu wanaishiwa kuitwa wasaliti bila hoja zao kujibiwa au kufanyiwa kazi?

Tuache chuki na kuzushiana, kwani hazitujengi hata kidogo na tabia hizi zinafanya chama kuonekana mali ya watu badala ya mali ya wanachama.
Tuhuma zisizothibitishwa ni uzushi, uzandiki na siasa chafu zenye lengo la kutimiza malengo binafsi badala ya chama.

Njano5.
0655345394
 
Hata mimi nyumbani kwetu ni shujaa! kama vipi mwambieni aanzishe chama chake cha kigoma tu tena mwandiga ha ha ha ha ha ha ha ha ha..??????
lile pumbafu lililokua linamkashi ben saanane lisome hapa
[h=1]Zitto na Demokrasia[/h]Zitto na Demokrasia

[h=2]Posts Tagged ‘Ben Saanane’[/h][h=2]PRESS RELEASE: ‘SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’-SIO KWELI[/h]with 74 comments
‘SIRI YA KUUAWA ZITTO’
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.
–
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013


 
Alishasema chama akijengwi na matukio

Mbona TANU na sasa CCM inabebwa na kuaminika na watanzania kwa sababu ya tukio la kutuletea uhuru,na uadilifu wa Nyerere.SIDHANI KAMA NI SAHIHI,Lazima chama kifanye mambo ya kijasiri ktk kutetea wananchi ili kiaminike na kujijenga.anyway,ni mtazamo wake tu,lakini huwezi kukaa ukisubiri kupewa nchi uiongoze bila kuwaonyesha watu stability yako wakati wote wa mapambano.
 
hata mandela aliitwa msaliti kwa kuwa tu alitaka uhuru na haki sawa kwa wote yaani waafrika na wazungu ila mwisho wa siku aliibuka shujaa. Zito kukubalika na cdm na ccm sioni kama ni tatizo kwani tunahitaji kiongozi atakayetuunganisha wote kwani siasa si uadui, upinzani haimanishi kuwa watu wa vurugu wasiotii mamlaka na vyombo vya usalama hadi kufikia hatua ya kusababisha mauaji. Zito anafanya siasa za kistarabu zenye lengo la kuikomboa tanzania toka mikononi mwa mkoloni mweusi(ccm). Na ili cdm ichukue dola inabidi ibadili mtazamo wa namna inavyoendesha siasa zake, na mtu pekee anayeweza kufanya kazi hiyo ni zzk.

Unakosea sana.JITIBU KWANZA UGONJWA WA KUMTEGEMEA MTU.Kama wewe pia ni mshauri wa Zitto basi niseme unakula hela yake bure kwani humsaidii kufikia malengo yake vizuri.Usimlinganishe Mandela na Zitto.tofautisha pia nyakati na mahala.Kama Zitto alisema atakuwa wa mwisho kutoka chadema basi nadhani atakuwa wa kwanza kutoka Chadema.Haya anayoyafanya ya kutaka kushindana hatoweza kwa mtazamo wangu.na niseme mapema kwa mwenendo ninaouona sasa, Zitto kadanganywa vibaya kuwa akitoka Chadema ataendelea kuwa shujaa unayemwona leo.Historia ni jambo zuri sana katika maisha.Waulize kina Lamwai na Mrema.Kumbukeni umaarufu wake ni kutokana na chadema na si CCM wanaomdanganya. Naamini akifukuzwa Chadema leo itabaki kuwa historia.

Siasa za siku hizi hususani Tanzania usizilinganishe na Afrika Kusini enzi za Mandela.Pitia pia historia ya Julius Malema kabla ya kuja kwa kina Kabourou. Zitto "kasingiziwa" kutaka kuua Chadema kupitia TISS na CCM. Ili kuonesha kweli kuwa kaonewa licha ya mambo mengine basi wakati huu angeonesha kuwa hayupo na hao TISS na CCM.Badala yake tunaona kuwa wanaoandaa mikutano na kuilipia kupitia LIve zao kwenye media ni CCM hao hao.Hivi hata kama viongozi wake "ni too local" na wana elimu "ndogo", watashindwa kujua ukweli huu unaonekana wazi wazi?
Hebu nyie mashabiki wake kuweni wa kweli. Msitake kuiga maneno ya Yusufu Makamba kuwa JK ni maarufu kuliko CCM.Huu ni uwongo na kutaka kujificha kwenye kichaka cha mti wa uyoga.Siku zote Chama ni maarufu kuliko mtu. Rai yangu kwenu ni kuwa ngonjera hizi zitapelekea Zitto kutafuta chama kingine bila kupenda.Na hili linafuata.Akishafukuzwa uanachama mtamshauri aende mahakamani ili awe kama Kafulila na Mohamed mbunge wa CUF.

Hapa pia mnadhibitisha kuwa watu wa Kigoma mnahongeka kirahisi sana.Kabouru naye aliishia kumfuata Makamba huko Kilimanjaro na kuvishwa kofia ya kijani.Leo anasikika tena.Na najua baada ya 2017 hatakuwa tena na cheo alicho nacho. Mmesahau yaliyotaka kumpata Sitta huko huko CCM hadi akaambulia kuukosa uspika kwa mara ya pili.Ngoja mfanye hayo mnayofanya baadae mtakuja kujua kuwa mlifanya makosa kumshauri huyo mnayemwona shujaa leo. NI AFADHALI CHADEMA IKAKOSA KUINGIA IKULU LAKINI IKAWA NA NIDHAMU YA CHAMA.CHAMA HAKIPASWI KUMTEGEME A MTU BALI KITEGEMEE MISINGI ILIYOJIWEKEA.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom