SoC02 Kilimo cha Pilipili Kichaa (Dhahabu nyekundu) kinavyonipa pesa bila kutarajia

Stories of Change - 2022 Competition

the_diplomat

Member
Sep 1, 2022
81
73
Baada ya kuhitimu Shahada ya Sanaa (BA)2011 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), nilitafuta kazi bila mafanikio. Nikaona nisome Stashahada ya Uzamili katika Elimu nikamaliza 2014 ili nipate ajira ya ualimu, sikufanikiwa kuipata. Mwaka 2016 nikaanza kusoma Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tazania nikiwa na malengo ya kujiaandaa kuwa mwanasheria wa kujitegemea na kuhitimu 2020.

Nikiwa natafakari jinsi yakupata pesa kwenda Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) mwaka, nikasikia watu wanaongelea habari ya kilimo cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Nikaona nitafute habari kamili ya kilimo hiki.

Nikatafuta tovuti mbalimbali na kwenye mitandao ya kijamii hususani Facebook nikaona kuna wakulima wengi ambao wanatoa ushuhuda wa kilimo hiki cha pilipili kichaa (DHAHABU NYEKUNDU). Lakini pia nikaona nchi kama Kenya na Uganda ni nchi ambazo pilipili kichaa hulimwa kwa wingi. Pia nikatafuta taarifa za masoko, nikaona masoko yake makuu ni nchi za bara la Asia na Ulaya. Hii ilinipa ‘moto mkuu’ usiozimika kuingia shambani na kuanza kazi ya kuandaa shamba.

Nikiwa na Kiasi cha 1,900,000/- ikiwa ndio akiba pekee. Sikujali nikaamua ‘ku-take risk’. Nikaamua kwenda inapolimwa pilipili Mkoa wa Kigoma , Uvinza na kuweka kambi ya kazi. Niliandaa shamba la ekari 2, gharama ya kukodi shamba 50,000/ ekari kwa mwaka.​

KAMBI YA KAZI.PNG


MAANDALIZI YA MBEGU

Nilitafuta mbegu aina ya African Bird’s Eye Chilli (ABE), hii ni aina ya mbegu ya pilipili yenye matunda kama macho ya ndege pori wengi wanaopatika Afrika. Aina hii ya pilipili huzaa sana na hususani ikipata maji ya kutosha. Nilichukua gramu 100 kwa 100,000/-, kwani hutosha la ekari 2 , kila ekari huchukua mimea 4500 hadi 5000.
MBEGU.PNG


MAANDALIZI YA VITALU
Nilitafuta maeneo yaliyo karibu na mto nikaandaa maeoneo ya vitalu 3 kwa ajili ya kusia mbegu. Niliweka mbolea ya samadi ya kutosha kiasi cha debe 3 kwa kila kitalu kulingana na ukubwa wa kitalu, nikaweka majani makavu kuhifadhi unyevu kwenye udongo (kama vinavyoonekana kwenye picha). Huchukua muda wa wiki 3 mbegu zote kuwa zimeota vizuri, katika picha kuna miche mikubwa ambayo niliitolea kivuli na midogo ambayo bado ilihitaji kivuli kwakuwa ilichelewa kuota, ingawa ilipandwa pamoja.
KITALU.PNG


KITALU 2.PNG



UPANDIKIZAJI WA MICHE
Shamba lililimwa kwa jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) ili kulainisha shamba. Baadaye nilitafuta vijana 3 niliingia nao makubaliano kunitengezea matuta shambani, shughuli za kutengeneza matuta kama vile kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kupandikiza miche kwa TZS 600,000/-. Kita tuta lilikuwa na mita 3.5, na kuchimba mashimo kwenye kila tuta, umbali wa sentimita 90 shimo hadi shimo, mita 1 msitari hadi msitari, na kila shimo liliwekewa mbolea ya samadi kilo 1 na hapa nilitumia vikombe viwili vya nusu lita.

KITALU3.PNG


Upandikizaji wa mimea hufanyika siku 45 tangu mbegu kuwekwa kitaluni. Kwa kipindi cha siku hizo mimea huwa na uwezo wa kustahimili hali ya ukame kidogo hata kama mvua isiponyesha wiki moja bado unauwezo wa kuendelea na uhai wake.
KITALU 4.PNG


UTUNZAJI NA UKUAJI WA MICHE/MIMEA YA PILIPILI SHAMBANI
1. Mbolea:

Niliweka mbolea ya Samadi ya kutosha kuanzia kitaluni hadi shambani. Mbolea ya Samadi sikununua kwa kuwa wafugaji ni wengimaeneo haya, niliwaomba nao wakanipatia bure, gharama ilikuwa ni kwenye kusomba mbolea hiyo. Nilitumia mkokoteni wa kukokotwa na ng’ombe, mbapo ilinigharimu 140,000/- kusomba mbolea ya kutosha shamba zima la ekari 2.​

KWAMA 22.PNG


Pia nilitafuta lita mbili za mbolea ya Organic inayotoka kampuni ya MOKUSAKU inayoitwa MOKUSAKU Cal-Phos na NPK PLUS kwa kuongeza virutubisho kwenye mimea na kuhifadhi maua yasidondoke. Kila lita ni 30,000/- hivyo kwa lita 4 ilinigharimu 120,000/-​

MOKUSAKU BN.PNG


PILIPILI MOKU.PNG


2. Palizi
Palizi ya kwanza ni baada ya wiki ya 3 mimea ikiwa shambani. Niliendelea kupalilia magugu yanapoota. Palizi lilinigharimu kiasi cha 200,000 mpaka mimea ilipokuwa na matawi na majani mengi na kuzuia magugu kuota kwa wingi.
MIMEA SHAMBA.PNG

pilipili new.PNG


CHANGAMOTO ZA UKUAJI WA MICHE YA PILIPILI
1. Magonjwa

Pilipili hukabiliwa na ugonjwa wa ukungu, usipodhibiti mapema majani hujikunja (kama inavyoonekana katika picha za mimes aliyaanza kuugua) na mmea kupukutisha majani yote. Nilitumia dawa ya Innovex 360 SC kudhibiti ugonjwa huu, gharama 80,000/-
UKUNGU.PNG

2. Mchwa na Panzi
Mchwa wanakata mashina chini kwenye udongo na panzi wanakula majani sana. Nilitumia dawa ya NINJA kuzuia panzi , na TERMITE KILLER kwa ajili ya mchwa , gharama 50,000/-.

UVUNAJI NA UKAUSHAJI

Kuanza kuweka mimea shambani mpaka kuanza kuvuna ni miezi 3, ongeza siku 45 za miche kitaluni. Uvunaji hufanyika kwa kuchuma pilipili iliyoiva na nyekundu kama nyanya. Uvunaji huwa ni kazi kwelikweli, ndoo ndogo ya lita kumi (ambayo ni 3.5-4 kg za pilipili) huvunwa kwa 3000/- hadi 3500/- (hapa ndipo gharama kubwa huitajika na ndio ilitumia kiasi kilichobakia). Na pilipili iliyoiva hutoka kwenye kikonyo chake kwa haraka. Pilipili iliyovunwa huwekwa juani kwa muda wa siku 3 baada ya hapo inakuwa imekauka, itunze ndani sehemu kavu yenye hewa na mwanga . Jambo la kupendeza katika katika MGODI HUU WA DHAHABU NYEKUNDU ni kwamba pilipili iliyo tayari inaingia sokoni na hivyo kukusaidia kupata pesa ya kuendesha uvunaji, hiki ndio kitu cha pekee katika zao hili. Nimeanza kuvuna Mei mpaka sasa naendelea kuvuna, uvunaji natarajia kuisha Septemba
stiveppp.PNG
kausha 2.PNG


KUCHAMBUA
Kabla ya kuuza pilipili uichambue iwe safi, usiweke iliyoharibika . Zitenge hizo zilizoharibika usizitupe nazo zinauzika pia.


