Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

mkuu safi sana, mimi huwa nayapanda kienyeji sehemu yoyote ambayo ina nafasi shambani huwa nayachanganya na mazao mengine kama mahindi, maharage, matikiti etc kwahiyo sielewi nalima hekari ngapi za mananasi na matikiti lakini mwishoni huwa naingiza fedha nzuri sana

Mimi mkulima pia. Katika hiyo 14,000 bado kunabaki nafasi na nimepanda Kunde kwa ajili ya Nitrogenization ya udongo.
 
Wakuu naomba kujua wapi ninaweza kupata mbegu ya minanasi, nina kajieneo mahali sina plan nako kwa mwaka huu hadi mwishoni mwa mwaka kesho. sasa sitaki kukaacha kakae bure ni wapi ninaweza kupata kama miche 40,000 au zaidi na kwa bei nafuu?

Jone Mwalwisi
budget yako ni bei gani kwa mche? je shamba lako liko wapi? nina uwezo wa kukupatia mbegu hadi 100,000 ukitaka
 
Mimi mkulima pia. Katika hiyo 14,000 bado kunabaki nafasi na nimepanda Kunde kwa ajili ya Nitrogenization ya udongo.

kumbe tupo wengi, hii njia inalipa sana mimi nimepanda mazao kama 8 hivi humo ndani kuna mbaazi, kunde(zikiwa mbichi ni fedha nzuri sana), karanga, ulezi na mtama kiasi. Somo la kilimo limenisaidia sana japo kipindi nalisoma nililiona kama kero kubwa kwangu
 
Wakuu,

Nawasalimu nyote.

Tunahitaji ‘mbegu' (suckers au slips) kama elfu arobaini (40,000) hivi za mananasi aina ya ‘mpingo' kwa ajili ya kupanda ndani ya miezi miwili kuanzia sasa (18 April 2012 katika shamba lililopo kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Temeke (DSM).

Ubora: Mbegu ninazohitaji ni yale machipukizi yanayotokea chini mche wa nanani (‘suckers') au yale machipukizi ya pembeni chini ya tunda (‘slips') na sio ile sehemu ya tunda ya juu (crown) inayoachwa baada ya tunda kuliwa. ‘Suckers' ni bora zaidi kuliko ‘slips' na hata bei itazingatia tofauti hiyo na pia ukubwa wa mbegu yenyewe (ikiwa kubwa ni bora zaidi).

Mahali: Shamba lipo kilomita 5 kutokea kijiji cha Mwasonga wilaya ya Temeke (Dar). Kijiji cha mwasonga kipo kama kilometa kama 34 kutokea ferry (kigamboni) ama kama ni kupitia njia ya mbagala ni kama kilometa 50 hivi au kwa wale wanaopafahamu Kibada, ni kilometa 25 kutoka hapo. Barabara kutokea Kibada ni changarawe na kwa ujumla ni nzuri – all weather (sehemu kubwa ya barabara unaweza kuendesha mpaka speed 80-90km/h kwa gari dogo). Gari linafika mpaka shambani.

Bei: Kutegemeana na ubora, nipo tayari kununua kwa mpaka shilingi 130 (haipungui sh 120) kwa mbegu kama ikifikishwa mpaka shambani au mpaka shilingi 120 (haipungui sh 100) kama ikifikishwa kijiji cha Mwasonga. Nipo tayari kununua mpaka kwa shilingi 60 (range 0-60) kwa mbegu kama nikiifuata mwenyewe katika sehemu ambayo inafikika kwa gari ya mizigo lakini eneo lenyewe liwe ni hapa Dar au kama ni nje basi lisilozidi kilometa 150 kutokea hapa Dar na mzigo uwe mkubwa unaoweza kufikia angalau tani mbili (roughly kama mbegu 5,000). Kama ni nje ya umbali huu, muuzaji mwenyewe itabidi afanye utaratibu wa kufikisha mzigo mpaka katika kituo ambacho kitakuwa ndani ya umbali/maeneo niliyotaja.

Uhakiki: Tunafahamu kuwa kama mbegu ni nyingi, inaweza kuwa ngumu kuhesabu mojamoja, hivyo katika hali kama hiyo tunaweza kukubaliana utaratibu rahisi zaidi wa kuhesabu (mf: kupima kwenye magunia au viroba na kutumia wastani wa mbegu zinazojaza gunia au kiroba husika). Tunaweza pia kutumia uzito katika kufikia idadi ya mbegu hizo. Kwa wastani, mbegu ya nanasi (suckers au slips) zina uzito wa gramu 350 mpaka 450 (i.e. pungufu kidogo ya nusu kilo).

