Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Kimenuka Dodoma, magamba yapata moto

Hawa vijana wa UVCCM wanachekesha sana. Kwahiyo assumptions zao ni kuwa
1. Yeyote anayetoka CCM akaenda CHADEMA basi atapokelewa kwa Red Carpet(natumai bado CDM wakumbuka ya Shibuda)

2. Kwamba wapo tayari kupigania ulaji wao ikiwemo kuwafungia ndani wajumbe wa NEC ili kitumbua chao kisiingie mchanga(kumbuka hakuna hata moja wanalopigania ni kwa maslahi ya mwananchi wa kawaida!).

3. Kwamba BAVICHA yenyewe imekaa tu bila uongozi makini, ikisubiria mataputapu ya UVCCM yaje kusimikwa uongozi BAVICHA kwa mbwembwe(hakika akutukanaye hakuchagulii tusi).

4. Kwamba iwapo NEC ikirudi nyuma na kutoufuta umoja wao UVCCM, basi wako tayari kusupport maamuzi ya chama isipokua ule unaogusa mafisadi kuvuliwa gamba.(hapa ni pamoja na ile sheria mbovu ya mchakato wa katiba mpya).

Halafu UVCCM ni daraja la wazee wanapotaka uongozi, si sauti huru ya kutetea matatizo ya vijana nchini na hasa miaka hii, ndiyo imezidi kujidhihirisha hivyo. Eti Malisa ni sawa na Malema, vichekesho!... Malema ni very independent thinker ambaye anapingana na chama chake on matters of principle hata kama ni controversial. Sio huyu wa kukimbilia Monduli kuwekewa mdomoni nini cha kusema kila akiamka.

Vijana wa namna hii hawana faida si kwa CDM tu bali kwa chama chochote cha siasa(including CCM) ambacho afya yake inatokana na umoja wa vijana ulio imara na unaosimamia misingi ya uanzishwaji wa hicho chama. Vijana wanaofikiria kwa matumbo yao ni hatari kuliko UKIMWI kwa mustakabali wa taifa.
 
si kweli kwaba vijana wote walioko UVCCM hawafai wapo wengi tu wenye fikra nzuri za kuendeleza nchi hii na hawa naomba kama wataomba wahamie CHADEMA wapokelewe kama ilivyokuwa kwa Mpendazoe, Shibuda, Nyimbo etc

Kama wanaona Chadema inafaa kwa mapambano kwa nini wasitoe tamko la kuwaunga mkono kuhusu katiba mpaya wakiwa bado ndani ya Chama chao. Wanataka kutueleza kuwa yanayofanywa na chama chao ni mazuri ikiwa wao binafsi hawadhuriki na ni mabaya ikiwa yanawadhuru. Utawasikia wakibakizwa wanaandamana kuunga mkono upitishwaji wa mswada wa sheria ya katiba mpya uliopitishwa na bunge. Wakifukuzwa wanaenda kuungana na Chadema pamoja na wadau wengine katika harakati za ukombozi wa nchi yetu ikiwemo katiba; huu ni unafiki mkubwa na wantumikia mungu TUMBO tu na wala sio uzalendo. Wenye hekima na kuona haja ya kupambana tayari wakpo kazini na wanapambana katika kutafuta haki ya watanzania wote na wala sio kikundi cha watu wachache kwa ajili ya masilahi binafsi.
 
Hawa vijana wa UVCCM wanachekesha sana. Kwahiyo assumptions zao ni kuwa
1. Yeyote anayetoka CCM akaenda CHADEMA basi atapokelewa kwa Red Carpet(natumai bado CDM wakumbuka ya Shibuda)

2. Kwamba wapo tayari kupigania ulaji wao ikiwemo kuwafungia ndani wajumbe wa NEC ili kitumbua chao kisiingie mchanga(kumbuka hakuna hata moja wanalopigania ni kwa maslahi ya mwananchi wa kawaida!).

3. Kwamba BAVICHA yenyewe imekaa tu bila uongozi makini, ikisubiria mataputapu ya UVCCM yaje kusimikwa uongozi BAVICHA kwa mbwembwe(hakika akutukanaye hakuchagulii tusi).

4. Kwamba iwapo NEC ikirudi nyuma na kutoufuta umoja wao UVCCM, basi wako tayari kusupport maamuzi ya chama isipokua ule unaogusa mafisadi kuvuliwa gamba.(hapa ni pamoja na ile sheria mbovu ya mchakato wa katiba mpya).

