Kilimo bora cha Mananasi: Uandaaji wa shamba, upandaji, utunzaji wa mimea na uvunaji wa mananasi

Ntemi Kazwile

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
2,160
1,225
Vipi mbuzi ulishapata mkuu?

Tuje kwenye nanasi, kama uko serious, nenda regional block Kibaha idara ya kilimo,pale watakupa kila kitu sawa na eneo ulilopata shamba kwa ukanda huu wa Dsm/Pwani. Kama hutajali nenda Kiwangwa bagamoyo ukajifunze kwa vitendo kwa wakulima, watakwambia faida ya mbegu za kisasa na faida ya mbegu za kienyeji kwa vitendo,naamu pia wakati na udongo gani unafaa.

Mbegu za nanasi ziko barabarani nyingi tu zinauzwa, ila kabla hujanunua fika Kibaha kwanza. Ukame unapunguza mavuno na kama unaweza nenda pale Mwenge njia ya Coca cola, kuna kituo cha serikali kwa ajili ya miche ya minazi/embe uliza kituo cha minazi. Pale kuna watalaamu kibao.

Mkuu kazi njema.
Nashukuru sana mkuu
 
Kifuniko

Kifuniko

Member
99
0
Wana JF nawapa heshima kwa kutoa ushauri na kupean mawazo mbalimbali, mimi nipo Geita Mwanza na nina shamba hekta 5 ninataka kuandika mchnganuo wa kuanzisha kilimo cha kisasa cha mananasi. Malengo ni kufikia hekta 100 in future lakini hizi ni kwa kuanzia. Naomba ushauri namna ya kuandika mchanganuo ili hata nikitafuta soko la bidhaa kwenye kampuni za juice na nyinginezo unisaidie kuwasilisha.
 
M

mwalwisi

Member
45
0
Wakuu naomba kujua wapi ninaweza kupata mbegu ya minanasi, nina kajieneo mahali sina plan nako kwa mwaka huu hadi mwishoni mwa mwaka kesho. sasa sitaki kukaacha kakae bure ni wapi ninaweza kupata kama miche 40,000 au zaidi na kwa bei nafuu?

Jone Mwalwisi

Wapendwa
Nashukuru kwa mchango wenu na maelekezo yaliyo bora, Mapendekezo mliyonipa nimeyatumia. Mbegu nyingi zilipatikana maeneo ya Bagamoyo na mimi nafanya shughuli za kilimo Mkuranga, hivyo basi ingawa bei ilionekana ipo chini kwa mbegu za Bagamoyo suala la usafiri liliadd gharama kubwa sana ukizingatia natumia usafiri wa kukodi. Hivyo nikaamua kutumia vyanzo vya mkuranga hukuhuku, nimepata mbegu kwa bei ya shilingi 100/- kwa mtoa mbegu kufikisha mwenyewe shambani. The only disadvantage ni kuwa sijapata mbegu nyingi za kutimiza lengo nililoweka, ila haijaniumiza sana kwani kwa vile ndio kwanza naanza acha nianze katika scale ndogo.

Kwa mara nyingine tena asanteni sana
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
34,457
2,000
Wakuu naomba kujua wapi ninaweza kupata mbegu ya minanasi, nina kajieneo mahali sina plan nako kwa mwaka huu hadi mwishoni mwa mwaka kesho. sasa sitaki kukaacha kakae bure ni wapi ninaweza kupata kama miche 40,000 au zaidi na kwa bei nafuu?

Jone Mwalwisi
Ingekua 100 ningekwambia njoo uchukue lakini 40000??? Mingi sana.
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
13,355
2,000
Mkuu Mwalwisi.

Uko maeneo gani ?.Pwani,Dar na Tanga ni maeneo yanayostawi mananasi,yapo mananasi yanayostawi kanda ya ziwa Geita na eneo kubwa la kanda hiyo.

Kama unaishi maeneo ya mkoa wa Pwani,Tanga na Dar nakushauri tembelea Kiwangwa ni eneo mashuhuri kwa kilimo cha nanasi na upatikanaji wa miche ya nanasi ni rahisi sana mche mmoja unauzwa kati ya tsh 30 - 50.Eka moja ya nanasi inaingia miche 10,000 - 12,000.Ni vyema ukaandaa eneo lako mapema kwasababu minanasi inaweza kupandwa hata kipindi cha kiangazi.
 
CAMARADERIE

CAMARADERIE

JF-Expert Member
4,428
1,250
Mpigie huyu 0714-298116 mche mmoja ni kati ya shs25 na 30
 
BUBE

BUBE

JF-Expert Member
844
195
Kama upo maeneo ya Mkuranga ni PM. Zipo nyingi hapa Dundani na Mwanambaya
 
M

mwalwisi

Member
45
0
Mkuu Mwalwisi.

Uko maeneo gani ?.Pwani,Dar na Tanga ni maeneo yanayostawi mananasi,yapo mananasi yanayostawi kanda ya ziwa Geita na eneo kubwa la kanda hiyo.

Kama unaishi maeneo ya mkoa wa Pwani,Tanga na Dar nakushauri tembelea Kiwangwa ni eneo mashuhuri kwa kilimo cha nanasi na upatikanaji wa miche ya nanasi ni rahisi sana mche mmoja unauzwa kati ya tsh 30 - 50.Eka moja ya nanasi inaingia miche 10,000 - 12,000.Ni vyema ukaandaa eneo lako mapema kwasababu minanasi inaweza kupandwa hata kipindi cha kiangazi.
Kaka nipo Dar nalimia Mkuranga katika vijiji vya mkiu na Mkuruwili, nahitaji mbegu kwa ajili ya mkuruwili
 
Sabayi

Sabayi

JF-Expert Member
2,314
1,225
Hivi nanasi tangu lipandwe hadi lizae linachukua muda gani?
 
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
2,214
1,500
Labda kama alitumia ya mtu. Mimi aliniuzia miche 280,000
mkuu unaweza kutupa dondoo kidogo ktk hiyo miche ulifanikiwa kuvuna mananasi mangapi na kwa kiwango kipi (ubora)? if you dont mind na mapato kwa kukadiria
 
CAMARADERIE

CAMARADERIE

JF-Expert Member
4,428
1,250
mkuu unaweza kutupa dondoo kidogo ktk hiyo miche ulifanikiwa kuvuna mananasi mangapi na kwa kiwango kipi (ubora)? if you dont na mapato kwa kukadiria
Nimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000
 
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
2,214
1,500
Nimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000
mkuu safi sana, mimi huwa nayapanda kienyeji sehemu yoyote ambayo ina nafasi shambani huwa nayachanganya na mazao mengine kama mahindi, maharage, matikiti etc kwahiyo sielewi nalima hekari ngapi za mananasi na matikiti lakini mwishoni huwa naingiza fedha nzuri sana
 
Forum statistics

Threads
1,424,512

Messages
35,065,363

Members
537,998
Top Bottom