Allah subhaanahu wataa'la- ndiye aliyetuumba sisi na tunayoyafanya.
Na yeye ndiye aliyeumba uhai na mauti ili kututahini, ni yupi kati yetu atakayefanya matendo mazuri.
Hivyo ametupa uhuru wa kutenda, na katika hili sote ni mashahidi ya uhuru huo.
Mfano wewe unao uamuzi wa kujijibu hii komenti yangu au kuiacha, na ndivyo hivyohivyo unavyoweza kuamua kumuamini Mwenyezimungu au kumkufuru, kumtii/kumuasi, kuzini/kuoa, kufanya kazi/ kuiba n.k
Na hayo yote ni matendo yako maana utayatenda kwa hiari yako.
Allah subhaanahu wataa'la- aliweza kupeleka hawa motoni na hawa motoni kwa elimu yake tu.
Lakini kwa hekma zake, rehema zake, na uadilifu wake, ametuleta nyumba ya matendo(duniani) na akatupa uhuru wa kutenda ili akatuhukumia kwa uadilifu katika nyumba ya malipo(akhera).
Hivyo hapa duniani kuna wema na waovu, hivyo kuna mema na maovu.
Umetoa mfano wa mauwaji, kwa sababu huu ndio uovu mkubwa ambao wanaadamu tunaweza kufanyiana, sijui kama kuna zaidi ya hapo, yaani mtu ubaya wa mwisho anaoweza kukufanyia ni kukuuwa tu.
Lakini kwa Allah subhaanahu wataa'la- kufa sio mwisho bali ni mwanzo wa maisha mengine ya akhera, ambayo mwanzo wake ni siku ya qiyama(siku ya malipo)
Siku ambayo tutafufuliwa na kulipwa kulingana na matendo yetu, na jambo la kwanza ambalo Allah atalihukumia ni suala la umwagaji damu(haki ya damu).
Hii haina kafiri Wala muislamu hata kama muislamu alimuuwa kafiri kwa kimdhulumu atahukumiwa siku hiyo.
Hivyo stori yako ya bwana Calvin haitoishia hapo, kuna siku ya malipo.
Hivyo utagundua kuwa kitendo cha Calvin kuwauwa hao wadada, amewadhulumu hivyo madada watapata haki yao, na kelvin atapa hukmu yake.
Na utagundua kuwa Calvin ni sababu tu yakifo cha hao wadada, kwa sababu hata kama asingewauwa yeye huwenda wangekufa kwa corona, kwa sababu kifo ni haki ya kila mtu.
Na pia utagundua kuwa kufa ni ishu kwa hapa duniani ila on the other hand ni kituo cha kwenda akhera kwenye maisha ya milele.
Wallahu aa'lam.