Utajiri ndani ya kilimo cha nanasi Kiwangwa

Dec 23, 2017
35
69
Zao la nanasi ni zao ambalo kiasili ni zao linalovumilia ukame na ni zao ambalo la kibiashara lenye faida kubwa.

Kwa hapa Tanzania yapo maeneo mengi ambapo zao hili la nanasi linastawi ila katika mji wa KIWANGWA-BAGAMOYO zao hili linastawi zaidi kutokana na hali ya mwinuko wake kutoka usawa wa bahari pia ardhi nzuri yenye rutuba ya kutosha.

Maeneo mengine yanayolima zao hili ni pamoja na Geita, Kigoma, Shinyanga, Lindi na Mtwara. Kwa baadhi ya maeneo ya Pwani ni Mkuranga, Kibiti na Kibaha.

Sasa leo nitakupa faida ya jinsi ya kulilima nanasi na jinsi ya kujipatia kipato twende wote mpaka mwisho....

NANASI LA KIWANGWA LIPOJE
Katika maeneo yote zao hili linapolimwa KIWANGWA ndiyo sehemu pekee unakutana na mbegu aina ya mpigo nanasi ambalo halistawi kwengine isipokuwa kiwangwa tu.

Pia nanasi la Kiwangwa kiasili ni tamu na ndiyo lenye msimu mzuri wa kilimo. Pamoja na yote rahisi kulifanyia usafirishaji kutokana na ukaribu na miji yote ya kibiashara kulizunguka eneo hili.

NB: Ni kawaida sana kumkuta mkulima wa nanasi wa KIWANGWA anamiliki magari majumba na mali za kutosha ilihali elimu yake ni darasa la saba.

JINSI YA KULIMA NANASI (MAHITAJI)

1. ENEO

Hapa kuna aina mbili za maeneo ya kuanzishia kilimo cha nanasi
i-Shamba jipya, hili ni lile jipya ambalo utaanza kukata miti n.k
ii-Shamba la zamani ambalo hili lilishalimwa limwa

Mashamba yote haya yanapatikana kwa namna mbili
i-Kukodi (laki tano kwa miaka mitano)
ii-Kununua (inategemea ubora wa ardhi, na umbali kutoka kwenye lami)

Kwanini tunaangalia umbali?
Tunaangalia umbali ili isije kusumbua wakati wa kuuza kulileta sokoni. Hivyo umbali ni kitu cha msingi na kujua miundombinu kunafikika kipindi cha mvua.

NB: Tunashauri kama unaanza na hauna hela anza kukodi ila ukinunua ni nzuri zaidi..

2. MBEGU
Kwa kawaida mbegu moja inauzwa wastani wa Tsh 20- 35 inategeemea na wakati kuna muda huwa chini kuna muda hupanda ila haizidi hapo.

Ni bora ukachukua mbegu za wastani na siyo ndogo sana au kubwa sana siyo nzuri kabisa kuzitumia...

Kwa shamba la hekari moja huitaji miche elfu 18 kwa upandaji wa kisasa au hata elfu 16. Tunapanda hivi ili isaidie kupata mananasi makubwa.

GHARAMA ZA KUPANDA
Mbegu tsh 35 × 18000
Kuvunja mbegu baada ya kununua tsh 10 × 18000
Kupakia kwenye gari na kushusha tsh 4 × 18000
Kupanda baada mbegu kufika shamba tsh 50 × 18000

MAANDALIZI YA SHAMBA
Kukodi laki tano
Kusafisha Tsh 80000
Trekta Tsh 50000

NB: Gharama za mbegu ni za mara moja tu mwanzoni unapoanza baada ya hapo zitakuwa zinajizalisha zenye kwahiyo utakuwa nyingine unauza na wewe pia utatumia za kukutosha..

PALIZI
Mpaka unavuna nanasi linahitaji si chini ya pali saba mpaka kumi

CHANGAMOTO ZA KILIMO
Hakuna jambo linalokosa changamoto ila kwa bahati nzuri zao hili halina changamoto ya wadudu wala sijui mvua hakuna nanasi hata iweje lazima liote tu hata kama utakisusa changamoto kubwa ni mbili au tatu...

