Unatokwa povu, mkuuPasco,
Unaposema ukweli watu hawataki kusikia. Tusiwekeze akili zetu kwa wazungu wakati hata wao wanayo yao. Seif kama alishauriwa vibaya basi alikubali kosa. Kwa nini hakujifunza ile ya UKAWA ya Uholanzi? Hivi anaona mataifa ya nje yako kwa ajili ya maslahi ya vyama au watu?
Yeye anaenda na picha za matukio ambazo si uthibitisho wa chochote katika matukio yanayoshitua dunia. Aangalie kwanza Mashariki ya Kati ndo ajue majanga ya kibinadamu yako vipi. Kama kundi lao linataka sana haki lingejitokeza kwa yale yanayotokea huko.
Pia, aiende Uganda aulize upinzani uko vipi. Hata mahakama hajaonja anaona anaonewa.
Shida zetu kwa sasa Watanzania wengi ni JF na FB, vijana wanaona wachambuzi na kutoa matamko hata kujua duania inaendeshwa namna gani.
Hapa ndio huwa nazichukia siasa za Afrika.. Kwamba hatuwezi kufanya mambo yetu wenyewe kwa ustaarabu na kuheshimiana mpaka mzungu atushikie fimbo..
Yaani nakereka pale tunapoenda kusemea kwa wazungu eti ndo waje kutushinikiza kufanya jambo Fulani... Childish
Walisahau kama cuf ni wananchi tafauti na ccm, asilimia ya wapiga kura wa ccm Tanzania nzima ni 30 tu, kwa zanzibar 8 tu, ukifanyika uchaguzi wa uhuru .Poleni sana. Inaonekana hamujui kinachoendelea. Nashangaa kusema kuwa CUF hawaja fuatilia suala hilii wakati palikuwa na vikao tisa vya viongozi wa CCM pamoja na maalim seif. Ali hassana mwinyi alikuwepo kwenye vikao na ni shahidi wa hilo. CUF walikwenda kwa Kikwete, wakaenda kwa magufuli, zote hizo ni njia ya kutaka kumaliza mambo kwa usalama. Kwa kuwa nyinyi hamukuwepo zanzibar hamujui kilichokuwa kikiendelea. Magufuli alileta jeshi na CCM zanzibar walileta janjaweed. Wamepiga na kuwatia ndani watu na mwisho wakaendelea na kura ya maech 20, sasa nawauliza, juhudi gani munayotaka nyinyi ifanyike?.. CCM walifikiri wakimhonga Lipumba, CUF itasambaratika hawakujua kuwa CUF haitegemei mtu mmoja. Hiki ni chama cha wananchi. Kama hili la leo la UN ni dogo, subiri wiki usikie mshindo. Tayari viongozi wa CCM zanzibar wameanza kuitana wachawi.
wataitoa mwaka huu.
Mkuu umenunuliwa tunajua, kumbe ndo nyie ambao alosema ole sendeka kuwa kuna vijana wa ccm kwenye mitandao? So shame my friend, eti zanzibar hakukuwa na unyanyasaji na ununjaji wa haki za binadamu?Kwanza Kikwete muondoe, kwa sababu yeye ameisha maliza muda wake.
Shein na Magufuli wasipokuwa makini issue gani itawatafuna?!. Zanzibar hakuna issue yoyote! . Hakuna ukiukwaji wowote wa haki za msingi za binaadamu!.
Uchaguzi ulipofutwa kihuni na kiubatili na Jecha, hakuna mtu yoyote aliyeupinga rasmi uhuni na ubatili huo!. Ubatili usipopingwa rasmi, hugeuka ni halali!.
Uchaguzi wa marudio ulipoitishwa tena, hakuna yeyote aliyepinga rasmi!. Japo ule ulikuwa ni ubakwaji wa demokrasia, lakini mtu akibakwa na kutulia tuu kumuacha mbakaji amfanye anavyotaka, na baada ya kubakwa ukatulia tuli!, utahesabika uliridhia ubakaji ule!.
