ahsante mkuu pale unapootesha hamna haja ya mbolea? na mbolea ya aina gani mkuu DAP, CAN, UREA,SA,..... kuna mdogo wangu huwa analima huko huwa anajitahidi sana ila anapata mazao kidogo
 
kiongozi hongera sana

Na pole kwa changamoto hizo kilimo ndivyo kilivyo,

KILIMO kinahitaji, 1. elimu sahihi ya hilo zao unalotaka kulima, 2. ulime kwa kutime soko,

Naomba nikusaidie kidogo hapo katika RED NILIPOBOLD huyo mdudu wakulima wanyemuita Kanitangaze, SI KANITANGAZE (Tuta Absoluta). Kanitangaze harisi (Tuta Absoluta) hashambulii vitunguu yeye anashambaulia mimea ya jamii ya Solanacea family, kama Nyanya, viazi mviringo, bilinganyi, hoho,mnavu etc

ISIPOKUWA HUYO MDUDU MUHARIBIFU WA VITUNGUU HASA VIKIWA VIMEHAMISHIWA SHAMBANI NI CUTWORM/CATEPILLER/AMERICAN BOLLWORM, YEYE HUKATA MAJANI YA KITUNGUU MPAKA SHINA-MDUDU HUYU KWA MENEO YA RUAHA MBUYUNI-IRINGA NI MAARUFU SANA KWA JINA LA NG'ONYO.

DAWA ULIYOTUMIA NI SAHIHI, MAANA HUYO NI KIWAVI (LARVA), NA HATA HUYO WA NYANYA NAYE ANAPOKUWA KATIKA HIYO STAGE YA KIWAVI (LARVA) WANAFANANA SANA NA HUYO LARVA WA KITUNGUU. NA DAWA HIYO ULIYOTUMIA YA BELT NI MOJA WAPO YA DAWA ZINAZOANGAMIZA HAO VIWAVI

SIKU NYINGINE UKIKOSA BELT, TAFUTA MOJAWAPO YA HIZI DAWA , MATCH, AU EVISECT, AU DURSBAN, AU FURADAN, KARATE 5EC, RAMDEX 5%EC, NINJA, NIMBECIDENE, PEGASUS AU PROVE 1.92 EC, METHOMEX, BLAST, AU DIMETHOATE, AU ATTAKAN ETC... ZIPO NYINGI


