Serikali ifanye lugha ya alama kuwa moja ya somo kwa shule za msingi

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu kwema? Twende moja kwa moja kwenye mada.

Watu wanaotumia lugha hii ni wachache ukilinganisha na wengine tunaoweza kuwasiliana kwa sauti/maneno. Kutokana na hii, watu wenye ulemavu huu wa kusikia hupitia changamoto kubwa toka watoto mpaka ukubwa wao.

Fikiria uko na mtoto mwenye changamoto hii, shule zenye kuwahudmia ni chache, lakini pia inakuwa changamoto kwasababu watoto wengine hawawezi kuwasiliana nae, hivyo wengi wanaishia kutengwa au kufungiwa ndani muda mwingi kwa uoga kwamba hata ikitokea amepotea au amepata changamoto kwa mazingira ya mbali kidogo na nyumbani ni vigumu kupata msaada.

Lakini fikiria kama lugha hii ingekuwa inafundishwa kwa ngazi ya shule msingi, watu hawa wenye changamoto hii wanakuwa hawaachwi nyuma, popote anapokuwa akipata changamoto inakuwa rahisi kupata msaada sababu watu hatakosa hata watu wanaoweza kuwasiliana naye popote alipo, na hata fursa za kiuchumi zitaongezeka upande wao.

Kwa sasa elimu hii inatolewa kwa watu walioathirika tu nchini au wanaotaka kuwa watafsiri wa lugha hiyo, ambayo inasaidia kwa baadhi ya matukio kama ya kiserikali wasipitwe na kinachoendelea maana mara nyingi huweka watafsiri, lakini hili halitoshi.

Fikiria wanakosa fursa ngapi sababu hakuna watu wa kutafsiri lugha lugha hiyo, kwa jinsi mambo yalivyo sasa ni kama hawaishi nasi, yaani hawa-exist, mambo mbalimbali yanafanywa kwa kuangalia/kuzingatia wanaosikia tu, fikiria huduma karibu zote za kijamii tunazopata, kama unachangamoto ya kusikia inadibidi ufanye kazi ya ziada kuzipata.

Teknolojia imekua na kuna vifaa vinavyowasaidia watu wenye changamoto hii kusikia, lakini vifaa hivi ni ghali sana kwa kila mtu kumudu. Hii ni fursa pia kwa wavumbuzi kuwekeza upande huu na kutatua changamoto hii kuendana na mazingira yetu pamoja na hali ya uchumi.

Hili halituzii kama taifa kupata ufumbuzi mwingine wa kukabiliana na jambo hili, kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma, kuwa na lugha hii kama moja ya somo kwa ngazi ya msingi itapunguza kwa kiasi kikubwa gap hii ambayo ipo kati ya wanaosikia na wenye ulemavu wa kutosikia.

Kwenu wakuu.
 
Wazo zuri sana,nimewahi kushuhudia mtoto mdogo aliyekuwa anasoma shule ya viziwi mikumi akiwa na mama yake,mtoto yule alijitahidi kuonyesha ishara kwa mama yake lakini mama yake hakuwa anaelewa chochote,hivyo basi mama yule aliishia kutabasamu tu bila kujua chochote.
Hili ni wazo zuri sana,hongera mkuu kwa wazo zuri.
 
Wasome kuanzia Olevel, liwe option, sio lazima, au iwekwe kama topic tu kwenye kiswahili, tusijaze masomo mengi sana, tuongeze tu biashara na uchumi iwe lazima
 
Ni kweli Mkuu
 
Wasome kuanzia Olevel, liwe option, sio lazima, au iwekwe kama topic tu kwenye kiswahili, tusijaze masomo mengi sana, tuongeze tu biashara na uchumi iwe lazima
Shule ya msingi ina masomo mangapi kwani? Na hii haii haitaathiri alama za mwanafunzi kwenye masomo yake core, kwenye biasha na uchumi labda elimu ya kupanga bajeti/ku-manage finance hili ni somo muhimu ambalo linahitajika sana kwenye maisha lakini hufundishwi shuleni lakini sio uchumi na biashara kwa ujumla wake
 
Watoto wa shule ya msingi wana masomo nane kama sikosei, ila wanayofanyia mtihani ni matano,

Uchumi na biashara ni kitu cha kila siku, ni muhimu kwa kila mtu kujua kodi, na jinsi ya kufanya biashara hususani wakati huu ajira zipo chache na wahitimu wengi,

Wazo lako zuri, iwe ni topic kwenye kiswahili, watu wajifunze
 
Back
Top Bottom