Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na masoko

K

kido madini

JF-Expert Member
223
250
Bei yake kwa kilo tafadhali
mi hapa ntakuuzia debe kwa laki 5 achana na habari za kilo na debe moja lina kilo 8 mpaka 12 inategemea ililimwa wapi kama kwenye mbuga inakupa mpaka kilo 12 wakati za makampuni tofauti yake ni kwamba zenyewe wanasafisha kwa mitambo wakati akina sisi tunasafisha kwa wakina mama kupeta kwenye upepo hizo za kilo bei zake ya chini 180000 na ya juu 320000/kg so jiongeze kuwa mwepesi ongeza spidi na kazi ya kufikiria hili
 
Elifuraha Bussism

Elifuraha Bussism

JF-Expert Member
207
250
Mbegu zipo na kwa debe ni TSH 250,000/ mpaka 300,000/ kitunguu chekundu yaani Red Bombay.
 
Vangigula

Vangigula

JF-Expert Member
412
1,000
Ni ainagani ya mbegu ya vitungu ambayo niya mda mfupi kama ya siku 90 naombeni ushauri na msaada juu ya hili
Kwa uzoefu wangu wa kilimo cha kitunguu, mbegu ya muda mfupi zaidi ni CV 6070 inayozalishwa na Monsanto (75-80 days). Changamoto yake ni bei, nadhani hadi sasa ndiyo mbegu inayouzwa aghali zaidi. Mbegu nyinginezo zinaanzia siku 90-120, kutegemeana na matunzo, Hali ya hewa etc.
 
mtimkav

mtimkav

JF-Expert Member
1,043
2,000
Nakushauri ukiipata fanya majaribio kwenye small scale maana hakuna utapeli kama ulioko kwenye mbegu hapa Tanzania
 
M

Marco J Massawe

New Member
2
20
Wana Jf habari. Naomba kujuzwa katika mkoa wa Dar es salaam ni maeneo gani mazuri ya kulima kilimo cha vituguu?
 
Doubleg Mwamasangula

Doubleg Mwamasangula

JF-Expert Member
1,145
2,000
Wana Jf habari. Naomba kujuzwa katika mkoa wa Dar es salaam ni maeneo gani mazuri ya kulima kilimo cha vituguu?

Daa ivi DSM kuna mashamba mkuu?
Labda tafuta ardhi mkoa jirani yaani wa pwani
Ila kwa dar hakuna mashamba boss
 
aldeo

aldeo

JF-Expert Member
952
1,000
Jamani wenye experience na kilimo Cha kitunguu maji nahitaji kujua vitu kadhaa:

1. Mbegu ya dukan na inayozalishwa mtaan na wakulima ipi n nzuri?
2. Kama n dukan mbegu ya kawaida na hybrid tofaut yake n nn kwenye hatua zote kuanzia kusia had kuvuna?

3. Ipi n mbegu Bora kabisa na Kama ikitunzwa vizuri Kama inavyotakiwa naweza pata gunia ngapi kwa hela?

4. Wapi nitapata mbegu nzur nabora maeneo ya Arusha na jiran mwake?

5. Kwawale mliopo Arusha naona vitunguu vingi sanasana kipindi hiki n bonge la kituu ya Kama Nazi hyo n mbegu gani vp ABCD zake kwenye ulimaji.

6. NIWEKENI KWENYE GROUP ZA KITUNGUU 0787485865
 
joboychali

joboychali

Senior Member
169
225

Ukubwa wa kitunguu Ni matokeo ya mbolea ya CAN

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MNYAMU ZE KB

MNYAMU ZE KB

Senior Member
158
225
Naomba mwenye utaalamu wa kilimo cha vitunguu swaum anisaidie ikiwa ni
Hali ya hewa
Muda sahihi wa kupanda( Nyanda za juu kusini na manyara na ruaha?
Muda wa zao kukomaa toka ulipopanda
Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
6,470
2,000

UTANGULIZI

Vitunguu saumu ni zao ambalo lipo katika jamii ya vitunguu na hufanana sana na vitunguu maji, zao hili linatumika sana duniani kama kiungo cha chakula na wengine hutumia kama dawa.

ASILI YAKE

Vitunguu swaumu asili yake ni maeneo ya Mediterranean na China, Asia lakini pia usitawi katika nchi za kitropik kwa hapa tanzania ustawi katika mikoa ya singida,Arusha,Iringa na Mbeya. pia utumika kama kiungo cha chakula dawa kwa binadamu na wanyama pia na pia utumika kutengeneza mafuta pia harufu yake kali ufukuza wadudu waalibifiu shambani.

hivyo shamba la vitunguu swaumu haliwi na wadudu wa halibifu sana ukiringanisha na mazao mengine.

AINA ZA VITUNGUU SWAUMU

Vitunguu swaumu vipo vya aina mbalimbali nazo ni:=

i) Antichoke – Hii kwa mbali inaonekana kama ni nyekundu lakini sio iliyokolea

ii) Soft neck – Kwa rangi ni nyeupe inatumika sana kwasababu hachukua mda mfupi shambani

iii) Silver skin – Hivi vina rangi nzuri ya silver na mara nyingi hutumiwa na wasindikaji maana vinadumu mda mrefu bila kuharibika.