Zingatia:

  • Hakuna malipo ya kabla (advance payment).
  • Kwa watakaotaka kuleta shambani, ukifikisha mzigo na kuhakikiwa unalipwa pesa yako (cash basis). Au kama tunakuja kuuchukua wenyewe mahali ulipo, tutalipa kabla hatujachuka mzigo wako (mara baada ya kuuhakiki).
  • Kabla ya kuanza safari ya kuleta mzigo katika maeneo niliyotaja, tafadhali tuwasiliane na kukubaliana muda/siku kwanza.
  • Hatutahusika na gharama zozote zitakazotokana na makosa ya muuzaji kuhusu vigezo na masharti tuliyoyataja hapo juu (aina ya mbegu, ubora, bei, mahali).

Zaidi ya nanasi, tunahitaji pia:

  • Mbolea (ya kinyesi cha ngombe) – lorry la tani 7 likijaa ni shilingi 150,000 (laki mbili) mpaka shambani.
  • Mbegu (miche) ya migomba (aina: Mtwike, Kiguruwe, Mzuzu, mkono wa tembo, Pukusa etc), kila mche tunanunua kwa shilingi 700 - 800 (ukifikishwa Mwasonga) au shilingi 900 -1,000 (ikifkishwa shambani). Kama mzigo ukifikishwa Mwasonga tunanunua kuanzia mzigo wa si chini ya mbegu/ miche 150 na kuendelea. Tunahitaji miche karibu 1,000.

Kwa yoyote ambaye angependa na anao uwezo wa ku-supply mbegu hizo na/au mbolea katika ubora, mahali na bei nilizotajata fadhali tuwasiliane kwa namba hii: +255-78-4308682. Kama unahitaji maelezo ya ziada kuhusu suala hili usisite kutuuliza.

Karibuni, biashara ni maelewano. Tupo tayari kupokea ushauri wenu pia.
 
Wakuu,

Nawasalimu nyote.

Tunahitaji ‘mbegu' (suckers au slips) kama elfu arobaini (40,000) hivi za mananasi aina ya ‘mpingo' kwa ajili ya kupanda ndani ya miezi miwili kuanzia sasa (18 April 2012) katika shamba lililopo kata ya Pembamnazi, Manispaa ya Temeke (DSM).

Ubora: Mbegu ninazohitaji ni yale machipukizi yanayotokea chini mche wa nanani (‘suckers') au yale machipukizi ya pembeni chini ya tunda (‘slips') na sio ile sehemu ya tunda ya juu (crown) inayoachwa baada ya tunda kuliwa. ‘Suckers' ni bora zaidi kuliko ‘slips' na hata bei itazingatia tofauti hiyo na pia ukubwa wa mbegu yenyewe (ikiwa kubwa ni bora zaidi).

Mahali: Shamba lipo kilomita 5 kutokea kijiji cha Mwasonga wilaya ya Temeke (Dar). Kijiji cha mwasonga kipo kama kilometa kama 34 kutokea ferry (kigamboni) ama kama ni kupitia njia ya mbagala ni kama kilometa 50 hivi au kwa wale wanaopafahamu Kibada, ni kilometa 25 kutoka hapo. Barabara kutokea Kibada ni changarawe na kwa ujumla ni nzuri – all weather (sehemu kubwa ya barabara unaweza kuendesha mpaka speed 80-90km/h kwa gari dogo). Gari linafika mpaka shambani.

Bei: Kutegemeana na ubora, tupo tayari kununua kwa mpaka shilingi 130 (haipungui sh 120) kwa mbegu kama ikifikishwa mpaka shambani au mpaka shilingi 120 (haipungui sh 100) kama ikifikishwa kijiji cha Mwasonga. Aidha, tupo tayari kununua mpaka kwa shilingi 60 (range 0-60) kwa mbegu kama tukiifuata wenyewe katika sehemu ambayo inafikika kwa gari ya mizigo lakini eneo lenyewe liwe ni hapa Dar au kama ni nje basi lisilozidi kilometa 150 kutokea hapa Dar na mzigo uwe mkubwa unaoweza kufikia angalau tani mbili (roughly kama mbegu 5,000). Kama ni nje ya umbali huu, muuzaji mwenyewe itabidi afanye utaratibu wa kufikisha mzigo mpaka katika kituo ambacho kitakuwa ndani ya umbali/maeneo niliyotaja.

Uhakiki: Tunafahamu kuwa kama mbegu ni nyingi, inaweza kuwa ngumu kuhesabu mojamoja, hivyo katika hali kama hiyo tunaweza kukubaliana utaratibu rahisi zaidi wa kuhesabu (mf: kupima kwenye magunia au viroba na kutumia wastani wa mbegu zinazojaza gunia au kiroba husika). Tunaweza pia kutumia uzito katika kufikia idadi ya mbegu hizo. Kwa wastani, mbegu ya nanasi (suckers au slips) zina uzito wa gramu 350 mpaka 450 (i.e. pungufu kidogo ya nusu kilo).

