Serikali: Mafuriko ya Katesh ni kuporomoka kwa mchanga wa mabaki ya mlipuko wa volkano uliotokea maelfu ya miaka

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Msemaji wa Serikali amesema Wananchi wa Hanang katika mji mdogo wa Katesh, na vitongoji vyake, mji mdogo wa Kateshi walisikia kelele ambazo walifananisha kama gari moshi likipita kwa kasi katika mlima wa Hanang ambapo katika usiku huo kulikuwa na mvua ya kawaida na si mvua kubwa sana ya kutisha, watu waliposikia huo mvumo, wapo walioamua kutoka nje ili wakaone ni nini, uamuzi wa kutoka nje wapo uliowaokoa na wengine ulichukua maisha ya wengine.

Baada ya kutoka nje, wakaona matope, magogo, maji yanakuja, kuna watu wanasema walikuwa wameshika watoto, mara magogo yakawagonga na kuwabeba, yaani wazee, kwa vijana watu na nyumba, maduka na vyote vilivyokuwa kwenye njia ya maji na matope vilisombwa. Nyumba, soko, kiwanda cha vinywaji zilisombwa kiasi kwamba ukifika eneo hilo huwezi jua kama watu waliwahi kuishi hapo.

Wataalam wetu wametumia sayansi, huwa wakati mwingine tunafikiria nchi zetu zinazoendelea hazina wataalam, ila tunaweza kuwa mbele kuliko hizo nchi zilizoendelea kwa kuwa changamoto tunazopitia tunajenga wataalam wenye uwezo mkubwa, kwa hiyo wataalam wetu kutoka Wizara ya madini walifika eneo hilo siku ileile ya tukio.

Kwanza kabisa uongozi wa Wilaya uliinuka kuja kupambana na tukio, ila ukajikuta unapambana na kitu kikubwa mo ikabidi uombe msaada kwa uongozi wa mkoa, na kufika siku hiyo jioni tulikuwa tayari na mamia ya vikosi vya uokoaji, hili ni janga ambalo hatujawahi kulipata Tanzania, tumewahi kupata mafuriko, ila hii ilikuwa ni zaidi ya mafuriko.

Kwa siku ya pili kazi zikaendelea na wataalam wetu walipanda kwa miguu wakawa wanapishana na mawe mengine yanashuka na wengine walipelekwa kwa helkopta, ili kufanya uchunguzi, maana tulikuwa tunahofu janga hili lisije kujirudia baada ya masaa machache.

Wataalam wetu wakaenda kuchunguza ule mlima kwa haraka, wakakuta ule mlima umeundwa na miamba laini, miamba laini ambao una mchanga wa mabaki ya mlipuko wa volkano ambayo ilitokea mamia maelefuya miaka huko, yalikuwa yakifyonza maji, kwa hiyo ikawa yameshiba, kwa hiyo ilipokuja hii mvua ya kawaida tu yale maudongo yanayouda ule mlima yakawa yamefikia mwisho yakashindwa kuyabeba maji kwa hiyo yakashuka, yale madongo yalikuwa na mawe na miti, yakageuka kuwa tope na miti ilivunjwa vunjwa .

Pale chini ya mlima kulikuwa na banio la maji, maji yakitoka huko yanakaa hapo halafu yanasambazwa kwenye matanki, kwa hiyo hilo banio likavunjwa na ndio maji yakawa mengi sana, na kuanza kutembea kama mto, mawe, maji, matope mito, na nyumba za kwanza kuvunjwa nazo zikageuka silaha za kuvunjwa na kubeba miti, nyumba, wanyama, magari soko, kiwanda na watu wengine.

Walikuja watu wa sensa ya watu na makazi, vile vishikwambi vina uwezo wa kutambua, wakibonyeza kama hapa kulikuwa na nyumba mahali fulani. Kwa hiyo kwa kutumia wataalam hao wa sensa tathimini za awali tumegundua zaidi ya nyumba 100 hazipo.
 
Back
Top Bottom