NAKUTAKIA MAFANIKIO

Habari zenu wadau.
Kama nilivyowaeleza hapo awali nita share experience ndogo niliyoipata katika kilimo cha kitunguu nilichoingia kufanya mwaka huu katika kijiji cha Igawa Mbalali.
Kwanza kabisa shamba langu lilikuwa na ukubwa wa 0.6 eka(Nililipima kwa kutumia GPS) hapa kitu nilichopata ni kwamba kwa ukubwa huu ambao kabla sijalipima niliambiwa ni eka moja, bahati mbaya nilipima wakati nimeshalilipia na kupanda tayari.
Katika shamba hili nilifanikiwa kukata vijaruba 202, na nilipanda mwezi wa saba mwanzoni na nimevuna mwezi huu wa 11 mwanzoni, gharama za kuendesha shamba hili ambapo kwangu ni kama shamba darasa ilifika 2.9m
Lesson learnt
1. Kitunguu ambacho wenyeji wanasadiki kuwa ni chenye faida mara nyingi ni kile kinacholimwa kuanzia mwezi wa 3 au 4 na kutolewa mwezi wa 6 au 7. Au kinacholimwa mwezi 7 au 8 na kutolewa wa 11 au 12 kwa ajili ya kuhifadhi kwenye Ghala.
2. Upandaji, kutokana na ugeni na kutofahamu mambo mengi, upandaji haukufuata utaratibu kwa baadhi ya jaluba na hivyo kubananisha vitunguu. Upandaji unaotakiwa ni ule maarufu wanasema upandaji wa umbali wa kiberiti.
3. Kitunguu nilichopanda mimi ni cha umwagiliaji, hapa napo kuna changamoto lukuki, ukimpata kijana mwaminifu gharama huwa chini kwani mara nyingi wanachakachua sana mafuta. Kijana aliyesimamia shamba langu alikuwa ni majanga tu.
4. Utunzaji wa shamba unahitaji ukaribu sana hasa kipindi chs kupiga dawa na kupiga mbolea. Usipoangalia utakuwa unanunulia wengine mbolea. Pia dawa, kwa kipindi ambacho nilipanda mimi huhitajika dawa nyingi kwa kuwa ni kipindi ambacho kunakuwa na wadudu wengi. Pia nilishambuliwa na wadudu wanaitwa kantangaze hawa wadudu kwa kweli ni balaa ila niliwatuliza kwa dawa moja inaitwa Belt.
5. Uvunaji, kwa kweli kama walivyochangia wadau wengine kipindi cha uvunaji hutakiwi kuingiza maji mengi kwenye jaluba, pia ukivuna omba mungu mvua isikukute maana vikinyeshewa na vikiwa vimesha katwa basi hapo ndio mwisho wa hadithi.
6. Uuzaji, ndugu zangu kama nilivyosema hapo juu kuhusu mvua, vitunguu vyangu vilinyeshewa, ila nashkuru ilikuwa bado havijakatwa ndio kwanza vimetoka kung'olewa. Hapo kwa kweli thamani ya kitunguu changu ilishuka, hata hivyo niliuza gunia kwa 50,000 na vile vilivyopasuka gunia 30,000. Ukweli ni kwamba kipindi hiki ambacho nimevuna vitunguu ni vingi sokoni, hivyo baadhi kipindi hiki vitunguu vyao huhifadhi gharani hadi Januari ambapo bei huwa juu kidogo na ya kuridhisha.
7. Mwisho ningependa kuwashirikisha wenzangu na kuwaambia ya kwamba vitunguu vina pesa ila ukilima kwa wakati sahihi, sehemu sahihi, kilimo na usimamizi sahihi.
Kwa kipindi hiki kitunguu kimenikata, sijapata faida ila kwa niliyojifunza katika awamu hii naamini ni silaha muhimu katika msimu ujao na lazima nifanikishe endapo Mungu akipenda nikawa hai, nitatoboa tu. Nitajitahidi mwezi wa tatu nitakuwa nishapanda Mungu akipenda.
Kwa wale wanaolima maeneo haya hasa kilimo cha umwagiliaji nasema nimeshakaribia tuendeleze mapambano.
Aluta kontinua, daima mbele nyuma mwiko.
davidson689@hotmail.com
 
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
mkuu nitakutafuta, hii jamii forum version mpya inazingua kuku pm siwezi
 
Beethoven. Mie pia nimeanza kulima vitunguu na nategemea kutoa awamu ya kwanza tar 5 July hivi. Nilitembelewa na wazungu flani shambani kwangu wakaniambia from August watanipa mtaalamu wao ambapo atakuwa ananielekeza namna bora ya kulima then nitapata soko la ku-export.

Kama walichosema wanamaanisha nadhani ntakuchek ili tuweze export at large scale. Mana nilikubaliana nao kupanda heka 10 kila mwezi ili kuwa na constant supply, as kwa sasa nina heka 80 ziko in irrigation scheme.