Zingatia:

  • Hakuna malipo ya kabla (advance payment).
  • Kwa watakaotaka kuleta shambani, ukifikisha mzigo na kuhakikiwa unalipwa pesa yako (cash basis). Au kama tunakuja kuuchukua wenyewe mahali ulipo, tutalipa kabla hatujachuka mzigo wako (mara baada ya kuuhakiki).
  • Kabla ya kuanza safari ya kuleta mzigo katika maeneo niliyotaja, tafadhali tuwasiliane na kukubaliana muda/siku kwanza.
  • Hatutahusika na gharama zozote zitakazotokana na makosa ya muuzaji kuhusu vigezo na masharti tuliyoyataja hapo juu (aina ya mbegu, ubora, bei, mahali).

Zaidi ya nanasi, tunahitaji pia:

  • Mbolea (ya kinyesi cha ngombe) – lorry la tani 7 likijaa ni shilingi 150,000 (laki moja na nusu) mpaka shambani.
  • Mbegu (miche) ya migomba (aina: Mtwike, Kiguruwe, Mzuzu, mkono wa tembo, Pukusa etc), kila mche tunanunua kwa shilingi 700 - 800 (ukifikishwa Mwasonga) au shilingi 900 -1,000 (ikifkishwa shambani). Kama mzigo ukifikishwa Mwasonga tunanunua kuanzia mzigo wa si chini ya mbegu/ miche 150 na kuendelea. Tunahitaji miche karibu 1,000.

Kwa yoyote ambaye angependa na anao uwezo wa ku-supply mbegu hizo na/au mbolea katika ubora, mahali na bei nilizotajata fadhali tuwasiliane kwa namba hii: +255-78-4308682. Kama unahitaji maelezo ya ziada kuhusu suala hili usisite kutuuliza.

Karibuni, biashara ni maelewano. Tupo tayari kupokea ushauri wenu pia.
 
Mkuu Safari_ni_Safari,

Safi sana mimi nimepanda ufuta unasaidia kuongeza Nitrogen pia kupunguza kuota majani pia kusaidia kuweka kivuli kwaajili ya kuzuia jua kali kipindi cha kiangazi na wanayama waaribifu.

Mimi mkulima pia. Katika hiyo 14,000 bado kunabaki nafasi na nimepanda Kunde kwa ajili ya Nitrogenization ya udongo.
 
Inafurahisha kumbe tuko wengi.....

kumbe tupo wengi, hii njia inalipa sana mimi nimepanda mazao kama 8 hivi humo ndani kuna mbaazi, kunde(zikiwa mbichi ni fedha nzuri sana), karanga, ulezi na mtama kiasi. Somo la kilimo limenisaidia sana japo kipindi nalisoma nililiona kama kero kubwa kwangu
 
Mkuu King Kong.

Sehemu ziko nyingi inategemea unapenda maeneo yapi kuanzia Mkoa wa Pwani,Tanga na Morogoro ni maeneo yanayostawi nanasi.Mkoa wa Tanga maeneo ya Korogwe mailikumi,Segera,Kwedizinga,Kabuku,Kwamkonga,Kwamkono,Mkata ukizama kijijini unapata ardhi kwa bei poa bila chenga.Ni PM kwa maelezo zaidi.

Wapi ninaweza pata hekari kama 20 hiv za kilimo? Za bei rahisi plz.
 
Hivi hakuna njia nzuri za kupreserve mananasi? maana msimu wa mananasi yanakuwa mengi sana then yanakata kama kuna njia ya kuyapreserve itasaidia sana kuuza kwa bei nzuri wakati yamekata
 
Hivi hakuna njia nzuri za kupreserve mananasi? maana msimu wa mananasi yanakuwa mengi sana then yanakata kama kuna njia ya kuyapreserve itasaidia sana kuuza kwa bei nzuri wakati yamekata

unatakiwa kuyapanda kwa awamu ili uvune kwa awamu. Mfano ktk shamba la hekari 20 unapanda kwa plots eg hk 5 janu, march, june, sept etc.
Note: Irrigation system iwepo
 
unatakiwa kuyapanda kwa awamu ili uvune kwa awamu. Mfano ktk shamba la hekari 20 unapanda kwa plots eg hk 5 janu, march, june, sept etc.
Note: Irrigation system iwepo

Kaka "Kada" nilitekwa kidogo na jukwaa la siasa nikapasahau huku nyumbani nilikuwa namiss vitu muhimu sana
Hivi kwa mwaka Nanasi zinazaa mara ngapi? ni mara moja tu au? I think suala la kupanda kwa awamu ni muhimu sana shida ni kuwa hatuna irrigation systems tunategemea maji ya sir God ukiweza kutime na kuvuna kipindi ambacho nanasi hakuna utapiga hela sana
 
Mkuu King Kong.

Sehemu ziko nyingi inategemea unapenda maeneo yapi kuanzia Mkoa wa Pwani,Tanga na Morogoro ni maeneo yanayostawi nanasi.Mkoa wa Tanga maeneo ya Korogwe mailikumi,Segera,Kwedizinga,Kabuku,Kwamkonga,Kwamkono,Mkata ukizama kijijini unapata ardhi kwa bei poa bila chenga.Ni PM kwa maelezo zaidi.

Nimenunua ekari 300 hapo Kabuku kwa 35,000 kwa eka. Shamba NI zuri sana japo sijaamua nilime nini kwa sasa. Kwa wakati huu nakata miti na kuchoma mkaa. Shamba linajiendesha lenyewe!
 
Hata mimi niko Kabuku karibu na kambi ya JKT Mgambo.

Nimenunua ekari 300 hapo Kabuku kwa 35,000 kwa eka. Shamba NI zuri sana japo sijaamua nilime nini kwa sasa. Kwa wakati huu nakata miti na kuchoma mkaa. Shamba linajiendesha lenyewe!
 
Ndugu wana JF,Binafsi
Nina shamba lenye ukubwa wa ekari 30 zilizopandwananasi hivi sasa, ambalo lina uwezo wa kuuza hadi tani 200 za mananasi kilamwaka. Nia yangu ni kupanua mradi huu mpaka ekari 100 ambazo zitakua na uwezowa kuzalisha hadi tani 700 kwa mwaka.Tuko kikundi cha watu nane na wote wanamalengo kama ya haya. Tuna mkakati wa kushirikiana na wakulima wengine ilituweze kuwa na uzalishaji mkubwa na wa kitaalamu endapo tuu, tutakuwa nauhakika wa soko la kudumu na la uhakika. Hivi sasa soko ni la msimu na sio la kuaminika hasaunapokua na volume kubwa, Mashamba yetu yapo huko Rufiji.Tunaomba mwenye mawazo kuhusu upatikanaji wa soko atujulishe.

Mkuu Hongeleni sana Kwa kilimo Kwanza,

Mkuu mimi nianze kwa kuwalaumi nyie/wewe kwa kuingia shambani kulima bila kujua utamzia nani, hili ndo Tatizo la wakulima wengi sana Tanzania, tunasukumwa kulima kitufulani na bei na sio soko, Bei ya Nyanya ikiwa juu kila mtu anataka alime bila kujalisha atamzia nani,

Matokeo ya kulima bila kujua utamzuia nani ndo haya ya madalali kuneemeka na product zako, na tumeshindwa kupiga hatua kwa sababu hizi za kulima kwa kusikia kwa wenzetu,

Mkuu ni lazima mbadilike, make wakati wa sasa sio wa miaka ya 90, kilimo ni biashara kama ilivyo biashara nyingine so ni lazima kabla ya kulima ujiridhishe kwamba umepata soko la uhakika la mazao yako, ni lazima ufanye Tafiti kwanza, ni lazima uje ni nani atakuwa consumer wako na kwa nini,

Tunaingia kilima na kuguga bila kwanza kufanya tafiti za masoko matokeo yake ni either mazo kuozea shambani, au mfugaji kuishia kumwaga maziwa chini, Na hata hayo mananasi it means usipo pata soko yataozea shambani au utakuja kuuza kwa hasara, na hapo utaanza kuilaumu serikali hijatafuta soko la mananasi,

Mkuu hakikisha mnafanya tafiti za kutosha za

1, Nani atanunua mazao yenu

2. Kwa kiwango gani atanunua

3. Kwa bei gani atanunua

4. Kwa mashariti yapi,

Inakuwa inashangaza hata wafugaji mtu akisha fuga kuku na kutaga mayai ndo anaanza kutafuta soko lakini wakati hajaanza kufuga hakutafuta soko,

NA MWISHO KAMA MNAONA SOKO LA MOJA KWA MOJA NI TATIZO BASI MNAWEZA NYIE WENYEWE KUONGEZEA THAMANI HAYO MANANASI YENU NA KUUZA EITHER JUICE YAKE AU HATA KUYAKAUSHA NA KUYAPAKI KWENYE PAKITI
 
Back
Top Bottom