Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,330
- 2,283
Kwanza nawapa pole wote waliokumbwa na janga lililotokea wilaya ya Hanang mji mdogo wa Kateshi.
Jambo la kujiuliza tutaendelea na majanga ya aina hii mpaka lini kwanini hatujifunzi? Mwaka 2009 lilitokea janga kama hili kule Same. www.jamiiforums.com/threads/wafariki-kwa-kufunikwa-na-mlima-same.44706/%3famp=1
Serikali ilitoa rambirambi na mambo yakapita, sasa ni Kateshi, serikali imefanya mengi sana pia litapita.
Je ni mwisho? Hapana ukiangalia kwenye milima ya Same kuna ujenzi mwingi sana holela, hivi mtu unajenga juu ya mlima au kando ya mlima maeneo yameisha? Kwanini wanadamu wana sahau mapema hivi? Serikali iko wapi?
Picha ya milima ya Same wakati wa usiku
Kosa si kosa, kosa kurudia kosa, serikali ichukue hatua sasa, ipime viwanja vya kutosha kila mji kila mtu anaetaka kujenga ajenge sehemu iliyopimwa na kuepukana na majanga haya.
Kawaida ya udongo ukiloa sana ni rahisi kumong'onyoka, kwa hiyo lazma ulete madhara kama kuna makaazi ya watu karibu.
Serikali iangalie sana hili.