HALI YA HEWA & UDONGO

Vitunguu saumu hulimwa kiasi cha mita 1800 au zaidi kutoka usawa wa bahari na mvua kiasi cha mm 1000 au zaidi na joto kiasi udongo tifutifu na mnyevunyevu na usio tuamisha maji ndio unafaa kulima vitunguu saumu.

UTAYALISHAJI WA SHAMBA

Shamba linapaswa kutayarishwa mapema kabisa, lima na akikisha udongo ni tifutifu na pia unaweza kutengeneza matuta kwaajili ya kupanda weka samadi shambani wiki 2 kabla ya kupanda.

UTAYALISHAJI WA MBEGU

Mbegu ya kitunguu swaumu ni ile punje (vikonyo) inayokuwa imebanguliwa kutoka kwenye kitunguu au tunguu iliyokomaa kabisa, kiasi cha kilo 300 – 500 hutumika kwa hekari moja na inatakiwa uchague mbegu isio na magonjwa au isio dhaifu.

UPANDAJI

Tabia ya mmea wa Vitunguu swaumu humea huanza kuota kipindi cha baridi ( miezi yenye baridi), kwa Tanzania kipindi ambacho hakuna joto ni miezi ya May mpaka August, Unachukua kitunguu swaumu na kutenganisha vitunguu kimoja kimoja (bulbs) na kuchagua vile vikubwa maana hivi ndivyo vitakavyo kupa mazao mengi na bora, nafasi kati ya kitunguu na kitunguu ni sentimeta 5 na kati ya mistari ni sentimeta 20 na kushuka chini kiwe na wastani wa inchi 2.5 .
Baada ya kupanda pandishia udongo na uukandamize kuhakikisha kwamba kimekaa vizuri na hakiwezi kuathiriwa na mvua au maji wakati wa kumwagilia ili kisikae upande au kung’olewa kabisa. Uotaji mzuri hutegemea pia namna vitunguu swaumu vilivyo hifadhiwa kabla ya kupandwa, kama vilihifadhiwa sehemu zenye joto na hewa finyu uotaji wake utakuwa duni na dhaifu. Pandia TSP kilo 40 kwa eka au kilo 100 kwa hekta.

MBOLEA

Mbolea huwekwa baada ya palizi, tumia mbolea ya kukuzia CAN au UREA. CAN kiasi cha kilo 75 kwa eka au 190 kwa Hekta au UREA kiasi cha kilo 40 kwa eka na 100 kwa hekta na palilia mara mbili au zaidi ili kuweka shamba katika hali ya usafi.

UPALILIAJI

Kuwa na juhudi ya kupalilia ili kuipa uhuru mimea kumea vizuri na kulifanya shamba lako kuwa safi, Palizi ya kwanza ifanyike mapema mara tu magugu yanapo tokeza wakati vikonyo vimesha chipua na baada ya palizi ya kwanza ndipo weka mbolea.

Unaweza kupulizia dawa ya kuua magugu endapo vitunguu vimeshaota kama vile Bromoxynil ambayo uua majani mapana na fusilade uua nyasi. Mmea unapoendelea kukua na kutoa maua yaache majani yarefuke mpaka yajikunje, ndipo utayakata ili kuongeza uzalishaji.

MAGONJWA & WADUDU
MAGONJWA

Vitunguu swaumu havishambuliwi sana na magonjo, ila magongwa yake ni kama:=

i) Fusari muozo-unasababishwa na ukungu katika majani au miziz na pia unaweza kudhibiti kwa kuchoma masalia ya mimea baada ya kuvuna

ii) Kutu ya majani-mmea unakua na vinundu vya ukngu vyenye rangi ya kahawia kama kutu katika majani tumia dawa ya ukungu kama fungaran nabayfidan na nordox ili kuzuia

iii) Kuoza kwa vitunguu-ukungu wa rangi ya blue ufunika vitunguu na usabibisha vitunguu kuoza na utokea gharan vuna kwa uangalifu ili kuepusha michubuko na hakikisha store ni safi

iv) Baka jani-vidonda vidogo hutokeza katika majani na badae vinakua vikubwa epuka kumwagilia maji mengi kupita kiasi na tumia mzunguko wa mazao

v) Muozo shingo-shingo kuonyesha dalili ya majimaji weka mbolea ya ntrogen kama CAN,UREA na mwagilia maji ya kutosha hasa vinapo elekea kuvunwa.

WADUDU

Wadudu kama chawa wekundu nondo na funza wanakata miche na mizizi tumia dawa ya karate,selecron,novthin,dursban hutumika kuuwa wadudu

UVUNAJI

Baada ya miezi 6-7 tokea kupanda ndio mda muafaka wa kuvuna vitunguu swaumu kwani vinakuwa vimekomaa na majani na mashina huonesha dalili ya kukauka, ndipo viache vitunguu shambani mpaka majani yanape kukauka kabisa ng’oa kwa mkono au jembe na pia kua muangalifu ili kuepusha kuchubua vitunguu. Kiasi cha tani 4 – 7 zinaweza kuvunwa katika heka moja.

SOKO

Soko lipo kwasababu Vitunguu Swaumu ni kiungo kinacho tumika na wengi, kwa bei ya shiling 3,000 – 3800 kwa kilo.
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
35,181

Ahsante kwa somo zuri la Kilimo katika kuunga juhudi ya nchi ya Viwanda.
 
Forum statistics

Threads
1,424,512

Messages
35,065,456

Members
537,998
Top Bottom