Kilimo kutofundishwa shule ya msingi ni kasoro kubwa kwa rasimu ya mtaala

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
679
824
Bado hali ya uchumi wa nchi yetu ktk sehemu kubwa ya taifa letu Wananchi hujishughulisha na kilimo na bado inasemekana uchumi wetu hutegemea kilimo.

Kwa kutofundishwa somo la kilimo ni tafsiri halisi kuwa hata Wananchi huko wanakolima hawatathamini kilimo na baadae wageni wawekezaji watakuja kuwekeza ktk kilimo hapo na wenyeji wataendelea kuwa watumwa ktk uchumi wao.
 
Bado hali ya uchumi wa nchi yetu ktk sehemu kubwa ya taifa letu Wananchi hujishughulisha na kilimo na bado inasemekana uchumi wetu hutegemea kilimo.

Kwa kutofundishwa somo la kilimo ni tafsiri halisi kuwa hata Wananchi huko wanakolima hawatathamini kilimo na baadae wageni wawekezaji watakuja kuwekeza ktk kilimo hapo na wenyeji wataendelea kuwa watumwa ktk uchumi wao.
Shida ni kwamba mtalima kisasa,mtapata hela nyingi sana hivyo tutashindwa kuwatawala
 
Naileta kwenu kama nilivyopokea.

Mapendekezo ya rasimu ya ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Maboresho ya Mitaala ambayo yanaenda kubadilisha mfumo wetu wa elimu.

Na Baltazari Luhanga.
  1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.
  2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).
  3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.
  4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa Kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, Kiswahili kitakuwa kama somo kwa shule za English medium.
  5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.
  6. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.
  7. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, Kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, Historia ya Tanzania na Maadili, Dini na Kiingereza, na Stadi za Kazi itachopekwa.
  8. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na Kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiingereza.
  9. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.
  10. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.
  11. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
  • Kilimo na ufugaji
  • Umakenika
  • Biashara na ujasiriamali
  • Sanaa bunifu
  • Elimu ya michezo
  • Ufugaji wa nyuki
  • Uchimbaji wa madini
  • Urembo
12. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.
13. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
  • Hisabati
  • Elimu ya biashara
  • Kiingereza
  • Historia ya Tanzania na Maadili
14. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
  • Cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
  • Cheti cha amali (NACTVET)
15. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.
16. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwa ajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.
17. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.
18. Coding itafundishwa shule ya msingi.
19. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.
20. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.
21. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala ya 7 ya sasa.
22. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwa sababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi, kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.
23. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.
24. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.
25. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.
26. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
  • Sanaa
  • Lugha
  • Muziki
  • Michezo
  • TEHAMA
27. Masomo ya O-level yatakuwa:
  • Biology
  • Physics
  • Chemistry
  • History
  • Geography
  • Historia ya Tanzania na Maadili
  • Hisabati
  • Kiswahili
  • English
  • Elimu ya biashara
  • Utunzaji wa taarifa za fedha
  • Computer Science
  • Bible Knowledge
  • Elimu ya dini ya Kiislamu, nk.
28. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.
29. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwa sababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.
30. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.
31. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada (cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.
32. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uhandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.
33. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.
34. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.
35. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.
36. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.
37. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwa sababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.
 
Naileta kwenu kama nilivyopokea.

MAPENDEKEZO YA RASIMU YA RIPOTI YA KAMATI YA KITAIFA YA MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU* .

Na Baltazari Luhanga.

1. Mtihani wa darasa la saba utafutwa. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize kidato cha nne.

2. Kutakuwa mtihani wa upimaji wa kitaifa wa darasa la sita (Standard Six National Assessment).

3. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza kidato Cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza.

4. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa Kama somo kwa shule za Kiswahili medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa shule za English medium.

5. Elimu ya msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6, tofauti na ya sasa miaka 7.

7. Elimu ya awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5.

8. Masomo ya elimu ya msingi yatakuwa KKK, Jiografia, kiswahili, Sanaa na michezo, hisabati, sayansi, historia ya Tanzania na maadili, dini na kiingereza na stadi za kazi itachopekwa.

9. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

10. Shule zenye uwezo zitafundisha walau somo moja la lugha za kigeni kama kichina au kifaransa.

11. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na amali (ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na
uwezo, matakwa na malengo yake ya badae.

12. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani za:
-kilimo na ufugaji
-umakenika
-biashara na ujasiriamali
-sanaa bunifu
-elimu ya michezo
-ufugaji wa nyuki
-uchimbaji wa madini
-urembo

13. Mwanafunzi wa mkondo wa amali atatakiwa kuchukua masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

14. Masomo ya jumla la wanafunzi wa amali ni:
-hisabati
-elimu ya biashara
-kiingereza
-historia ya Tanzania na maadili

15. Wahitimu wa amali watapata vyeti viwili yaani:
-cheti cha ujumla cha elimu ya sekondari (NECTA)
-cheti cha amali (NACTVET)

16. Kila shule itakuwa na wakala wa VETA ili kusimamia maswala ya ufundi.

17. Kila shule haitakuwa na mikondo zaidi ya miwili ya ufundi, hii ni kwaajili ya ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

18. Kutaanzishwa somo jipya la mawasiliano ya kitaaluma (academic communication) katika A-level na ualimu.

19. Coding itafundishwa shule ya msingi.

20. Information and Computer Studies (ICS) itabadilishwa na kuitwa Computer Science. Somo limesukwa upya.

21. Civics itaunganishwa na historia ya Tanzania na maadili kwa O-level.

22. O-level masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

23. Katika O-level masomo ya Biology na Geography yatakuwa masomo ya kuchagua pia kwasababu maudhui yake yamekuwa kwenye masomo ya jiografia na sayansi ya shule ya msingi kwa mfano afya ya jamii, afya ya uzazi, magonjwa ambukizi nk.

