Mbunge Jumanne Kibera Kishimba Aishauri Wizara ya Elimu Kuhusu Mtaala na Sera ya Elimu Inayokuja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE JUMANNE KIBERA KISHIMBA AMETOA USHAURI KWENYE KONGAMANO LA MITAALA NA SERA YA ELIMU

Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini, Mhe. Jumanne Kibera Kishimba ametoa maoni yake kwenye Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu Tanzania lililofanyika Jumapili ya tarehe 14 Mei, 2023 Jijini Dodoma.

"Elimu yetu iliyoandikwa ni asilimia 5 tu ya Elimu Duniani na Dunia inakwenda haraka. Kama kitatokea chochote Wizara ya Elimu wawe wanakiingiza ndani ili kwenda haraka na Dunia. Tunachelewa sana" - Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kinachotupa shinda wote ni kwamba, kwanini hawa ambao ni darasa la kwanza mpaka darasa la saba mpaka kidato cha nne [Form Four] ndiyo wanaonekana kuishi maisha ahueni hata Serikali haiteseki nao? - Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kwanini Serikali hiyo hiyo inateseka na watu ambao wamesoma?. Wazazi wanateseka kuhakikisha anapata kazi na kumkarisha, Serikali inateseka pia kumtafutia ajira. Lakini, maana ya kwenda Shule ni nini? Ndiyo maana ya kuanza kwa huu mjadala" - Jumanne Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Maana ya kusoma ni nini? Maana ya kusoma ni kuja kumpunguzia matatizo mzazi. Inawezekanaje mtu aliyesoma ndiyo aendelee kuwa mzigo kwa Serikali na Mzazi? Nafikiri ndiyo hoja yetu ya Msingi ipo hapo" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge wa Kahama Mjini

"Suala la umasikini, sisi ambao ni wawakilishi wa wananchi tunalifahamu Suala la umasikini kwa wananchi wetu. Lakini Elimu yetu inasema wewe utafuata utaratibu huu. Hakuna mahali ambapo inaliongelea suala la umasikini. Kuna wakati Bungeni tunazozana, kwanini Shule binafsi wasomee daftari hili na hawa wengine wasomee hili" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kuzaa na kuwa na mali havina mahusiano. Mtu anaweza kuwa hana mali akawa na watoto wengi. Na huyu mwenye mali akahangaika kupata mtoto. Mtaala wetu lazima uliangalie hili huyu mwenye watoto anaingiaje. Anaweza kuwa na watoto wenye akili kabisa lakini hana uwezo" - Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Elimu yetu tumeirithi kutoka Uingereza. Uingereza kama una watoto wanne wanaangalia mshahara wako unaweza kutunza watoto wangapi. Kama un unaweza kutunza watoto wawili hawa wengine wawili Serikali inakusaidia. Sisi huku Tanzania hakuna kitu kama hicho." - Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Tunaweza kupeleka mabadiriko Kijijini lakini wananchi wasipokee kama tulivyopeleka kwasababu suala la umasikini hatuliangalii" - Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Muda wa kufunga shule umetuathiri sana Kijijini kwa sababu ni utaratibu ambao umetoka Ulaya kwamba wakati wa baridi wakoloni walikuwa wanafunga shule na sisi tukarithi kulekule. Muda wa Masika kama tutafunga shule itawasaidia Wazazi kuwa na wanafunzi wao kwenye shughuli za kilimo" - Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Mtoto afundishwe Elimu ya kujitegemea ya kiuchumi. Uchumi darasa la kwanza. Kinachompeleka mtu kwenda kujiajiri ni faida anayoipata kule. Kinachomfanya Mtoto apende kazi ya kujiajiri na kujitegemea ni faida anayoipata kule" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kwenye vitabu vyetu tueleze kwamba nikilima Mahindi matano ni sawa na kilo moja ya Mahindi ambayo ni Shilingi 1000 kwa bei ya leo na ndoo moja ya Maji inaweza kumwagilia Mahindi labda 50. Huyu mtoto kichwani anakuwa na akili akiwa bado darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Utamzuiaje rushwa mtu kama wewe unamkataza kuelewa namna ya kutafuta hela? Atakapojua namna ya kumwagilia Mahindi wakati wa kiangazi atajua ugumu wa hela, kwahiyo hawezi kununua chocolate ataitunza pesa. Ukikataa atakwenda ataingia kwenye rushwa maana rushwa ndiyo njia rahisi. Lakini kama atakuwa amefundishwa itatusaidia sana darasa la kwanza" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kwa sisi Mikoa ya Shinyanga na Mwanza, Pamba asilimia 80 hailimwi na wazee wenye familia maana ni kama kazi ya ziada (Extras) ni kama kilaba (Part time). Ifundishwe shuleni, ieleze faida na bei, isije ikasema labda watoto wataharibika" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Mtoto akifika darasa la tatu akaharibika lakini anashinda shambani itakuwa ni kosa akawa mtoro anatorokea shambani? Tunajihofia nini? Hamna kesi yoyote. Kama anapenda kusoma aende hata jioni lakini si aende shambani kwake? - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Sualaa VETA; Gari binafsi huwa hatuulizi fundi wa gereji amesoma wapi. Hata chakula huwa hatuulizi. VETA anatumia muda mwingi sana kumkalisha mtoto lakini kinachofanyika huku uraiani sicho anachozalisha (produce) VETA." - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"VETA hawana hata mtaala wa simu, na tuna simu zaidi ya Milioni 50. VETA hawana mtaala wa kutengeneza Pikipiki. VETA hawajui kutengeneza Madirisha ya Aluminium. Unajenga VETA unamwambia mtu aende VETA akafanye nini? Wakati mtaani anaenda kufundishwa kwa dakika tano anaelewa na mteja anakutana naye kulekule" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Hawa watu wa mtaani sasa hivi wanaishi pekee yao kabisa na hakuna mahala elimu inatumika. Wanachukua ile yenye faida ndiyo wanakwenda kuitumia hii nyingine wanaacha" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Kinachotupa shida, mtoto wangu kuanzia ana miaka 6 & 7 unamuona ni mchangamfu, kadiri anavyoendelea mpaka anakuja kumaliza kwenye GPA anarudi kazorota kabisa. Je, tatizo liko wapi? Tatizo lipo kwenu GPA mnazompa ni kubwa mno anachanganyikiwa au ni nini kinaendelea? - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Huyu aliyebaki darasa la saba na kidato cha nne unamuona kweli ni mtu unaweza kumuacha hata dukani. Huyu wa GPA kubwa unaogopa hata kumuacha dukani" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Suala la maboresho ya Elimu halikuwagusa watu wa elimu ya juu, lakini kule si ndiyo chanzo tunapata watu wamezorota, kwanini wanazorota? Kwanini tunamuhangaisha Mhe. Bashe kuanza kuwatafutia mahali pa kulima? - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Hawa darasa la saba ni lini mliwatafutia, si wanalimaga wao tu! Kule usukumani mtoto miaka 4 anaweza kusaidia kung'oa Mbegu za Mpunga. Miaka 5 kabla hajaenda shule Lazima apande Mpunga. Ndiyo huu mnaotaka kila siku utelemke bei. Unalimwaga na wazee? Unalimwa na hao hao" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini

"Huyu mwananchi wa kawaida masikini anampataje mtoto ambaye atakuwa mzuri. Kesi ya ajira mtapambana nayo wenyewe. Sisi tunataka huyu mtu aliyesoma akirudi nyumbani tuwe tunaweza kufanya naye kazi. Ndiyo hoja yetu kubwa. Mkituondolea hilo tutakuwa tumefanya vizuri sana" - Mhe. Jumanne Kibera Kishimba, Mbunge Kahama Mjini
 

Attachments

  • pic-kitukosad.jpg
    pic-kitukosad.jpg
    115.7 KB · Views: 5
  • maxresdefaulta.jpg
    maxresdefaulta.jpg
    99.1 KB · Views: 4
Kuna Watu humu wana elimu kubwa na wanawabeza sana darasa la Saba

Ila nawahakikishia nondo Kama Hizi sio prof.lipumba, dr.bashiru au kabudi wanaweza kuzishuka kwa mpangilio Safi,wenye mantiki na unaoeleweka Kama huu.

Kila haya imebeba Maneno mazito Sana
 
Kishimba kashuka nondo nzito balaa
Hawa ndo wakupewa PhD sio kina nanihii
Kwa kuongea hajambo ana biadhara kibao tena kubwa kilichonishangaza ni yeye kulalamika bungeni kuwa mwanae kamaliza digrii na hajapata ajira

Anashindwa nini kumwajiri kwenye biashara zake kana wanavyofanya wahindi,waarabu

waandishi wa habari watafute watoto wake wawahoji.au wMgoji yeye mwenyewe.watoto.wake kawaajiri kwenye kampuni zake? Wapi? Ili wakawahoji na kama hajawaajiri aseme ni kwa nini?
 
Kishimba ni muelewa sana. Kuna kipindi nilikua nafanya nae biashara kwa mfufulizo hakika hana kona kona.
 
Kasema vizuri sana. Hasa alipomsema. Watoto wa manda ya ziwa wafundishwe mpunga.
Kusisitiza hili ningeshauri elimu itolewe kulingana na maeneo. Mfano. Watoto wa Moshi wawe na mtaala wa kilimo cha kahawa, mahindi. Wa Mtwara, Lindi, Kwanu wafundishwe Korosho. Wa kigoma michikichi. Mbeya, Iringa, Rukwa, Katavi mahindi.
Manda ya ziwa mpunga, mifugo, madini.

Hiyo ndio ingekuwa mitaala ya shule. Akifaulu anakuwa anajua kilimo na ufugaji
 
Tufunge shule wakati wa masika Ili wanafunzi wasaidie kazi za shambani- kishimba
Mwanafunzi akitoroka shuleni akaenda shambani hana kosa- kishimba
 
Hizi points hata maprofesaa hawawezi kuzitoa.
Kweli akilinna elimu ilitangulia akili.
 
Kwa kuongea hajambo ana biadhara kibao tena kubwa kilichonishangaza ni yeye kulalamika bungeni kuwa mwanae kamaliza digrii na hajapata ajira

Anashindwa nini kumwajiri kwenye biashara zake kana wanavyofanya wahindi,waarabu

waandishi wa habari watafute watoto wake wawahoji.au wMgoji yeye mwenyewe.watoto.wake kawaajiri kwenye kampuni zake? Wapi? Ili wakawahoji na kama hajawaajiri aseme ni kwa nini?
Anawasemea watoto wa watanzania wengine.anatuwakilisha SIsi wa tandale Kwa mtogole.
 
Kuna Watu humu wana elimu kubwa na wanawabeza sana darasa la Saba

Ila nawahakikishia nondo Kama Hizi sio prof.lipumba, dr.bashiru au kabudi wanaweza kuzishuka kwa mpangilio Safi,wenye mantiki na unaoeleweka Kama huu.

Kila haya imebeba Maneno mazito Sana
Halafu ni Kiswahili sanifu...hakuna vijimaneno vya Kiingereza
 
Huyu mzee ana akili sana kuliko yule aliyekua na PhD ya mchongo ya maganda ya korosho
 
Street education hata japan ipo, ukisema ufundishe kila kitu kinacho fanyika ni impossible.

Sio lazima veta wafundishe kila kinacho fanyika mitaani..
 
Back
Top Bottom