Je wewe unalima maeneo gani? Tweza kuchek kama vp tukapeana views zaidi mana nami nina info kidogo kuhusu SOKO.
aisee mkuu nitakucheki na nitakufanyia tour kwenye shamba lako, ushirikiano wako plz
 
Rafiki yangu, sisi watanzania tuna maajabu yetu kaka. Mimi nalima shamba kubwa kiasi lakini challenge kubwa inayonikabili ni nguvukazi kwa maana ya watu wa kufanya kazi. Wenyeji wa eneo lilipo shamba langu naweza kusema hawana moyo wa kazi, mtu anakuja kufanya kazi siku moja ukimlipa anaenda kutumia hela hadi iishe ndio anarudi kufanya kazi tena, inaweza kuchukua hadi wiki ndio mtu arudi tena. Katika hali kama hiyo nakuwa nashindwa kutimiza malengo yangu. Kwa mfano lengo langu kwa mwezi January ilikuwa nilime ekari 25 lakini niliambulia kulima ekari 11, watu hawafanyi kazi. Inanilazimu kwenda mikoani kama kanda ya ziwa na Dodoma kutafuta watu wa kuja kulima huku pwani, hao watu inabidi niwajengee kambi shambani na kuwasimamia kwelikweli ndio kazi iende, yaani kama wanafanya kwa kujitolea vile kumbe wanapata malipo. Kwahiyo ndugu yangu usishangae kuona wakenya wanaajiriwa hadi mashambani, sisi userious wa kazi ni mdogo na ni tatizo kubwa sana. Sometimes nakuwa nikifikiria sana nagundua hata wakoloni walipoamua kujenga miundo mbinu kama reli na barabara hawakuwa na jinsi bali kuwashikia fimbo na mijeledi mababu zetu, bila hivyo wabongo hatuendi ndugu yangu. Samahani kwa kutumia maneno yasiyo mazuri sana ila niko dissapointed mno na baadhi ya wananchi wenzangu. Tunajaribu kugawana hiki kidogo kwa kupeana viajira hivi vya mashambani lakini tunaangushana kwelikweli, jamani maofisini tunajaza raia wa kigeni (Experts),biashara zimeshikwa na wageni, sasa hata mashambani tuweke wageni???? Watanzania hebu tupende kazi bwana tunajiangusha wenyewe!
HAHAAAAA HII NDIO TANZANIA MKUU, ALAFU UTASIKIA WATU WANASHABIKIA MPAKA 2020 TUTAKUA UCHUMI WA KATI! ETI MAGUFULI ATAFANYA MAMBO.........DUH NCHI YANGU HII
 
wadau mimi mgeni ndani ya jamii hii nahitaji kupata taarifa za jinsi ya kuingia katka kilimo cha kitunguu kupata gharama zote kwa yule anaejua maeneo ya mbalali au pengne kwa mkoa wa mbeya kwani ndo maeneo niliyopo
 
kilimo kinalipa sana lakini ni bahati nasibu,nililima vitunguu,nyanya,tikiti,maharage na kufuga layers,mabadiliko ya tabia nchi, nyanya zikaharibiwa na mvua wiki la kwanza kuanza kuchuma,vitunguu hakuna uhakika wa kuvuna kwani huenda vikaenda na maji,vitakuwa tayari machi 20,tikiti zilioza baada ya mvua kujaza maji shamba,mahagwe ekari tatu yamekomaa,mvua inanyesha kupita kiasi-yataoza mengi,ekari mbili yanakaribia kukomaa pia. kuku wako wiki ya kumi;zaidi ya milioni saba zimetumika,hasara tupu but najipanga upya kulima ekari tatu za nyanya(nimeshamwaga mbegu na kukodisha shamba) name kufuka broilers 300(wanakuja next wiki) ili kukuza mtaji. ukiingia kwenye kilimo jipange,vinginevyo utakufa kwa pressure.
MKUUHASARA KAMA HIZI MTU HAWEZI KUZIKWEPA KWA KUPIGA HESABU MVUA ZITAANZA KUNYESHA BAADA YA MUDA GANI NA MAZAO YANGU YATAKUA YAMEFIKIA HATUA GANI ILI KAMA MVUA ZITAYAHARIBU USIPANDE UPANDE KATIKA MUDA AMBAO MVUA HAZITAYAKUTA BADO HAYAJAVUNWA? NA HAO KUKU LAYERS HASARA YAKE IMEKUJAJE MKUU HEBU TUFAFANULIE TUJIFUNZE TUJENGE NCHI TUACHE KUCHEKWA
 