Uchaguzi wa marudio umefuata kanuni zote za uchaguzi huru na wa haki, hivyo Shein ni rais halali wa Zanzibar hadi mwaka 2020 na hakuna yoyote wa kufanya lolote na rais Magufuli hapaswi kufanya jambo lolote, kwa sababu uchaguzi ni mambo ya ndani na Zanzibar ina autonomy yake!.
Lakini kwenye tuhuma za ukiukwaji wa haki za binaadamu kimataifa, hakuna kitu kinachoitwa Zanzibar kinachotambulika kimataifa, kinachotambulika kimataifa ni Tanzania!. Maalim Seif akizidisha choko choko za kutaka kuchafua recodi ya Tanzania katika haki za binaadamu kimataifa, anakuwa ni anamchokoa Magufuli! . Kuna msemo maarufu kule Zanzibar kuhusu choko choko, wanasema "choko choko mchokoe pweza binadamu hutamuweza!", hivyo ndivyo ilivyo kwa Magufuli, Seif hatamuweza!. Hizo kelele za Maalim Seif zinaweza kutafsiriwa kuwa ni fyokofyoko hivyo sana atakachoambulia Maalim Seif ni Magufuli anaweza kumhifadhi katika mahala salama!, kule wanaita pahala salama!
Au Magufuli akijiridhisha hizo kelele za Maalim Seif hazina athari zozote kiusalama, anaweza kumpuuzia tuu ila kwanza atamtafuta na kumpa mkono aone Maalim Seif atafanya nini, baada ya hapo mtashuhudia heshima na adabu! .
Pasco
Wape Moyo mahafidhuna wenzako, Magu kaja zanzibar povu juu na unafiki kuwagawa Wazanzibari, eti kuwashukuru wa pemba kwa kuichagua ccm, kaangalie zile kura zake pemba alipata ngapi na Lowassa. Shame on you, nilikuwa nakuona mtu makini sana kumbe huna maana, unaongea utumbo siku hizi kwa elf 7500 unazo lip wa na ccmMkuu Chuma cha Mjeru, sio kupinga huo ndio ukweli wenyewe! . Zanzibar hakuna kitu, hakuna issue mpaka 2020! .
Pasco
Mkuu Ghibuu, kwanza mimi sio CCM na sijawahi kuwa!. Tofauti kati ya mimi na wewe ni mmoja kuandika kwa hisia za kilichotakiwa kufanyika na mimi kuandika ukweli halisi wa mambo!. Hivyo kosa langu ni kuusema ukweli jinsi ile ile ukweli huo ulivyo bila kujali ni mchungu kiasi gani au unauma kiasi gani, ukweli siku zote unabaki kuwa ndio ukweli na ndio unaosimama mpaka mwisho!. Sasa kwenye suala la uchaguzi wa Zanzibar, no one can do anything hadi 2020! .Mkuu umenunuliwa tunajua, kumbe ndo nyie ambao alosema ole sendeka kuwa kuna vijana wa ccm kwenye mitandao? So shame my friend, eti zanzibar hakukuwa na unyanyasaji na ununjaji wa haki za binadamu?
Hivi wakati na kabla ya uchaguzi ulikuwepo zanzibar? Shame on you shame on you
Nionavyo mimi nchi inayoongoza kwa kuwa na viongozi wenye mioyo migumu kama Tanzania .ZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda, anaandika Jabir Idrissa.
Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”
Katika tamko walilolitoa na kufikishwa mbele ya Mkutano wa 33 wa Baraza hilo uliofanyika Septemba mosi mwaka huu, Liberal International imetaka jumuiya ya kimataifa, kufikiria kuweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za watu wote walioshiriki kuidhinisha vitendo vya utesaji wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao.
Taasisi hiyo ambayo CUF ni mwanachama wa muda mrefu, imetoa wito kwa wabunge wanaofuata mtizamo wa kiliberali walioko upande wa serikali na upinzani katika mataifa yote duniani kuchukua msimamo imara kupitia mabunge ya nchi zao na kutoa matamko ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”
“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI.
Hatua hiyo ya LI kuandikia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa inakuja wiki kadhaa baada ya Maalim Seif kukutana na taasisi mbalimbali za kimataifa zinazoshughulikia maendeleo ya demokrasia na utawala bora, pamoja na wakuu wa serikali za Marekani, Ulaya na Canada.
Maalim Seif aliyefuatana na baadhi ya wasaidizi wake pia alifika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague, Uholanzi ambako aliwasilisha malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa Zanzibar kwa idhini ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua ya Maalim Seif na CUF imekuja baada ya CCM kumuamuru Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, 28 Oktoba, baada ya kubaini kuwa chama hicho kimepoteza madaraka kupitia sanduku la kura.
Chanzo: Mwanahalisi Online
Jecha atakufa kwa presha akiipata hii taarifa.
Mfano CUF, tunaletewa Mgombea anayeporwa ushindi kila mara kwa vipindi vitano(5).Amekuwa Sultani kwani? Wengine akina John Okello wazalendo hawapo wakajaribu nao?Mfano CUF, tunaletewa Mgombea anayeshindwa kila mara kwa vipindi vitano(5). Amekuwa Sultani kwani? Wengine hawapo wakajaribu nao?
Zanzibar inajuulikana sio tu UN lakini duniani kote kuliko Tanganyika au Tanzania. Safiri uujue ukweli huo unaouma. Hata hao Bongo fleva wanapokwenda hapo tu Afrika ya Kusini wanapopata taabu ya kujibu mswali. Wanaposema Dodoma wanaulizwa iko Zanzibar. Kila kizuri kuhusu Tanganyika jibu ni Zanzibar. Pasco maneno yako haya nimeyahifadhi na panipo uhai nitakukumbusha. Zanzibar katika dunia hii ni matusi kuifananisha na Tanganyika kwa kila kitu labda kwa kuchunana ngozi na kuuwa vikongwe na albino.Zanzibar anajulikana?
Chuki zako dhidi ya wazanazibari ni sawa mwanamke aleinyimwa unyumba. Hivi wewe unataka tuingie barabarani tukipiga makelele tumebakwa! tumebakwa! tupambane na mtu asie na utu wala kuheshimu maisha ya mtu,ili tukaangwe kwa risasi kama wanavyo fanyiwa DRC , Burundi nk. Hatujayasahau yaliotokea Pemba yenye sura kama hii, damu ya wazanzibari ilimwagika, hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliofikishwa mbele ya haki. Damu ya wazanazibari "is more precious" kuliko mkandamizo wa mtawala Tanganyika.What did you do kuhusiana na huo ukiukwaji wa haki za msingi za binaadamu?
Mtamuelewa lowassa kwa nini alisema 2020 wataingia ikulu kiulaini
Lowassa alisema upinzani usipochukua dola 2015 utasubiri miaka mingine 50.Kama UN haikuingilia kati 2001 ilipomwagika damu Zanzibar mpaka kukawa na wakimbizi,haya ya Maalim Seif kuzungukazunguka duniani Mara ICC Mara UN,ni maigizo tu.Pengine ndo style yake ya kutafuna ruzuku ya chama.Mtamuelewa lowassa kwa nini alisema 2020 wataingia ikulu kiulaini
Ktk ile safari yao ya UN na mapicha kibao akiwa mbele ya mimbar ya UN ilikuwa usanii auZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda, anaandika Jabir Idrissa.
Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”
Katika tamko walilolitoa na kufikishwa mbele ya Mkutano wa 33 wa Baraza hilo uliofanyika Septemba mosi mwaka huu, Liberal International imetaka jumuiya ya kimataifa, kufikiria kuweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali za watu wote walioshiriki kuidhinisha vitendo vya utesaji wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao.
Taasisi hiyo ambayo CUF ni mwanachama wa muda mrefu, imetoa wito kwa wabunge wanaofuata mtizamo wa kiliberali walioko upande wa serikali na upinzani katika mataifa yote duniani kuchukua msimamo imara kupitia mabunge ya nchi zao na kutoa matamko ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”
“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI.
Hatua hiyo ya LI kuandikia Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa inakuja wiki kadhaa baada ya Maalim Seif kukutana na taasisi mbalimbali za kimataifa zinazoshughulikia maendeleo ya demokrasia na utawala bora, pamoja na wakuu wa serikali za Marekani, Ulaya na Canada.
Maalim Seif aliyefuatana na baadhi ya wasaidizi wake pia alifika Mahakama ya Uhalifu wa Kivita ya The Hague, Uholanzi ambako aliwasilisha malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu unaofanywa Zanzibar kwa idhini ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hatua ya Maalim Seif na CUF imekuja baada ya CCM kumuamuru Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, 28 Oktoba, baada ya kubaini kuwa chama hicho kimepoteza madaraka kupitia sanduku la kura.
Chanzo: Mwanahalisi Online
Kanuni ya uchaguzi ni "the winner takes it all ". Hata kama asilimia 99 % ya wapiga kura wa Pemba hamkumchagua Magufuli, lakini kuna asilimia 1% tuu ndio waliomchagua, lakini mwisho wa siku the overall winner ni Magufuli, then, Magufuli as the winner takes it all zikiwemo kura za Wapemba wote kwa sababu uchaguzi umekwisha aliyeshinda ndie rais wa wote, waliomchagua na wasio mchagua! .Wape Moyo mahafidhuna wenzako, Magu kaja zanzibar povu juu na unafiki kuwagawa Wazanzibari, eti kuwashukuru wa pemba kwa kuichagua ccm, kaangalie zile kura zake pemba alipata ngapi na Lowassa. Shame on you, nilikuwa nakuona mtu makini sana kumbe huna maana, unaongea utumbo siku hizi kwa elf 7500 unazo lip wa na ccm
Kujulikana ndio nini kama huna dola?, nakiri Zanzibar Kujulikana sana as an exotic tourist destination lakini not inside UN or International Bodies and Organisations, yenye recognition ni Tanzania, take it or leave it! .Zanzibar inajuulikana sio tu UN lakini duniani kote kuliko Tanganyika au Tanzania. Safiri uujue ukweli huo unaouma. Hata hao Bongo fleva wanapokwenda hapo tu Afrika ya Kusini wanapopata taabu ya kujibu mswali. Wanaposema Dodoma wanaulizwa iko Zanzibar. Kila kizuri kuhusu Tanganyika jibu ni Zanzibar. Pasco maneno yako haya nimeyahifadhi na panipo uhai nitakukumbusha. Zanzibar katika dunia hii ni matusi kuifananisha na Tanganyika kwa kila kitu labda kwa kuchunana ngozi na kuuwa vikongwe na albino.
Chuki zako dhidi ya wazanazibari ni sawa mwanamke aleinyimwa unyumba. Hivi wewe unataka tuingie barabarani tukipiga makelele tumebakwa! tumebakwa! tupambane na mtu asie na utu wala kuheshimu maisha ya mtu,ili tukaangwe kwa risasi kama wanavyo fanyiwa DRC , Burundi nk. Hatujayasahau yaliotokea Pemba yenye sura kama hii, damu ya wazanzibari ilimwagika, hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliofikishwa mbele ya haki. Damu ya wazanazibari "is more precious" kuliko mkandamizo wa mtawala Tanganyika.
Hahaha Pasco,Zanzibar wanananue Umeme kutoka Tanganyika,Tanesco haitaki kukosa mamikioni ya pesa yakila mwezi na ndio maana hawaukati umeme ZanzibarKujulikana ndio nini kama huna dola?, nakiri Zanzibar Kujulikana sana as an exotic tourist destination lakini not inside UN or International Bodies and Organisations, yenye recognition ni Tanzania, take it or leave it! .
Hili la chuki dhidi ya Wanzibari laiti ungelijua! . Almanusura nibadili dini na kusilimu shauri ya Mzanzibari! . Kiukweli tunawapendeni kuliko, utashuhudia sisi huku bara tukikatiwa umeme lakini wenzetu umeme wetu bure na hawakatiwi! . Visiwa vyenyewe havijai hata kwenye kiganja ila vina mgao wa 4.5%ya misaada yote ya nchi! . Tuko kwenye muungano lakini anayebeba gharama zote za kuendesha muungano ni msharika mmoja tuu, mwingine kazi ya ni kubebwa tuu na gubu lisiloisha!.
Mnaitaka mpendwe vipi?.
Pasco