Halafu UVCCM ni daraja la wazee wanapotaka uongozi, si sauti huru ya kutetea matatizo ya vijana nchini na hasa miaka hii, ndiyo imezidi kujidhihirisha hivyo. Eti Malisa ni sawa na Malema, vichekesho!... Malema ni very independent thinker ambaye anapingana na chama chake on matters of principle hata kama ni controversial. Sio huyu wa kukimbilia Monduli kuwekewa mdomoni nini cha kusema kila akiamka.

Vijana wa namna hii hawana faida si kwa CDM tu bali kwa chama chochote cha siasa(including CCM) ambacho afya yake inatokana na umoja wa vijana ulio imara na unaosimamia misingi ya uanzishwaji wa hicho chama. Vijana wanaofikiria kwa matumbo yao ni hatari kuliko UKIMWI kwa mustakabali wa taifa.

Well said! Natoa ushauri - Ikiwa watahamia CDM - wanahitaji probation ya mwaka mmoja hivi ili yasije kuwa kama ya Makamba na 'Tambo Hizi' kwenye chama cha magamba.
 
Nimekuta mmoja wa wafuasi Lowassa, ambaye toka jana amekua akilalamika kupambana, Ally Bananga, amebandika maneno haya katika kundi la Tanuri la Fikra ndani ya Facebok;

"Ally Bananga Mwatiga5:29pm Nov 21
eti wanataka kuivunja UVCCM, tumewakosea nn?"

Taarifa zinasema huenda Jumuiya hiyo na nyingine zikavunjwa kwa muda. Hiyo ni wakati sasa hali ikiendelea kufukuta mjini Dodoma ambako mabilioni ya fedha yamemwagwa kwa wajumbe wa NEC kuhakikisha kila azimio linapigiwa kura ili azimio la kuvua gamba lipingwe.

Tayari waraka wa mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu uliokua na mambo mengi mazuri ulishaingia dosari kwa kuchomeka hoja ya kuwasamehe mafisadi kwa lengo la "kunusuru chama"... Mwenyekiti akapinga kwa kusema, "chama kitanusurikaje kwa kulinda uvundo?" Sasa kazi ipo. Magamba yanazidi kuwaka moto, hadi yatapasuka.

Mafisadi na wafuasi wao nguo za ndani zinawabana.
 
CCM is intentionally attempting to drive people's attention away from discussing otherwise national's grave matters and make them focus on its internal turmoils.

Mwita25, hi man! Has someone stolen your password. I am impressed with your recent comments. I feel like adding you as a first friend in this mtandao. Tell FF and Rejao that I am waiting for their conversion as well.
 
They should go sooner rather later. Hawa walishapoteza uhalali wa kushikilia nafasi za kitaifa, yet ni wapapmbe wa watu ambao integrity yao imashachafuka. Kama wanataka kuwa foot soldiers wa mtu basi wamfuate hukoa atakakokuwa.
 
Kuvunja UVCCM ni kama ngumu kutokea lakini ngoja tuone maana na wale hawachelewi kuwa wanasoma upepo huku JF, ila wakivunja UVCCM, pia wavunje na Kamati kuu ya CCM
 
CCM is intentionally attempting to drive people's attention away from discussing otherwise national's grave matters and make them focus on its internal turmoils.

That is CCM my friend.
 
njaa mbaya sana ndugu yangu! Ukiangalia vjana wengi waliopo ccm,either ni mtoto wa kigogo au rafiki zake ambao wananufaika na uhalifu unaofanyika humu nchini au ni kijana mwenye mipango ya dili fulani la uhalifu anapanga kulifanya/analifanya. Hivi hivi huwezi ukamkuta huko! Ukombozi wa nchi hii ni mgumu lakini ushindi waja!

The quarrel of devils is the Priests jubilee!
 
For sure mwita,i agree with u!
CCM is intentionally attempting to drive people's attention away from discussing otherwise national's grave matters and make them focus on its internal turmoils.
 
kama walishindwa kujivua gamba ndo wataweza kuifuta taasisi rasmi ya chama? Uvccm wala wasihofu chochote. Mwenyekiti wao wa chama ndo kimeo
 
They should go sooner rather later. Hawa walishapoteza uhalali wa kushikilia nafasi za kitaifa, yet ni wapapmbe wa watu ambao integrity yao imashachafuka. Kama wanataka kuwa foot soldiers wa mtu basi wamfuate hukoa atakakokuwa.

Mkuu nasikia stori ya gamba ndiyo imeenda hivyo sasa EL na mkuu wako si patachimbika hahahaha!!!!!!!!
 
Hawa vijana wa UVCCM wanachekesha sana. Kwahiyo assumptions zao ni kuwa
1. Yeyote anayetoka CCM akaenda CHADEMA basi atapokelewa kwa Red Carpet(natumai bado CDM wakumbuka ya Shibuda)

2. Kwamba wapo tayari kupigania ulaji wao ikiwemo kuwafungia ndani wajumbe wa NEC ili kitumbua chao kisiingie mchanga(kumbuka hakuna hata moja wanalopigania ni kwa maslahi ya mwananchi wa kawaida!).

3. Kwamba BAVICHA yenyewe imekaa tu bila uongozi makini, ikisubiria mataputapu ya UVCCM yaje kusimikwa uongozi BAVICHA kwa mbwembwe(hakika akutukanaye hakuchagulii tusi).

4. Kwamba iwapo NEC ikirudi nyuma na kutoufuta umoja wao UVCCM, basi wako tayari kusupport maamuzi ya chama isipokua ule unaogusa mafisadi kuvuliwa gamba.(hapa ni pamoja na ile sheria mbovu ya mchakato wa katiba mpya).

Halafu UVCCM ni daraja la wazee wanapotaka uongozi, si sauti huru ya kutetea matatizo ya vijana nchini na hasa miaka hii, ndiyo imezidi kujidhihirisha hivyo. Eti Malisa ni sawa na Malema, vichekesho!... Malema ni very independent thinker ambaye anapingana na chama chake on matters of principle hata kama ni controversial. Sio huyu wa kukimbilia Monduli kuwekewa mdomoni nini cha kusema kila akiamka.

Vijana wa namna hii hawana faida si kwa CDM tu bali kwa chama chochote cha siasa(including CCM) ambacho afya yake inatokana na umoja wa vijana ulio imara na unaosimamia misingi ya uanzishwaji wa hicho chama. Vijana wanaofikiria kwa matumbo yao ni hatari kuliko UKIMWI kwa mustakabali wa taifa.
....Ndio matatizo ya vijana kugeuza chama kuwa kampuni yao ya kuwaajiri kwa hiyo wanahofia matumbo yao tu hakuna jipya!!
 
Hiyo avatar yako PATHFINDER ni kama umekula makaange ya kutosha sasa yameshambulia mfumo wa fahamu na ukajikuta umechapa mbonji hahahaaaaaaaaaaaaaa!!!
 
UVCCM WAPANGA KUASI, NI HOFU YA KUFUTWA KWA UMOJA WAO
Neville Meena, Dodoma
HALI imezidi kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.Hatua ya viongozi wa UVCCM kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini Dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni “kupigania umoja wao na chama chao,” imezidi kuchafua hali ya hewa.

Taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kamati Kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo Rais Kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na Kikwete.

Juzi usiku, wenyeviti wa UVCCM kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la Area D mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa UVCCM utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja Chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM na wale wa Baraza Kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe NEC ya CCM iwapo wataridhia kufanya hivyo.

Kauli za viongozi
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambaye hakupenda kuandikwa jina gazetini alisema hakuna mpango wa kufuta UVCCM na kuziita taarifa hizo kuwa ni za kupika.

Kauli yake iliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema: “Hakuna kitu kama hicho, mimi ni mshiriki wa vikao vyote vya Sekretarieti hakuna ajenda hiyo kwenye vikao vyetu hivi.”

“Ndiyo maana kwenye mkutano na waandishi wa habari nimesema kwamba watu waache kupandikiza vitu ambavyo kimsingi havipo, vikao hivi ni vya kawaida na ajenda zimewekwa wazi, sasa kama kuna watu wanaleta hizi hoja, basi wana malengo yao tu.”

Mapema Nape akizumgunza na waandishi wa habari alisema kumekuwapo na taarifa nyingi zinazowafanya Watanzania kutaharuki kana kwamba kuna vita inayotarajiwa kutokea mjini hapa.

“Naomba wanahabari wenzangu, nisaidieni maana haya yote yanatokana na taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari, lakini ajenda zetu kama nilivyosema jana (juzi) zinafahamika, kubwa ni kupitia utekelezaji wa mabadiliko ndani ya chama chetu,” alisema Nape.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema hana taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa mpango wa kufutwa kwa umoja huo ambao yeye ni mtendaji wake mkuu na kwamba hata katika kikao cha sekretarieti ambacho yeye ni mjumbe hakukuwa na ajenda ya aina hiyo.