Naomba lifunguliwe group la whatsapp, tujadili vizuri na kubadilishana mawazo kwa urahisi zaidi, wenye kujifanya ni ma-admin halafu kumbe matapeli haipendezi tunarudishana nyuma kimaendeleo na sio ungwana

Hilo group lishafunguliwa?
 
wadau mimi mgeni ndani ya jamii hii nahitaji kupata taarifa za jinsi ya kuingia katka kilimo cha kitunguu kupata gharama zote kwa yule anaejua maeneo ya mbalali au pengne kwa mkoa wa mbeya kwani ndo maeneo niliyopo

Huu uzi umeelezea mengi sana.
Ushauri: anza kupitia kuanzia page ya kwanza kabisa. Mpaka ukifika page ya mwisho utakuwa umejifunza mengi.
 
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.
hizo pump za kusuka zinapatikana wapi?
 
Hilo group lishafunguliwa?
Habari zenu wakuu! Huu uzi ni mzuri kwa wale wakulima wa kitunguu ningependekeza na kutilia mkazo kweli lingeundwa group humu la whatsapp kwa wale wadau ili tuwe na umoja wetu tukutane tupange na kueleweshana mikakati juu ya kilimo cha kitunguu naona itakuwa jambo jema kwa wale wageni kama mimi kupata uelewa mpana wa kilimo hichi
 
Tafadhali sana kabla ya kulima ni vizuri sana ukafanya marketi analysis, kujua ni wakati gani bei inakuwa nzuri.

Napia uwe makini na eneo ulilopo,kwa mfano kama morogoro wanaanza Kuivisha nyanya nyingi mwezi wa 4, na wewe uko na nyanya zako nyingi mwezi huo huo Iringa au mbeya utapata bei mbovu maana wanunuzi wengi watavamia Morogoro mpaka ziiishe ndio watakuja hiyo mikoa mingine, mtu hawezi acha nyanya morogoro akaenda mbeya.

KATIKA KITUNGUU si kila wakati kitunguu kinakuwa na bei nzuri hizo tsh 100,000+ , miezi ya kuingiza kitunguu sokoni ni November (70,000tsh) to June 170,000+), baada ya hapo vingi vinaaza kutoka mabondeni, na mashamba ya mpunga, bei huporomoka sana
 
Tafadhali sana kabla ya kulima ni vizuri sana ukafanya marketi analysis, kujua ni wakati gani bei inakuwa nzuri.Napia uwe makini na eneo ulilopo,kwa mfano kama morogoro wanaanza Kuivisha nyanya nyingi mwezi wa 4, na wewe uko na nyanya zako nyingi mwezi huo huo Iringa au mbeya utapata bei mbovu maana wanunuzi wengi watavamia Morogoro mpaka ziiishe ndio watakuja hiyo mikoa mingine, mtu hawezi acha nyanya morogoro akaenda mbeya. KATIKA KITUNGUU si kila wakati kitunguu kinakuwa na bei nzuri hizo tsh 100,000+ , miezi ya kuingiza kitunguu sokoni ni November (70,000tsh) to June 170,000+), baada ya hapo vingi vinaaza kutoka mabondeni, na mashamba ya mpunga, bei huporomoka sana
Nashukuru sana ndg kwa msaada wako.
 
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
Naomba ruhusa yako mkuu nikutafute
 
Wadau mim ni mkuwa wa vitunguu ila sijawahi kulima kipindi cha masika nataka nijaribu kipindi hiki nalimia mkoani dodoma naomba mwenye experience wa kulima kipindi hiki anipe ushauri nini changamoto risk ikoje na namna ya anavyokabiliana nayo
Ulikijaribu kitunguu cha masika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom