Uchaguzi 2020 Kilimanjaro: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,829
12,010
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kilimanjaro. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Kilimanjaro una una jumla ya majimbo ya uchaguzi 9. Walioshinda katika hayo majimbo ambayo ni;

1. Hai:
Saasisha Mafue (CCM) - Kura - 89,786
Freeman Mbowe (CHADEMA) - Kura 27, 684

2. Siha:
Godwin Mollel (CCM) - Kura 22,172
Elvis Mossi (CHADEMA) - Kura 8,614

3. Moshi Mjini:
Priscus Tarimo(CCM) - Kura 31,169.
Raymond Mboya(CHADEMA) - Kura 22,555

4. Mwanga:
Joseph Anania (CCM) - Kura 27,127
Henry John Kilewo (CHADEMA) - Kura 4,128

5. Same Mashiriki:
Anne Malecela(CCM) - Kura 26,225
Naghenjwa Livingstone (CHADEMA) - Kura 8,836.

6. Same Magharibi:
David Mathayo (CCM) - Kura 24,260
Gerivance Mgonja (CHADEMA) - Kura 758

7. Moshi Vijijini:
Patrick Ndakidemi (CCM) - Kura 53,891
Anthony Komu (NCCR Mageuzi) - Kura 3,888

8. Vunjo:
Dkt. Charles Kimei (CCM) - Kura 40,170
Grace Kiwelu wa (Chadema) - Kura 8,675
James Mbatia (NCCR Mageuzi) - Kura 4, 949
Agustino Mrema (TLP) - Kura 606.

9. Rombo:
Profesa. Adolf Mkenda(CCM) - Kura 48,122
Patrick Asenga (CHADEMA) - Kura 9,519

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
UPDATES mbalimbali

1) Wananchi wameanza kujitokeza. Hapa ni Kilimanjaro, Moshi mjini katika shule ya Langon

2603746_E1A9528F-AAA5-4789-906C-3220E68E2D5A.jpg
 
Kilimanjaro kumepoa sana tena sana kuliko chaguzi za nyuma, hiki ni kiashiria kwamba CCM itaibuka kidedea.
 
Hlf sasa watu hata kupiga kura hawajaenda kivile..kumepoa sana, Hai kwa mbowe nako kimya sana
Kama Mbowe anashindwa kusimama kama Mwanaume kutetea Jimbo lake dhidi ya Uharamia wa Sabaya, ajiuzulu Uenyekiti Wa Chama tu amwachie Tundu Lissu..
 
Kama Mbowe anashindwa kusimama kama Mwanaume kutetea Jimbo lake dhidi ya Uharamia Wa Sabaya, ajiuzulu Uenyekiti Wa Chama tu amwachie Tundu Lissu..
Shida ukisimama kiume uhai hautakua nao tena. Nani hapendi kuishi ndugu yangu!
Hata yeye unakuta yuko nyuma ya keyboard!
 
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kilimanjaro. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka...
Vip Hai?..maana Magufuli alilia sana kwa wananchi wamletee Saashisha
 
Kama Mbowe anashindwa kusimama kama Mwanaume kutetea Jimbo lake dhidi ya Uharamia wa Sabaya, ajiuzulu Uenyekiti Wa Chama tu amwachie Tundu Lissu..
Ole Sabaya haendi kupambana na Mbowe man to man, kumbuka anaenda kupambana na Mbowe kwa kivuli cha mwenyekiti wa kamati ya ulinzi & usalama wa wilaya...hivyo anakwenda na kundi la askari wenye silaha wanaomtii!!.

unataka Mbowe apambane vp hapo kama sio kumuonea?!.
 
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Jimbo la Moshi ametangaza matokeo kama ifuatavyo
Moshi >>>>>> CCM 31,169
Raymond Mbuya CHADEMA 22,555
DK. Malissa NCCR 59
SAU 93
ACT 374
 
Back
Top Bottom