1. Usimamizi mbovu
2. Ukosefu wa huduma kwa wakati
3. Kwenda kombo kwa soko(ila kwa ulimaji wa kisasa ni rahisi kuliepuka hili)

Muendelezo soma - Muendelezo soma hapa


73330d289587b8c1c6505585455693ad.jpg
0ce190498d38725b43a23ebfe7abafe9.jpg
images%20(19).jpg
images%20(18).jpg
images%20(16).jpg
images%20(15).jpg
images%20(13).jpg
images%20(14).jpg
images%20(10).jpg
images%20(10).jpg
images%20(9).jpg
images%20(6).jpg
images%20(7).jpg
images%20(8).jpg
images%20(5).jpg
73330d289587b8c1c6505585455693ad.jpg
 

Attachments

  • images%20(12).jpg
    images%20(12).jpg
    21.7 KB · Views: 48
  • images%20(11).jpg
    images%20(11).jpg
    21 KB · Views: 49
  • images%20(12).jpg
    images%20(12).jpg
    21.7 KB · Views: 49
  • images%20(4).jpg
    images%20(4).jpg
    51.9 KB · Views: 39
Wiki hii nitaenda shambani kwangu Fukayosi. Nimelima nanasi kwenye heka moja na nyumba ya mtu anaeishi hapo. Alichosema jamaa yuko sahihi mnooo.

Na ndio ukweli kabisa. Na mimi mbegu nilichukua kabla ya kufika Kiwangwa maeneo ya fitina haina posho. Sema nanasi za wilaya ya Bagamoyo ni tamu sana jamani. Nimepanda miche elfu 12 kwa kuweka nafasi kubwa kati y mche na mche.

Sema aliekuwa mbunge wa Bagamoyo, Shukuru Kawambwa jamani analima nanasi sio poa, kukagua shamba wakati wa palizi anatumia gari kupita ndani ya shamba. Mimi na macho yangu nimejionea hilo shamba na sio moja.

Pia kuna wakulima wengi tu wako vizuri kama mbunge Eric Shigongo. Hawa nimewataja kwakuwa ni maarufu tu. Ila underground wako poa.

Hapo miche ni mwaka jana ikiwa na miezi 9 tu.

20220824_132135.jpg
20220824_132135.jpg
 
Hapa anatafutwa mtu hapa na mrejesho mlete hapa hapa
chif hapa apigwi mtu,alichosema mleta mada ni ukweli tupu.

kama miaka mitano nyuma nilifka Kiwangwa sehemu moja inaitwa Mwavi nilienda kumsalimia swahiba wangu niliyesoma nae.aliamua kurudi huko kumsaidia mzee wake kwenye usimamizi na kuhudumia mashamba ya nanasi.
Bagamoyo sio mbali kama upo Dar fanya ziara huko Kiwangwa angalau tu ukaone fursa zipi zinapatikana huko.
 
Pia palizi umesema mpaka kuvuna ni mara kumi je gharama ni kiasi gani kwa makadirio
 
Leo tunaendelea pale tulipoishia jana ila kwana niseme natoa somo hili ili kuwafungua watu waone fursa zingine nje ya zile wanazozifikilia.

SI CHINI ya milioni mbili mpaka tatu utawekeza kwenye nanasi ingawa uzuri wake kamwe haitoki pamoja unaweza ukakuta laki laki au hamsini hamsini mpaka mwisho wastani nanasi moja mpaka linafikia kuvuna ni shilingi 190 sasa zidisha mara miche elfu 18,16,15 inategemea unahitaji liweje.

Kwa kawaida baada ya kulima vizuri kwa kufuata taratibu zote za kilimo hiki kinachofuata itakuwa ni kuuza mananasi yako.

Nanasi huchukua mwaka na nusu(kisasa zaidi) au miaka miwili pia kama huli hudumii linaweza kukaa hata miaka mitatu mpaka kuvuna.

Kwa huku kiwangwa uvunaji unafanyika mara tatu
1- kipindi cha msimu mkuu( october - februari)
2-Demani
Kuna demani mbili ndani ya mwaka ile ya mwezi wa tatu na ile ya mwezi wa tisa na kipindi hiki nanasi inakuwa na hela sana sema shambani huwa ni machache...

Kwa sasa kuna mbolea maalumu ambayo hustawisha nanasi mapema ambapo kibiashara ni nzuri sana kwani nanasi unaamua uvune wakati..

NB:
Kwa bahati mbaya mbolea hiyo ni ghali ila ndiyo nanasi lenye hela sana kwani nanasi lake huvunwa mwezi wa saba,nane na tisa kipindi ambacho sokoni hakuna tunda lolote....

UUZAJI KWA UJUMLA
Nanasi moja utauza kwa wastani wa shilingi 250 mpaka 600 hapa utauza yaani kwenye nanasi tukisema umekosa na tunaita hasara yaani utapata si chini ya milioni tatu haishuki zaidi ya hapo(utarudisha uwekezaji wako)...

Kifupi nanasi halina kukosa kabisa hichokitu hakipo hata iweje,na sisemi kwaajili ya kukutia moyo hapana huo ndiyo uhalisia...

MASOKO
Kuna aina mbili za masoko
1- kuuzia shamba bei ndiyo 200- 600 kutegemea na ukubwa
2-kuuzia kijiweni bei 500 - 3000 kutegemea ukubwa

NB:
Kuuza vijiweni ni nzuri zaidi na inafaida kubwa sana ila uwe na kijiwe kinacho ruhusu mchangamano mkubwa wa watu kama vile stand,nje ya nyumba za ibada n.k

CHANGAMOTO
Narudia kilimo hiki hakina changamoto ya wadudu wala kukosekana kwa mvua changamoto kubwa ni wingi wa mananasi tunaita humbo huwa hapo bei inashuka...

Pamoja na HUMBO HILO ila nanasi utauza tu ila nakushauri lima kisasa kukwepa kukutana na msimu....
NB:
Unaweza chukua muda wako siku tembelea maeneo ya kiwangwa,mwavi,magogoni,msinune,misani,kijiweni uje ujionee kilimo hiki tunakukarubisha sana....

Kumbuka kama hutalima unaweza pia kuwa mfanyabiashara wa tunda hili
 
Leo tunaendelea pale tulipoishia jana ila kwana niseme natoa somo hili ili kuwafungua watu waone fursa zingine nje ya zile wanazozifikilia.

SI CHINI ya milioni mbili mpaka tatu utawekeza kwenye nanasi ingawa uzuri wake kamwe haitoki pamoja unaweza ukakuta laki laki au hamsini hamsini mpaka mwisho wastani nanasi moja mpaka linafikia kuvuna ni shilingi 190 sasa zidisha mara miche elfu 18,16,15 inategemea unahitaji liweje.

Kwa kawaida baada ya kulima vizuri kwa kufuata taratibu zote za kilimo hiki kinachofuata itakuwa ni kuuza mananasi yako.

Nanasi huchukua mwaka na nusu(kisasa zaidi) au miaka miwili pia kama huli hudumii linaweza kukaa hata miaka mitatu mpaka kuvuna.

Kwa huku kiwangwa uvunaji unafanyika mara tatu
1- kipindi cha msimu mkuu( october - februari)
2-Demani
Kuna demani mbili ndani ya mwaka ile ya mwezi wa tatu na ile ya mwezi wa tisa na kipindi hiki nanasi inakuwa na hela sana sema shambani huwa ni machache...

Kwa sasa kuna mbolea maalumu ambayo hustawisha nanasi mapema ambapo kibiashara ni nzuri sana kwani nanasi unaamua uvune wakati..

NB:
Kwa bahati mbaya mbolea hiyo ni ghali ila ndiyo nanasi lenye hela sana kwani nanasi lake huvunwa mwezi wa saba,nane na tisa kipindi ambacho sokoni hakuna tunda lolote....

UUZAJI KWA UJUMLA
Nanasi moja utauza kwa wastani wa shilingi 250 mpaka 600 hapa utauza yaani kwenye nanasi tukisema umekosa na tunaita hasara yaani utapata si chini ya milioni tatu haishuki zaidi ya hapo(utarudisha uwekezaji wako)...

Kifupi nanasi halina kukosa kabisa hichokitu hakipo hata iweje,na sisemi kwaajili ya kukutia moyo hapana huo ndiyo uhalisia...

