Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Kila mwaka tangu mpendwa wetu ashike madaraka ya uraisi kumekuwa na maadhimisho ya kuazimisha madaraka yake.
Je, haya mabango, matangazo kwenye vyombo vya habari, Makongamano na dhifa zinazoandaliwa zipo kwenye bajeti ya serikali au kuna wafadhili wenye moyo mwema wanaochangia gharama za maadhimisho haya?
Tunasikia orodha ndefu zinatajwa za aliyoyafanya ambapo mengi hayaonekaniki kwa macho bali tunalazimishwa kwenye orodha kuwa yamefanyika na utukufu unaenda kwake. Ina maana Watanzania hawana taarifa ama ufahamu wa nchi yao? Je, aliapishwa madarakani ili akae tu na asifanye lolote kiasi kwamba akifanya hata jambo dogo zitatumika gharama kubwa kulitangaza?
Tumeshuhudia misafara mikubwa ya watendaji waandamizi wa serikali kwenda kuzindua matundu ya vyoo na kadhalika ambapo gharama za masurufu ya misafara hiyo zingetisha kupunguza vifo vya mama na mtoto wanaokosa tiba bora hususani kipindi hiki ambacho dada Ummy ameshikilia ofisi ya Afya.
Wakati tunakumbuka mema na mabaya ya Hayati JPM, kinachofuatia na kinafanywa kwa nguvu kubwa ni kuadhimisha miaka kadhaa ya utawala wa mama. Ninaomba kuelimishwa haya

- Umuhimu wake
- Taifa linapata tija gani kwenye hizi kumbukizi?
- Ni utekelezaji wa ilani?