OGOPASANA
JF-Expert Member
- Apr 30, 2009
- 262
- 144
Nawashauri mjifunze elimu mbalimbali za ujasiliamali za usindikaji na utengenezaji wa bidhaa kutokana na kilimo hicho kisha muandae mchanganuo mzuri wa investment hiyo then mnaweza kwenda bank kuombea mkopo mradi huo na kuanzisha kiwanda chenu kidogo cha kutengeneza bidhaa mbalimbali kuokana na kilimo hicho kama wanavyofanya hao mnaowauzia, then kwa upande mwingine ningewashauri mtafute kijiofisi maeneo ya mjini kisha muwaajiri watu waliobobea katika taaluma ya masoko ili kuwatafutia masoko ya bidhaa zenu kutokana na kilimo hicho, mfano mnaweza kuuza katika migahawa, mahoteli, majumbani, supermarkets na kusafirisha mikoani na nchi za jirani endapo mtajipanga kiofisi zaidi kama kampuni. Mwisho nawashauri vijana hasa mliomaliza chuo na mliosomea taaluma za masoko na ICT muweze kuwasaidia wakulima wetu hapa nchini ambao hawana elimu ya kutosha kuhusu kutafuta na kumudu masoko ya mazao yanayotokana na kilimo chao kwa kuandaa semina za kuwaelimisha, kufanya biashara ya kuwatafutia masoko wakulima kama wanavyofanya madalali wa bidhaa nyingine kama magari, nyumba , viwanja nk.
Nawasilisha.
Nawasilisha.