MASOKO
Kuna aina mbili za masoko
1- kuuzia shamba bei ndiyo 200- 600 kutegemea na ukubwa
2-kuuzia kijiweni bei 500 - 3000 kutegemea ukubwa

NB:
Kuuza vijiweni ni nzuri zaidi na inafaida kubwa sana ila uwe na kijiwe kinacho ruhusu mchangamano mkubwa wa watu kama vile stand,nje ya nyumba za ibada n.k

CHANGAMOTO
Narudia kilimo hiki hakina changamoto ya wadudu wala kukosekana kwa mvua changamoto kubwa ni wingi wa mananasi tunaita humbo huwa hapo bei inashuka...

Pamoja na HUMBO HILO ila nanasi utauza tu ila nakushauri lima kisasa kukwepa kukutana na msimu....
NB:
Unaweza chukua muda wako siku tembelea maeneo ya kiwangwa,mwavi,magogoni,msinune,misani,kijiweni uje ujionee kilimo hiki tunakukarubisha sana....

Kumbuka kama hutalima unaweza pia kuwa mfanyabiashara wa tunda hili

Kwa maelezo zaidi
0621180082
0719929030
Mzee uliposema misani umenikumbusha mbali sana aisee nilikuwepo kama mwanafunzi wa sekondari ya Kiwangwa 2005-2008 kiukweli Kiwangwa imebarikiwa sana.

Nitakuja kuwekeza hapo one day...Mungu aniongoze katika hilo.
 
Umenikumbusha mbali kidogo mkuu, kipindi fulani nipo najitafuta sina hili wala lile nipo kitaa tu mishe hazisomeki...

Nikakutana na jamaa mmoja mchacharikaji kidogo wanamuita CHAPAKA ( jina la utani ), huyu jamaa alikua ni mwenyeji wa huko kiwangwa. Alikua ni bodaboda pale bagamoyo stand, na hapo ndipo nilipojuana nae maana ni mtu wa stori sana. Nilikua napanda bodaboda kwa Tsh 500/=, YES ni JERO tu kutoka hapo stand hadi soko la mwembe yanga, hii ilikua ni 2019 - 2021 kwaiyo sina hakika kama bado ipo hiyo ukizingatia kupanda kwa hizi gharama za maisha.

Jamaa kila msimu alikua ananunua nanasi huko mashambani anakuja kuuza bagamoyo na kijiwe chake kilikua stand ya daladala palepale kwenye maskani ya bodaboda. Dah kuona ile idea nikavutiwa nayo kidogo nikaona ngoja nimuulize anaipe ramani ya hii kitu.

Home kulikua na gari ( pick up ) kuu kuu imepaki tu nje haitumiki imekaa inaozeana tu pale, sasa nilipoona idea ya nanasi kwa chapaka ndio nika connect dots zangu nikaona YES tunaweza kufanya kitu katika ukubwa fulani.

Siku moja nikamfata kijiweni kwake chapaka nikamwambia mwanangu ukifunga ofisi naomba twende kiwanja flani kumwagilia moyo kidogo pamoja na kusuka ramani za kimaisha, kwa sababu tulishazoeana jamaa hakua na pingamizi akanambia poa mida fulani ntakucheki.

Kwasababu nilikua na vipesa vyangu kidogo nikamuita mshkaji mmoja mtaani pale jamaa ninfundi tukaipiga gari service kidogo pamoja na kufanya ukaguz mwengine, jamaa akanambia gari ipo sawa lakin brake pads za nyuma zimeisha, kipara kabisa yaani.

Nikamwambia midhali gari inawaka na inatembea hizo brake pads nitabadiki siku nyengine maana gari ni manual, ( wazee wa manual nadhani mtakua mnaijua ile style ya chench down, itakusaidia kusimama bila hata kutumia brakes )

Basi buaana usiku mida ya saa 3 nikampitia pale kijiweni tukaenda baa flani nimeisahau jina, nikaagiza nyama choma 2 plates na ugali, msosi ulivyokuja nikaanzisha mada.

_______

_______

_______


Kiufupi jamaa alikubali kunipa A to Z ya ile biashara na nikamuomba trip ya mwanzo atakapoenda kufata mzigo wake basi tuongozane nami nikafunge wakwangu ili nizijue chochoro zote anazopita kupata mzigo mzuri wa bei chee, akakubali basi tukasubiri siku 1 amalizie mzigo wake, siku ya pili tuanze safari.

