Kilio cha Maalim Seif chafikishwa UN

Kilio cha Maalim Seif chafikishwa UN

Kwanza Kikwete muondoe, kwa sababu yeye ameisha maliza muda wake.

Shein na Magufuli wasipokuwa makini issue gani itawatafuna?!. Zanzibar hakuna issue yoyote! . Hakuna ukiukwaji wowote wa haki za msingi za binaadamu!.

Uchaguzi ulipofutwa kihuni na kiubatili na Jecha, hakuna mtu yoyote aliyeupinga rasmi uhuni na ubatili huo!. Ubatili usipopingwa rasmi, hugeuka ni halali!.

Uchaguzi wa marudio ulipoitishwa tena, hakuna yeyote aliyepinga rasmi!. Japo ule ulikuwa ni ubakwaji wa demokrasia, lakini mtu akibakwa na kutulia tuu kumuacha mbakaji amfanye anavyotaka, na baada ya kubakwa ukatulia tuli!, utahesabika uliridhia ubakaji ule!.

Uchaguzi wa marudio umefuata kanuni zote za uchaguzi huru na wa haki, hivyo Shein ni rais halali wa Zanzibar hadi mwaka 2020 na hakuna yoyote wa kufanya lolote na rais Magufuli hapaswi kufanya jambo lolote, kwa sababu uchaguzi ni mambo ya ndani na Zanzibar ina autonomy yake!.

Lakini kwenye tuhuma za ukiukwaji wa haki za binaadamu kimataifa, hakuna kitu kinachoitwa Zanzibar kinachotambulika kimataifa, kinachotambulika kimataifa ni Tanzania!. Maalim Seif akizidisha choko choko za kutaka kuchafua recodi ya Tanzania katika haki za binaadamu kimataifa, anakuwa ni anamchokoa Magufuli! . Kuna msemo maarufu kule Zanzibar kuhusu choko choko, wanasema "choko choko mchokoe pweza binadamu hutamuweza!", hivyo ndivyo ilivyo kwa Magufuli, Seif hatamuweza!. Hizo kelele za Maalim Seif zinaweza kutafsiriwa kuwa ni fyokofyoko hivyo sana atakachoambulia Maalim Seif ni Magufuli anaweza kumhifadhi katika mahala salama!, kule wanaita pahala salama!

Au Magufuli akijiridhisha hizo kelele za Maalim Seif hazina athari zozote kiusalama, anaweza kumpuuzia tuu ila kwanza atamtafuta na kumpa mkono aone Maalim Seif atafanya nini, baada ya hapo mtashuhudia heshima na adabu! .
Pasco

Huu ushauri wako haumsaidii Rais Magufuli, Dr Shein wala Tanzania. Unashindwa kuoanisha mambo katika uhalisia wake.

Suala la Zanzibar na chaguzi halijaanza leo wala jana. Unaposhindwa wewe unatamani wapinzani wa kule wangemwaga damu kwanza baada ya Jecha kufuta uchaguzi halali eti ndio wasikilizwe hivyo ndivyo unavyoamini.

Nikukumbushe mpaka inaundwa GNU hao wazungu walishachoka na suala la Zanzibar na kama kuna mitego mara hii CCM wamenasa. Ile attention yote iliyojengwa na Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar kuelekea uchaguzi wa Oktoba, 2015 unafikiri ulikuwa ya bure? Wale wataalamu wa uangalizi wa Uchaguzi walioletwa na jumuiya za kimataifa unafikiri ilikuwa bure?

Unafikiri jumuiya ya kimataifa haijuwi tatizo la Zanzibar wewe unataka kwanza watu wapinge kwa kumwaga damu? ndio uamini kuwa alichofanya Jecha si halali? Kwa sababu CUf wamemaliza jitihada zote kuanzia 1995,2000,2005 na 2010 hawakuchoka na walifuata njia zote za kidemokrasia. Umesahau kuwa mwaka 2001 kulifanywa mauaji kwa kudai ushindi na kuilalamikia ZEC?
 
Mkuu Chuma cha Mjeru, sio kupinga huo ndio ukweli wenyewe! . Zanzibar hakuna kitu, hakuna issue mpaka 2020! .
Pasco

Endelea kuamini hivyo kwa sababu huna namna nyengine ya kufikiri. Huoni diplomasia yetu inavyoharibika na kuingia katika rekodi mbaya kila kukicha. Suala hili sasa liko UN halijawahi kufika kwa staili hii. Viongozi wetu hawana hamu. Masindikizo na kukosa milahaka na wenye dunia yao inazidi na huoneshi walau njia ya ushauri na suluhu.

Yaani wewe unafurahia kile kinachoendelea unawatazama CUF kwa jicho la Kukosa na kutaka wasifanikiwe huku ukishindwa kuitazama Tanzania na athari inazozipata kwa suala hili la Zanzibar.

By the way mimi naamini kuna jambo kubwa linakuja kabla ya hio 2020 unayoitamani. Zanzibar kuna mgogoro na lazima usuluhishwe.
 
Nimewahi kusema humu kwamba UKAWA wapeleke hoja Bungeni, ili Tanzania ipitishe sheria ya kutambua haki za wananchi chini ya International Covenant on Civil and Political Rights - ICCPR . Lakini nina wasiwasi na akina Mbowe, T. Lissu na Mnyika na wengine kama wana sababu zao ambazo hazijulikani, hadi kunyamazia hii kitu myaka yote kama vile haipo au hawaijuwi! Wanapigwa wanawekwa ndani <baadhi yao, sio wote> nk. lakini huwasikii wakiitaja hii covenant! Ndio maana watu wanasema mambo ya kususia Bunge yanawanyima nafasi nzuri ya kudai haki za wananchi za msingi kama ilivyoainishwa ktk ICCPR.

Inashangaza sana kwamba masuala kama ya juzijuzi kuhusu "Fao la Kujitoa" Serikali inatumia vigezo vya kimataifa "Minimum Standards for Social Security - Convention 102" kuhalalisha msimamo wake ambao ukiacha vitu vichache vinavyolalamikiwa, ni mzuri sana. Lakini masuala ya demokrasia sivyo! Ni kama vile Tanzania iko katika sayari nyingine kabisaaaa!!
 
Togo siyo Tanzania wewe. Chunguza ni Vyama vingapi vya Ukombozi vimebaki Afrika kama siyo CCM, MPLA, FRELIMO, ANC. Kuna vingine?..... Sababu ni kwamba Vyama vya Upinzani katika Nchi hizo havijawa na Sera za kuwashawishi Wananchi wasikichague Chama kinachotawala. Mfano CUF, tunaletewa Mgombea anayeshindwa kila mara kwa vipindi vitano(5). Amekuwa Sultani kwani? Wengine hawapo wakajaribu nao?
Togo?? Hivi kumbe ni mweupe kichwani kiasi hiki.................hahahhhhhaaaa
 
Togo?? Hivi kumbe ni mweupe kichwani kiasi hiki.................hahahhhhhaaaa
Nilikupima kama unasoma posts vizuri. Wade ni wa Senegal. Kumbe unaelewa kidogo japo unabisha mambo ya maana kijana wangu!
 
Lakini si walisema hakwenda mahali alikuwa kajificha Tanzania Bara? Mbona mnatuchanganya wajemeni?
 
Si magu alisema atamsaidia,shein amwambie ukute magu ana suluhu,lakin hizi ni baadhi ya sabab zinazopelekea rais asisafir nin?
 
Daa habari mpyaa hii,in mwalusakos voice.
Hapo hakuna kitu kaka ni kujidanganya tu na hii habari imejaa uongo tu maana hakuna viongozi waliofungwa na kuteswa kama inavyofanya. Huyo Seif safari zake zenyewe analipiwa na serikali akamuulize Bisigye akitaka kujua haki za wapinzani
 
Huu nao ni upuuzi...haitakuja kutokea mambo kama hayo,afu hichi chama kinaamin katika wazungu cjui wenzetu bado hawajapata uhuru
 
Hamna kitu hapo jamaa anatamani ile nafasi yake arejeshewe apate kucheka cheka na vijana watanashati alafu anakazia na ule msemo wake sawa sawa aaah aah nasema sawa sawa..
 
Back
Top Bottom