chambua 2.PNG


UUZAJI
Masoko ya Pilipili kichaa yapo na unatakiwa kuwa makini na madalali wa pilipili, wengi wao ni matapeli. Mimi nawauzia kampuni ya TAZAMA ambayo inachukua mzigo na kupeleka Kenya, hii kampuni ni ya uhakika na wanatoa pesa yote kwa mkulima.​
MAUZO.PNG

Na uuzaji hufanyika kila baada ya wiki mbili. Hata sasa ninavyomalizia kuandika Habari(Story) TAZAMA wamenitumia pesa ya awali kwa mzigo ulisafiri wiki hii.​
muamala.PNG


FAIDA
Faida ya zao hili, kuna mimea 9400 shambani. Nilijiwekea mmea mmoja utoe robo kilo, naelekea kuvuka malengo ya robo kilo kwa mmea, kuna mimea inatoa mpaka robo tatu ya kilo 3/4 . Na kila kilo bei yake ni TZS. 5000/- Lakini pia zile zilizoharibika bei yake ni TZS 1000/ kwa kilo moja. Na zao hili nitaendelea kuvuna kwa miaka mingine mitatu. MUNGU NI MWEMA, SANA KARIBU MGODINI​
 

Attachments

  • ukaushaji.PNG
    ukaushaji.PNG
    129.6 KB · Views: 140
Hongera sana

Nakumbuka niliwahiw kukutana na baba mmoja akanipa habari juu ya kilimo cha pilipili na kuingia mkataba na JWTZ,

Ilikuwa juu juu na niliandika namba nikasahau kusave.

Kama Kuna yoyote mwenye details ya aina hiyo ya kilimo cha pilipili kushirikiana na jeshi, naomba tuzipate Tafadhali.
 
Hongera sana

Nakumbuka niliwahiw kukutana na baba mmoja akanipa habari juu ya kilimo cha pilipili na kuingia mkataba na JWTZ,

Ilikuwa juu juu na niliandika namba nikasahau kusave.

Kama Kuna yoyote mwenye details ya aina hiyo ya kilimo cha pilipili kushirikiana na jeshi, naomba tuzipate Tafadhali.

Anza na huyu jamaa, utapata manufaa zaidi. Bora Kenda Mkononi kuliko kumi nenda rudi.
 
Kasema kila mti unatowa robo kilo. Hiyo robo tatu ni baadhi tu ndiyo inatowa.
Hesabu ya kufanyiwa kazi iwe 9400x0.25x5000=11,750,000.
Uweke na gharama za wasaidizi wa kazi. Ila hata akibakisha 5m bado si mbaya kama maelezo yake mengine ni sahihi.
Elewa kiswahili amesema
-alijiwekea malengo ya robo kilo kwa kila mmea ila amevuka lengo kuna mimea inatoa hadi 3/4kg kwa kila mmea na atavuna kwa miaka mitatu mingine mbele..)....sasa sahau kuhusu miaka mitatu mingine mimi nime- approximate kwa huu mwaka mmoja at the pick level....🤓🤓🤓
 
Hizi ni zile Spining za wakina JATU ,ukiona kitu kinahanasihwa sana kilimwe ogopa sana, ni zile mambo za Vanila. Kwenye pililipi kuna uhuni mkubwa sana wanacho fanya jamaa wanauza mbegu ndio biashara zaoa kubwa, ila kwamba ina soko sijui nchi gani ni uongo mkubwa sana.ni zile mambo za sungura
 
Hizi ni zile Spining za wakina JATU ,ukiona kitu kinahanasihwa sana kilimwe ogopa sana, ni zile mambo za Vanila. Kwenye pililipi kuna uhuni mkubwa sana wanacho fanya jamaa wanauza mbegu ndio biashara zaoa kubwa, ila kwamba ina soko sijui nchi gani ni uongo mkubwa sana.ni zile mambo za sungura
Tusiwe too negative Mpwa, tumshukuru kwa hili then the rest yabakie ya mtu binafsi
 
Back
Top Bottom