Hata hivyo, Shigela hakuwa tayari kuweka bayana iwapo alifahamu mkusanyiko wa viongozi wa UVCCM kutoka mikoani waliopo Dodoma, zaidi ya kusisitiza kwamba kipindi hiki ni cha kutulia kwa wana CCM kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingine ambazo wakati mwingine vyanzo vyake si bayana.

Chimbuko la hisia
Chimbuko la hisia za kufutwa kwa UVCCM ni taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya vikao vya Kamati ya Maadili ambayo katika siku yake ya kwanza iliwahoji baadhi ya viongozi wake akiwamo Kaimu Mwenyekiti, Benno Malisa.

Wengi walihojiwa kuhusu utendaji wa kamati ya kutathmini upya uendeshaji wa UVCCM, ambayo tayari imefanya kazi yake katika mikoa 19 ya Tanzania Bara. Kamati hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Baraza Kuu ya UVCCM, Hussein Bashe, inatuhumiwa kuendesha mikutano iliyotumika kuwakashifu viongozi wa juu wa CCM wakiwamo Mwenyekiti Kikwete na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

“Kuna taarifa za uhakika kwamba ajenda hii haikupitia kwenye sekretarieti, inatoka kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma kwamba eti sehemu kubwa ya UVCCM tuko nyuma ya kundi moja ndani ya chama,” alisema mmoja wa wenyeviti wa umoja huo na kuongeza:

“Sasa mpango wao ni kufuta viongozi wote wa kuchaguliwa na baada ya hapo waandae uchaguzi mwingine ili kuwaweka viongozi wanaowataka, sasa hili sisi tunasema hapana kama ni tatizo litatuliwe lakini wasituulie umoja.”

Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu alisema jana kuwa taarifa kwamba UVCCM inafutwa zimezagaa katika ofisi hizo lakini bado zilikuwa hazijathibitishwa kutokana uamuzi wa vikao vya Kamati ya Maadili kufanywa kwa siri kubwa.

Mkakati wa Kupinga
Taarifa za mpango huo ndizo zilizowatia wazimu UVCCM kiasi cha kuitana Dodoma kwa lengo la kukabiliana na NEC ikiwa ‘itathubutu’ kuubariki.

Habari kutoka ndani ya kikao cha juzi usiku zinasema wenyeviti hao walikubaliana kwa kauli moja kuwaita wenyeviti wa wilaya wa umoja huo wa vijana ili kuongeza nguvu za kuwakabili wakuu wa CCM.

Mmoja wa wenyeviti kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki alisema juzi usiku kwamba: “Katika hili tumejipanga, tunao vijana zaidi ya 300 wapo kambini, tutawaleta hapa, tutaungana nao kupinga uamuzi huu.”

Harakati za UVCCM zinakwenda sambamba na kupinga utekelezaji wa mpango wa kujivua gamba ambao wanasema unatekelezwa kwa upendeleo ukiwalenga baadhi tu ya watu.

Mmoja wa viongozi hao alinukuliwa na chanzo chetu akisema wanaopaswa kufukuzwa au kuchukuliwa kwa hatua na CCM ni makada ambako Rais Kikwete alipata kura chache wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Kwa mantiki hiyo, vijana hao walisema mpango wa kujivua gamba hauna tija kwa sasa kwani unakigawa chama na kwamba CCM kina matatizo makubwa zaidi kinayopaswa kushughulikia badala na siyo kuchochea chuki miongoni mwa wanachama wake.

Maazimio ya NEC
NEC inakutana miezi minne tangu kilipokutana mara ya mwisho na kutoa maazimio ambayo yalisababisha mmoja wa makada wake, Rostam Aziz kujiuzulu ubunge katika Jimbo la Igunga pamoja na ujumbe wa NEC.

Rostam katika kujiuzulu huko aliitupia lawama sekretarieti ya chama hicho kwa kile alichokiita kuwa ni kuendesha siasa chafu dhidi yake na kuwataja kwa majina Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, John Chiligati na Nape kuwa wahusika.

Kujiuzulu kwa Rostam ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi katika mjadala wa CC na NEC.

Katika mazingira hayo, kuna kila uwezekano wa kutathmini jinsi falsafa ya kujivua gamba ilivyotekelezwa. Kuna madai kwamba Sekretarieti inayoongozwa na Mukama nayo imegawanyika katika suala la utekelezaji wa uamuzi wa NEC, hali inayoongeza sintofahamu ndani ya chama hicho.

Source: Mwananchi la leo
 
Back
Top Bottom