24. Civics, maarifa ya jamii, uraia na maadili yamefutwa. Maudhui yake yameingia katika somo la historia ya Tanzania na maadili.

25. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na maudhui yake yatawekwa katika somo la historia ya Tanzania na maadili na mawasiliano ya kitaaluma.

26. Kufuta baadhi ya masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudia rudia kwa maudhui.

27. Michepuo katika elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9). Michepuko iliyoongezeka ni:
-sanaa
-lugha
-muziki
-michezo
-TEHAMA

28. Masomo ya O-level yatakuwa:
-biology
-physics
-chemistry
-history
-geography
-historia ya Tanzania na maadili
-hisabati
-kiswahili
-english
-elimu ya biashara
-utunzaji wa taarifa za fedha
-computer science
-bible knowledge
-elimu ya dini ya kiislamu etc

29. Astashahada ya ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (diploma) ya elimu ya awali, ualimu wa msingi na ualimu wa elimu maalumu. Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza kidato cha sita na itasomwa kwa miaka miwili.

30. Walimu wa sekondari wote watakuwa na Shahada (degree). Kwasababu nchi nyingi ndio wanaenda muelekeo huu.

31. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (diploma) ya ualimu wa sekondari vitatumika kutoa continuous professional development.

32. Walimu watakaofundisha mkondo wa amali (ufundi) watakuwa Wahitimu wa kozi mbalimbali za amali na watapewa astashahada
(cheti) ya ualimu huo kwa miezi 6.

33. Vyuo vya elimu ya juu vitaanzisha kozi za ualimu wa uandisi, urembo, uvuvi, sanaa bunifu nk. Hii itasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu katika maeneo hayo ya ufundi.

34. Kutakuwa na internship kwa walimu kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kumaliza ualimu ili wawe
na umahiri zaidi. Kisha walimu watapata leseni.

35. Mafunzo kwa vitendo ya walimu tarajali yatafanyika katika shule zilizo karibu na vyuo vya ualimu ili zifanyike kwa umakini zaidi.

36. Kutakuwa na motisha kwa walimu na upandaji wa madaraja utakuwa kwa utaratibu mzuri.

37. Bodi ya usajili wa walimu itaanza kufanya kazi.

38. Utekelezaji wa mtaala mpya na sera ya elimu ya mwaka 2023 itaanza kwa awamu kwa darasa moja moja katika kila level. Hii itasaidia kwenda sawa na bajeti kwasababu kuanza kwa madarasa yote na levels zote ni gharama kubwa sana. Utekelezaji utaanza mwaka 2024 kama sera na mtaala zitapitishwa kama ilivyo.
Ahsante Sana kiongozi.
 
Nani alimfundisha kilimo bibi yako ? Nani akiwafundisha bodaboda, machinga, wadangaji , wanaobeti na mama ntilie?

Huyo Bakhresa amesoma chuo gani cha biashara?

Waliosoma shahada za kilimo kule SUA mashamba yao yako wapi??

Waliosoma shahada za biashara vyuo vikuu maduka yao yako wapi??
 
Nani alimfundisha kilimo bibi yako ? Nani akiwafundisha bodaboda, machinga, wadangaji , wanaobeti na mama ntilie?

Huyo Bakhresa amesoma chuo gani cha biashara?

Waliosoma shahada za kilimo kule SUA mashamba yao yako wapi??

Waliosoma shahada za biashara vyuo vikuu maduka yao yako wapi??
Kwa sasa kama taifa tunataka kufanya mambo kwa weledi wenye tija kubwa ya ushindani wa uzalishaji na soko la dunia ktk ajira, siyo kulima kwa mazoea ktk kipindi ambacho hata mabadiliko ya tabianchi yameathiri ardhi na mazingira kwa ujumla.

Kama ndivyo unavyosema kwa nini historia na kiswahili yamepewa kipaumbele wakati baby zetu wanatuhadithia na kiswahili tunakizungumza kila siku?

Kilimo liwe somo halisi ili tuandae watoto wetu kutumia ardhi vizuri na si kuchukua kilimo.

Pili mbona kuna fani ya makenika inayohusiana na physics iko ktk ufundi na physics bado ni somo toka shule ya msingi na sekondari vivyo hivyo hata kilimo kianzie msingi na sekondari ikibidi hata kwa baadhi ya mikoa walau mikoa yenye miji/ majiji yasiyo na kilimo wao wanaweza kuacha kusoma kilimo.
 
Back
Top Bottom