GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Ni mwaka Jana ndiyo nilifahamu kwa mara ya kwanza juu ya uwepo wa tunda liitwalo dragon.
Dragon ni kama jina la "utani"
Jina lake halisi, kama sikosei, ni PITAYA au MSHOKISHOKI.
Uchunguzi wangu nilioufanya umenibainisha kuwa zao hili lingali lina soko sana hapa Tanzania na hata Afrika Mashariki kwa ujumla
Nimejiridhisha kuwa ni uwekezaji sahihi kuufanya.
Naomba wadau wenye kufahamu zaidi wanijuze:
1. Ekari moja itahitaji miche mingapi?
2. Ikiwa nitaamua kununua miche kidogo kidogo, labda miche minne kila mwezi, itanichukua muda gani kukamilisha ekari moja?
3. Kuna ulazima wa kuwa na miundombinu ya umwagiliaji kwenye shamba husika?
4. Ni mambo gani ya kuzingatia sana unapoamua kufanya kilimo husika?
Ni hayo tu!
Asante🙏🙏🙏