Isiku iliuowadia saa 1 asubuhi tukaanza safari dereva mwenyewe, chapa gia around saa 2 haoo tukaingia kiwangwa, tuka park gari pale pembezoni ya barabara tukapiga breakfast kabisa baada ya hapo tukachukua bodaboda tukaingia mashambani sasa ( unajua kule mashambani kuna madalali kwaiyo kama sio mwenyeji inabidi utafute msaada wabdalali, yeye ndio anajua wakulipa wote mashamba yao yalipo ana fulani ana mzigo fulani hana kashamaliza )

Sasa kwasababu nilikua na sterring CHAPAKA niliepuka hizi kero za kukimbizana na madalali jamaa anazijua chocho zote za kule na anafahamiana na madalali maana madalali nao wanamjua kama dalali mwenzao ( dah jamaa nilikua na mchukulia poa kumbe ni DOUBLE AGENT kabisa )

Basi kwa kua nilikua na jamaa tulizungukia mashamba 2 tu tukapata mzigo wa 150k, yaani tulikua tunanunua kwa size tofaut kubwa zaidi, kubwa, wastani, ndogo ili tukienda kuuza tusiache hela. Baada ya kufunga mzigo ili bidi tusubiri jua lizame kwanza ili kuwaepuka wale yange yange barabarani.

Tukaenda kwao kwa wazazi wake na jamaa nikakaribishwa pale nikatulia zangu jamvini nikaanza kuruzura JF .

Saa 12 : 30 tukatoka kiwangwa kurudi bagamoyo... Tulipofika baga nikamwambia huu mzigo kwasababu nina gari nitaenda kuuza DAR kariakoo maana nilitaka siku inayofuata niuze nimalize nigeuze siku hiyo hiyo nirudi kiwangwa, jamaa akashangaa sana inawezekanaje ( maana yeye kashazoea anakaa na mzigo siku 3 alafu mzigo wa 70 tu, sasa inakuaje mzigo wab150k uishe kwa siku moja ) akasema inabidi twende wote, mzigo wake atamuachia mu amuuzie kisha yeye aje kusaidiana kuuza mzigo wangu apate experience mpya. Nikamwambia kama ni hivyo njoo ulale hapa home maana kesho tunaondoka alfajiri 11 kamili.

Kesho yake 11 : 00 imetukutia barabarani kuelekea kariakoo ( lengo la kutoka alfajiri ni kuwaepuka trafic na kupata parking nzuri kariakoo )

Around 12 na madakika tukakawa kariakoo natafuta parking nikaona ngoja nika park sokoni pale nivutika na mtaa wa tandamti / sikukuu. Aisee hata kabla gari haijapaki wale wafanyabiashara pale sokoni wakatuvamia, tukaanza kuuza mzigo kwa spidi ya hatari, nanasi tulionunua 500 tulikua tunauza 1500 na zile nanasi za bei ndogo kabisa tulikua tunauza 700 - 800.

Hadi kufika saa 9 almost mzigo wote tumemaliza maana zilikua zimebaki pisi chache tu pale, tukakomaa komaa mida ya 11 jioni mzigonwote umeisha nikalipa mdada wa parking 2000 kwa kutwa nzima nikapiga hesabu zangu nikakuta nina zaidi 450k yaani na maelfu kadhaa (sikumbuki real digit) nikampa CHAPAKA 30,000 kama ujira wa kuuza nanasi. Kifupi nilipiga takribadi 250,000 faida ghafi ukitoka expenses zote... Mafuta, msosi, parking n.k

Saa 1 jioni tukawa barabarani kurudi bagamoyo huku storry za furaha zikitamalaki, nikaona this is a real deal, hata chapaka mwenyewe alionekana kudata ( famchezo nini ).

Nikawa namuhoji ni mazao gani mengine yanapatikanankwa wingi kule kwa bei rahisi ili msimu wa nanasi ukikata nishike kwengine, akaniambia ndizi mzuzu, aisee kule kiwangwa wanauza kati ya 5000 hadi 8000 mkungu, alafu sokoni kariakoo ni 15,000 na hazina msimu , aiseee nikamwambia chapaka tushatoboa maisha, sasa ni kuanza kazi.


Anyways mtoa mada umenikumbusha tu sehemu ya hustles zangu nilizowahi kupitia, japokua hivi sasa nafanya biashara nyengine kabisa sio ya mazao wala matunda.

Kiwangwa kazi iendelee.

Alamsiki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom