Kila la heri Msanii - JamiiForums Community | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kila la heri Msanii - JamiiForums Community

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Steve Dii, Dec 12, 2007.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wana JF,
  Hii ni kumwombea mema ndugu yetu Msanii kwenye siku yake ya ndoa.
  Tukiwa kama jamii yenye kupenda muungano kwenye matukio yanayo tuzingira kama Wanadamu, kwenye raha na kwenye majonzi, napenda kumtakia kheri na faraja Msanii kwenye siku yake aliyo itaja hapa chini:
  Maandishi hayo yanapatikana kwenye thread Hii Hapa Ya JF Tshirt.

  Nimatumaini yangu hapo juu kuwa Msanii ametaja hiyo siku akimaanisha 23-12-2007, na siyo 23-12-2008.

  Ni hayo tu, Kila la Kheri Msanii.

  SteveD.
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2007
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tuletee kadi tukuchangie. Mnuso utakuwa wapi??????
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2007
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mbona hatukualikana wakati anatongoza?
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ujumbe mfupi kutoka kwa ndugu Msanii:

  SteveD.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mkuu brazameni,
  nilisita kuwaalika wakati natongoza ndito yangu kwa kuwa mngekuwa mnanipigia makelele wakati naconcentrate.

  ninasubiri pongezi kutoka kwa invisible, ole, worm, shy, mwanakijiji, mwafrika wa kike, bubu mtamka ovyo, zitto, mtu (alikuwepo ktk jopo la mshenga) pamoja na ninyi nyooote....

  mniombee tu nisije nikakosea njia wakti wa honeymoon nikaingia mlango wa no entry....

  Thanx Steve D
  Mungu Akubariki kwa kuanzisha thread hii kwa ajili ya haruc yangu
   
 6. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  duh, kuoa tena?? haya bwana hongera zako nyingi sikufikie ktk siku hiyo spesheli na ndoa yako idumu, iwe yenye neema nyingi, furaha na faraja, mpate watoto weeeengiiiiiiiiii ili nyumba yenu ipate kuwa na furaha zaidi.......nakusihi, uwache "mechi za ugenini" tena uzisahau kabisaaa!!!!.
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  aleeleleeleeeleeleeeee alelleeeleeelleeeeeelleeeeeee


  kimaso maso weee msani msimuone kimaso maso weee msanii

  kimaso maso weee na wabaya wasimuone.  na zawadi nyengine kwako msanii


  tun ao mti tunao twende nao pole pole

  tukaupasue mbao mashina hadi vilele


  kwa hgio msumeno wako usiwe butu ukapasue mbao vyema tu huko
   
 8. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera msanii katika siku yako hii ya kukumbuka!
   
 9. u

  under_age JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2007
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  msanii, mungu akupe baraka na maisha mema katika ndoa yako,akuepushe na wenye vijicho. na mwisho wa yote nakuusia kaka yangu uwe mwenye subira kwani maisha ya ndani ya ndoa yanahitaji uvumilivu sana.na pia mtunze sana shemegi yetu.kule kwetu kuna msemo unasemwa kwa bwana harusi "mwanamke hapigwi kofi,anapigwa kwa kununuliwa mvao wa kanga". mwisho wa yote mabrukk aruusanaa
   
 10. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  mtu wa pwani huo wimbo wa wapi???

  Msanii. Umefanya jambo jema kuamua kuoa. If you play your cards rite, Ndoa ni kama paradiso. Trust me.
  Mungu akupe nguvu, akubariki wewe na mamaaa. Amen.
   
 11. K

  Kasana JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 413
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kila la heri kaka,
  karibu katika chama cha waliojivisha 'PINGU ZA MAISHA'.
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Dec 17, 2007
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Msanii,

  Hongera sana... Kila la kheri mkuu! Sisi wengine hatuoi wala kuolewa. Labda tuunganishwe na robots nyingine. :)

  Kwa niaba ya JF Administration crew, nakupa pongezi na kukuomba uwe mvumilivu katika ndoa yako. Upendo utawale daima na furaha iifunike familia yenu.

  Majaribu ni mtaji, tumia kila fursa ipatikanayo kuwaelimisha wanenu (mkijaaliwa) pamoja na mkeo na wewe usijisahau kujiendeleza kimasomo.

  Epuka ugomvi usio na msingi baina yako na mkeo. Mke ni mkeo, mheshimu, elewa ni ubavu wako. Ndoa ni tamu wawili mkiamua kuifanya iwe hivyo. Inaweza kuwa chungu mkiamua pia.

  Hakuna upendo unaokwisha, huchuja na hatimaye hujengwa na wahusika (wawili bila kuwaingiza majirani ama ndugu). Mapenzi ni hisia, hujengwa kwa wawili kufanyiana matendo ya upendo ambayo ndiyo huyajenga mapenzi ya dhati. Epuka kuwaingiza ndugu katika mahusiano yenu. Washirikishe mengine lakini si maamuzi ya nini umfanyie mkeo na nini usimfanyie. