Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

hata ukurasa wa abdala ulega facebook analalamika hivyo hivyo inaweza kuwa kweli
 
Hakuna cha hisia, ni mambo yaliyozungumzwa na mikakati imeonekana wazi, maamuzi yanaweza yakafanyika, yamefanyika ama yatafanyika. Ila na wahusika wamejipanga na wako Dodoma kuzuia, na jana na leo wamekua na vikao vya kuzuia maamuzi hayi yasifanyike, ikiwa ni pamoja na kutaka kuonana na Mwenyekiti ama Katibu Mkuu, na walikua wakiangalia uwezekano wa kuitisha kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Dodoma kutoa matamko, na walipanga kufanya Press Conf leo kulaani hatua yoyote ya kuvunjwa kwa UVCCM ama hata kuondolewa madarakani kwa viongozi wake wa juu wakiongozwa na Benno Malisa. Bahati nzuri vijana safari hii wako safi saana, wanatanua katika viunga vya Dodoma. Baadhi wameamua kuonndoka hata kabla ya taarifa rasmi. Hofu ni kubwa mno kwa leo.
Mkuu ungeziweka tetesi kama zilivyo...Binafsi ni wazi umeongezea vikorombwezo ama hata kupotosha kuhusu "tetesi" hizo.

Kwa mfano "Kutaka kuvunjwa" bado pia inaweza kuwa tetesi.

Sijui kwanini tetesi ulizozisikia kuwa "inataka kuvunjwa" wewe umezibadili na kuwa "imefutwa"

Kama unatuwekea tetesi ambayo source yake nayo ni tetesi na inasema "wanataka kuvunja"

Wewe hiyo tetesi ya "kuifuta" source yake ni ipi?

Again,we mwandishi mkuu?
 
Nahisi kama kutatokea jambo kubwa sana nalo litabadili mwelekeo wa siasa ya nchi hii..sijui kama ni vision ama ni hisia lakini one of this is true!
 
chondechonde isije ikawa hizi ni mbinu za uvccm za kutuma ujumbe
kwa wazee wa ccm. wametoa wasiwasi wao facebook, ujumbe umejikita jf,
na hatimaye great thinkers wa jf wanatuma ujumbe ccm kwamba "mkivunja uvccm mmekwisha".
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]CCM kwachafuka [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 21 November 2011 18:54 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0diggsdigg

UVCCM WAPANGA KUASI, NI HOFU YA KUFUTWA KWA UMOJA WAO
Neville Meena, Dodoma
HALI imezidi kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.Hatua ya viongozi wa UVCCM kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini Dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni “kupigania umoja wao na chama chao,” imezidi kuchafua hali ya hewa.

Taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kamati Kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo Rais Kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na Kikwete.

Juzi usiku, wenyeviti wa UVCCM kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la Area D mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa UVCCM utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja Chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM na wale wa Baraza Kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe NEC ya CCM iwapo wataridhia kufanya hivyo.

Kauli za viongozi
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambaye hakupenda kuandikwa jina gazetini alisema hakuna mpango wa kufuta UVCCM na kuziita taarifa hizo kuwa ni za kupika.

Kauli yake iliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema: “Hakuna kitu kama hicho, mimi ni mshiriki wa vikao vyote vya Sekretarieti hakuna ajenda hiyo kwenye vikao vyetu hivi.”

“Ndiyo maana kwenye mkutano na waandishi wa habari nimesema kwamba watu waache kupandikiza vitu ambavyo kimsingi havipo, vikao hivi ni vya kawaida na ajenda zimewekwa wazi, sasa kama kuna watu wanaleta hizi hoja, basi wana malengo yao tu.”

Mapema Nape akizumgunza na waandishi wa habari alisema kumekuwapo na taarifa nyingi zinazowafanya Watanzania kutaharuki kana kwamba kuna vita inayotarajiwa kutokea mjini hapa.

“Naomba wanahabari wenzangu, nisaidieni maana haya yote yanatokana na taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari, lakini ajenda zetu kama nilivyosema jana (juzi) zinafahamika, kubwa ni kupitia utekelezaji wa mabadiliko ndani ya chama chetu,” alisema Nape.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema hana taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa mpango wa kufutwa kwa umoja huo ambao yeye ni mtendaji wake mkuu na kwamba hata katika kikao cha sekretarieti ambacho yeye ni mjumbe hakukuwa na ajenda ya aina hiyo.

Hata hivyo, Shigela hakuwa tayari kuweka bayana iwapo alifahamu mkusanyiko wa viongozi wa UVCCM kutoka mikoani waliopo Dodoma, zaidi ya kusisitiza kwamba kipindi hiki ni cha kutulia kwa wana CCM kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingine ambazo wakati mwingine vyanzo vyake si bayana.

Chimbuko la hisia
Chimbuko la hisia za kufutwa kwa UVCCM ni taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya vikao vya Kamati ya Maadili ambayo katika siku yake ya kwanza iliwahoji baadhi ya viongozi wake akiwamo Kaimu Mwenyekiti, Benno Malisa.

Wengi walihojiwa kuhusu utendaji wa kamati ya kutathmini upya uendeshaji wa UVCCM, ambayo tayari imefanya kazi yake katika mikoa 19 ya Tanzania Bara. Kamati hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Baraza Kuu ya UVCCM, Hussein Bashe, inatuhumiwa kuendesha mikutano iliyotumika kuwakashifu viongozi wa juu wa CCM wakiwamo Mwenyekiti Kikwete na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

“Kuna taarifa za uhakika kwamba ajenda hii haikupitia kwenye sekretarieti, inatoka kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma kwamba eti sehemu kubwa ya UVCCM tuko nyuma ya kundi moja ndani ya chama,” alisema mmoja wa wenyeviti wa umoja huo na kuongeza:

“Sasa mpango wao ni kufuta viongozi wote wa kuchaguliwa na baada ya hapo waandae uchaguzi mwingine ili kuwaweka viongozi wanaowataka, sasa hili sisi tunasema hapana kama ni tatizo litatuliwe lakini wasituulie umoja.”

Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu alisema jana kuwa taarifa kwamba UVCCM inafutwa zimezagaa katika ofisi hizo lakini bado zilikuwa hazijathibitishwa kutokana uamuzi wa vikao vya Kamati ya Maadili kufanywa kwa siri kubwa.

Mkakati wa Kupinga
Taarifa za mpango huo ndizo zilizowatia wazimu UVCCM kiasi cha kuitana Dodoma kwa lengo la kukabiliana na NEC ikiwa ‘itathubutu’ kuubariki.

Habari kutoka ndani ya kikao cha juzi usiku zinasema wenyeviti hao walikubaliana kwa kauli moja kuwaita wenyeviti wa wilaya wa umoja huo wa vijana ili kuongeza nguvu za kuwakabili wakuu wa CCM.

Mmoja wa wenyeviti kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki alisema juzi usiku kwamba: “Katika hili tumejipanga, tunao vijana zaidi ya 300 wapo kambini, tutawaleta hapa, tutaungana nao kupinga uamuzi huu.”

Harakati za UVCCM zinakwenda sambamba na kupinga utekelezaji wa mpango wa kujivua gamba ambao wanasema unatekelezwa kwa upendeleo ukiwalenga baadhi tu ya watu.

Mmoja wa viongozi hao alinukuliwa na chanzo chetu akisema wanaopaswa kufukuzwa au kuchukuliwa kwa hatua na CCM ni makada ambako Rais Kikwete alipata kura chache wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Kwa mantiki hiyo, vijana hao walisema mpango wa kujivua gamba hauna tija kwa sasa kwani unakigawa chama na kwamba CCM kina matatizo makubwa zaidi kinayopaswa kushughulikia badala na siyo kuchochea chuki miongoni mwa wanachama wake.

Maazimio ya NEC
NEC inakutana miezi minne tangu kilipokutana mara ya mwisho na kutoa maazimio ambayo yalisababisha mmoja wa makada wake, Rostam Aziz kujiuzulu ubunge katika Jimbo la Igunga pamoja na ujumbe wa NEC.

Rostam katika kujiuzulu huko aliitupia lawama sekretarieti ya chama hicho kwa kile alichokiita kuwa ni kuendesha siasa chafu dhidi yake na kuwataja kwa majina Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, John Chiligati na Nape kuwa wahusika.

Kujiuzulu kwa Rostam ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi katika mjadala wa CC na NEC.

Katika mazingira hayo, kuna kila uwezekano wa kutathmini jinsi falsafa ya kujivua gamba ilivyotekelezwa. Kuna madai kwamba Sekretarieti inayoongozwa na Mukama nayo imegawanyika katika suala la utekelezaji wa uamuzi wa NEC, hali inayoongeza sintofahamu ndani ya chama hicho.

SOURCE: Mwananchi

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kama hawa waliokutana Dodoma ni vijana na bado wanang'ang'ania kuendelea kuwa vijana ndani ya hiki chama cha mamluki (CCM) basi kuna kasoro katika fikira na dhamira zao kwa Taifa letu.

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]CCM kwachafuka
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 21 November 2011 18:54
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

CCM imefika kwenye turning point, haiwezi tena kuendelea kwenda juu ni kurudi chini kwanza ndo waanze kujenga upya.
 
... Too much stress of unresolved internal conflicts can totally compromise ones immunity ... SOURCE: Emotional Intelligence!

My concern!

From now onwards .. We will receive several news of Poor healthy for those who are really victims of this Situations.. It will be a surprise in that .. People have lent to fight in all ares of their life.. but not how to preserve their health ... AND.. The key factor for any NOBLE Leader to have his Health in Place ...Is... HONEST, TRUTHFULNESS AND CREDIBILITY!!

YES!!

Its not all about rushing to India etc ... When its too late!!.. Its about being .. Honest, Noble, Credible and Truthful in serving the community!

Nahisi kama kutatokea jambo kubwa sana nalo litabadili mwelekeo wa siasa ya nchi hii..sijui kama ni vision ama ni hisia lakini one of this is true!

Ame ... Naunga mkono ...Lakini labada jambo lenyewe liwe AFYA zao kuzorota ...baada ya misuguano na minyukano ..Lingine ? Mhh!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hawa vijana wa UVCCM wanachekesha sana. Kwahiyo assumptions zao ni kuwa
1. Yeyote anayetoka CCM akaenda CHADEMA basi atapokelewa kwa Red Carpet(natumai bado CDM wakumbuka ya Shibuda)

2. Kwamba wapo tayari kupigania ulaji wao ikiwemo kuwafungia ndani wajumbe wa NEC ili kitumbua chao kisiingie mchanga(kumbuka hakuna hata moja wanalopigania ni kwa maslahi ya mwananchi wa kawaida!).

3. Kwamba BAVICHA yenyewe imekaa tu bila uongozi makini, ikisubiria mataputapu ya UVCCM yaje kusimikwa uongozi BAVICHA kwa mbwembwe(hakika akutukanaye hakuchagulii tusi).

4. Kwamba iwapo NEC ikirudi nyuma na kutoufuta umoja wao UVCCM, basi wako tayari kusupport maamuzi ya chama isipokua ule unaogusa mafisadi kuvuliwa gamba.(hapa ni pamoja na ile sheria mbovu ya mchakato wa katiba mpya).

Halafu UVCCM ni daraja la wazee wanapotaka uongozi, si sauti huru ya kutetea matatizo ya vijana nchini na hasa miaka hii, ndiyo imezidi kujidhihirisha hivyo. Eti Malisa ni sawa na Malema, vichekesho!... Malema ni very independent thinker ambaye anapingana na chama chake on matters of principle hata kama ni controversial. Sio huyu wa kukimbilia Monduli kuwekewa mdomoni nini cha kusema kila akiamka.

Vijana wa namna hii hawana faida si kwa CDM tu bali kwa chama chochote cha siasa(including CCM) ambacho afya yake inatokana na umoja wa vijana ulio imara na unaosimamia misingi ya uanzishwaji wa hicho chama. Vijana wanaofikiria kwa matumbo yao ni hatari kuliko UKIMWI kwa mustakabali wa taifa.
 
Kama hawa waliokutana Dodoma ni vijana na bado wanang'ang'ania kuendelea kuwa vijana ndani ya hiki chama cha mamluki (CCM) basi kuna kasoro katika fikira na dhamira zao kwa Taifa letu.

njaa mbaya sana ndugu yangu! Ukiangalia vjana wengi waliopo ccm,either ni mtoto wa kigogo au rafiki zake ambao wananufaika na uhalifu unaofanyika humu nchini au ni kijana mwenye mipango ya dili fulani la uhalifu anapanga kulifanya/analifanya. Hivi hivi huwezi ukamkuta huko! Ukombozi wa nchi hii ni mgumu lakini ushindi waja!
 
si kweli kwaba vijana wote walioko UVCCM hawafai wapo wengi tu wenye fikra nzuri za kuendeleza nchi hii na hawa naomba kama wataomba wahamie CHADEMA wapokelewe kama ilivyokuwa kwa Mpendazoe, Shibuda, Nyimbo etc
 
HALI imezidi kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.Hatua ya viongozi wa UVCCM kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini Dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni “kupigania umoja wao na chama chao,” imezidi kuchafua hali ya hewa.Taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.Kamati Kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo Rais Kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na Kikwete.Juzi usiku, wenyeviti wa UVCCM kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la Area D mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa UVCCM utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja Chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM na wale wa Baraza Kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe NEC ya CCM iwapo wataridhia kufanya hivyo.source gazeti la mwananchi.
 
"alisema,alisema,alisema mwalimu alisema vijana amkeni kumekucha sasa ni wakati wa mchakamchaka! Chinja!mchakamcha chinja!"
 
Nadhani utakuwa ni uamuzi wa busara iwapo wataamua kuasi chama pindi watakapolazimishwa kukubali kuburuzwa..
 
hali imezidi kuwa tete ndani ya chama cha mapinduzi (ccm), kundi kubwa la umoja wa vijana wa chama hicho (uvccm), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.hatua ya viongozi wa uvccm kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni "kupigania umoja wao na chama chao," imezidi kuchafua hali ya hewa.taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni kamati kuu (cc) na halmashauri kuu ya taifa (nec), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, rais jakaya kikwete.kamati kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo rais kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha kamati ya maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na kikwete.juzi usiku, wenyeviti wa uvccm kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la area d mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa uvccm utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ya uvccm na wale wa baraza kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe nec ya ccm iwapo wataridhia kufanya hivyo.source gazeti la mwananchi.

sasa wanasubiri nini wangehamia tu ili majamaa yajirekebishe,,,
 
Hivi haya mambo ni rahisi kiasi hcho?
Kuhamia CDM kama kuhamia Airtel??
 
CCM is intentionally attempting to drive people's attention away from discussing otherwise national's grave matters and make them focus on its internal turmoils.

Kweli sana, wanataka wananchi wasahau ripoti ya tume kuhusu kina Jairo, Dowans ishasahaulika kwa wengi, Muswada nao ndio usahaulike na mengine mengi. Hawa jamaa wanaishi kwa ujanja ujanja
 
Back
Top Bottom