Kilio cha Maalim Seif chafikishwa UN

Kilio cha Maalim Seif chafikishwa UN

Hakuna mjomba nje ya nchi Tanzania atakaye tuondolea umaskini zaidi ya kutupa mikopo na misaada yenye masharti magumu. Ila kuna "viongozi wa siasa" nchini walio na fikra mgando wakidhani uongozi unaweza kuamuliwa kwenye meza za hao "wajomba".

Maalim Seif amini hiyo ni ndoto ya mchana kweupe anayoiota.
 
Sio tuu haina impact bali pia ni empty words. Nilipitia kidogo some international law instruments, zinahitaji kwanza ku exhaust local remedies. CUF did nothing at home about hizo claimed gross human rights violation. Tuna Tume ya Haki za binaadamu CUF walipaswa kuanzia huku. Kwenda kumshitaki nchi kwenye NGO ni just attention seeking, but is is just wastage of time and resources!.

Pasco

Lakini NGO hiyo UN wamepokea ripoti yao
 
Sasa hiyo IL inatoa pendekezo kwa UN baada ya kumsikiliza Maalim bila kupata maelezo ya pande nyingine hii sio sahihi ili utoe maamuz ya haki ni lazima usikilize pande zote.
 
Yule mzee anazeeka vibaya,atazunguka dunia mpaka iishe,zanzibar maisha yanaendelea na yataendelea na bara maisha yataendelea,mlio na imani na mnaiombea nchi sijui iwekewe vikwazo na sijui mkiwa na faida gani,mnaota mchana kweupe
 
Patamu hapo!
Patamu kuwekewa vikwazo?
Hakuna jipya hapo,sefu alishafanya fitna Zanzibar ikakosa misaada lakini hakuupata urais
Sefu alishajaribu kufanya fitna JMT iwekewe vikwazo lakini hoja zake zikakosa mashiko
Kosa kubwa alilofanya Sefu ni kususa,hakuna Urais wa mezani
 
You are misled Pasco.....impact ipo. Mind you these countries.....speak the same language....which means given the chance and a conducive environment....mtapewa za uso TU.....rejected in several international aspects. Kumbuka , intention ya Maalium na CUF sio military intervention but to expose the weakness part.

By the way, how can you build an economy i.e. viwanda as we claimed it, when you are faced with such international allegations? Hizi nchi kwanza hazichelewi kuwapa yale majina yaleee...yale...."terrorist countries". Ukishapewa hilo jina umekwisha. Kuna yale ya least developed tayari yanatuathiri....sasa ukipewa hilo la terrorist tena. Hawa wanakubatiza tu jina baya...haupenyi kokote.

Tutaishia kuwa watazamji tu.
Acha upenzi wewe. Shughulikieni mgogoro wenu na Lipumba. Hayo ya ICC mnapoteza muda bure! Andaeni Mgombea kwa ajili ya 2020. Huyo Bwana afanye biashara nyingine ya kufanya
 
You are misled Pasco.....impact ipo. Mind you these countries.....speak the same language....which means given the chance and a conducive environment....mtapewa za uso TU.....rejected in several international aspects. Kumbuka , intention ya Maalium na CUF sio military intervention but to expose the weakness part.

By the way, how can you build an economy i.e. viwanda as we claimed it, when you are faced with such international allegations? Hizi nchi kwanza hazichelewi kuwapa yale majina yaleee...yale...."terrorist countries". Ukishapewa hilo jina umekwisha. Kuna yale ya least developed tayari yanatuathiri....sasa ukipewa hilo la terrorist tena. Hawa wanakubatiza tu jina baya...haupenyi kokote.

Tutaishia kuwa watazamji tu.

Hivyo vikwazo huwa vinawekwa kama mmegusa interest za hao wazungu mfano Zimbabwe,Iraq.Issue ya Zanzibar haina impact kwa mataifa ya nje ndio maana wako kimya
 
Hao ndo walizivuruga libya, Iraq, Congo, Syria na nk. Ndo mna waomba watuvuruge?
Ndiyo hao hao. Bora waje watuvuruge na sisi tuanze moja na wote tuishi kama mashetani. Si ndivyo bwana mkubwa anavyotaka...!?
 
Kwani hamna MTU mwingine wa kugombea mpaka anatanga na njia miaka yote bila mafanikio?
 
Mashine ya propaganda Lumumba ipo kazini kusambaza uvundo wakati ukweli unajisimamia
 
ZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda, anaandika Jabir Idrissa.

Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”

Katika tamko walilolitoa na kufikishwa mbele ya Mkutano wa 33 wa Baraza hilo uliofanyika Septemba mosi mwaka huu, Liberal International imetaka jumuiya ya kimataifa, kufikiria kuweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za watu wote walioshiriki kuidhinisha vitendo vya utesaji wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao.

Taasisi hiyo ambayo CUF ni mwanachama wa muda mrefu, imetoa wito kwa wabunge wanaofuata mtizamo wa kiliberali walioko upande wa serikali na upinzani katika mataifa yote duniani kuchukua msimamo imara kupitia mabunge ya nchi zao na kutoa matamko ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”

“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI.

Hatua hiyo ya LI kuandikia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa inakuja wiki kadhaa baada ya Maalim Seif kukutana na taasisi mbalimbali za kimataifa zinazoshughulikia maendeleo ya demokrasia na utawala bora, pamoja na wakuu wa serikali za Marekani, Ulaya na Canada.

Maalim Seif aliyefuatana na baadhi ya wasaidizi wake pia alifika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague, Uholanzi ambako aliwasilisha malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa Zanzibar kwa idhini ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hatua ya Maalim Seif na CUF imekuja baada ya CCM kumuamuru Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, 28 Oktoba, baada ya kubaini kuwa chama hicho kimepoteza madaraka kupitia sanduku la kura.

Chanzo: Mwanahalisi Online
Good. Tena naomba Donald Trump apate urais aje atunyooshe
 
You are misled Pasco.....impact ipo. Mind you these countries.....speak the same language....which means given the chance and a conducive environment....mtapewa za uso TU.....rejected in several international aspects. Kumbuka , intention ya Maalium na CUF sio military intervention but to expose the weakness part.

By the way, how can you build an economy i.e. viwanda as we claimed it, when you are faced with such international allegations? Hizi nchi kwanza hazichelewi kuwapa yale majina yaleee...yale...."terrorist countries". Ukishapewa hilo jina umekwisha. Kuna yale ya least developed tayari yanatuathiri....sasa ukipewa hilo la terrorist tena. Hawa wanakubatiza tu jina baya...haupenyi kokote.

Tutaishia kuwa watazamji tu.
Mkuu Nara, bahati nzuri nimehudhuria UN GA na baadhi ya international conferences ambapo NGO zina organize demonstration tena kubwa tuu kupinga hili au lile, lakini mwisho wa siku kinachopatikana ni attention tuu! , NGOso zinabaki kuwa ni NGOs. The correct forum CUF wange exhaust the local remedies, wakishindwa then wanakwenda kwenye international level, lakini they did nothing! .

Hata huo uchaguzi hawakufanya lolote kupinga uhuni wa Jecha, hawakufanya chochote kuuzuia uchaguzi batili usifanyike wakasusia kushiriki. Amini nakuambia hakuna taasisi yoyote rasmi inaweza kuitertain ujinga kama huo, take it from me, ni mpaka 2020 and for some it might be a bit too little too late.
Pasco
 
Haina haja ya kuweka propaganda nyingi wakati wazanzibar wameshaipata serikali yao inayowahudumia wananchi bila ubaguzi wowote cha msingi maalim akae kimya na kusubiri 2020 huo ndo uanaume siyo kwenda kujikomba komba kwa watu ambao walitutawala na kuchukua Mali zetu!
Ya ccm sio Wazanzibari
 
Sasa hiyo IL inatoa pendekezo kwa UN baada ya kumsikiliza Maalim bila kupata maelezo ya pande nyingine hii sio sahihi ili utoe maamuz ya haki ni lazima usikilize pande zote.
Hea a unasubiri maelezo yepi wakati walikuwepo international observer ,kutoka ulaya na America na waliridhika na uchaguzi wa 25 October.

Suala la maalim kupeleka malalamiko huko Un sio la chama bali ni international community, hili suala sio la kupuuza, cuf wana ushahidi wa maandishi kuwa wameshinda uchaguzi na tume ya uchaguzi ilisaini màndishi hayo, sio wajinga
 
Back to the medieval times story of a hyena waiting anxiously for a human being's seemingly loosely-attached forelimbs to get unhitched and fall off! 20% of the 2015-2020 term is literally gone!!!
 
(1)UNHRC waliifanya nini MAREKANI kwa kitendo cha kuivamia IRAQ mwaka 2003 bila sababu za msingi tena kwa kupuuza katazo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
(2)Kuna mzungu gani aliwahi kushtakiwa katika mahakama ya ICC?
Watanzania /waafrika tukumbuke kuwa watu hawa si Baba zetu wala mama zetu. Tuache ujinga.
 
Kwani hamna MTU mwingine wa kugombea mpaka anatanga na njia miaka yote bila mafanikio?
Kwani ipo sheria inamzuia kugombea mara nyingi? Unajua Abdulwaye Wade aligombea mara ngapia hadi akafanikiwa kuwa rais?
 
Watanzania wakiona kizungu wanatamani wawe wazungu. Hivi wanayofanya Libya, Syria, Iraq na kwingine hawajui?

Huyu anayejidanganya aendelee.

nakumbuka ile ya UKAWA Kwenda nao Uholanzi eti wazungu wasaidie kutengua uchaguzi.

Seif angeenda Uganda ndo ajuwe maana ya upinzani. Hapa watu kuhojiwa tu wanalalama.
Hayana tofauti na haya yanayofanywa na wakoloni weusi tunaowapa dhamana katika nchi zetu
 
ZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda, anaandika Jabir Idrissa.

Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”

Katika tamko walilolitoa na kufikishwa mbele ya Mkutano wa 33 wa Baraza hilo uliofanyika Septemba mosi mwaka huu, Liberal International imetaka jumuiya ya kimataifa, kufikiria kuweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za watu wote walioshiriki kuidhinisha vitendo vya utesaji wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao.

Taasisi hiyo ambayo CUF ni mwanachama wa muda mrefu, imetoa wito kwa wabunge wanaofuata mtizamo wa kiliberali walioko upande wa serikali na upinzani katika mataifa yote duniani kuchukua msimamo imara kupitia mabunge ya nchi zao na kutoa matamko ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”

“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI.

Hatua hiyo ya LI kuandikia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa inakuja wiki kadhaa baada ya Maalim Seif kukutana na taasisi mbalimbali za kimataifa zinazoshughulikia maendeleo ya demokrasia na utawala bora, pamoja na wakuu wa serikali za Marekani, Ulaya na Canada.

Maalim Seif aliyefuatana na baadhi ya wasaidizi wake pia alifika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague, Uholanzi ambako aliwasilisha malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa Zanzibar kwa idhini ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hatua ya Maalim Seif na CUF imekuja baada ya CCM kumuamuru Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, 28 Oktoba, baada ya kubaini kuwa chama hicho kimepoteza madaraka kupitia sanduku la kura.

Chanzo: Mwanahalisi Online

Si tuliambiwa Maalim Seif alijifungia pale Dar Es Salaam hakwenda popote???
 
Back
Top Bottom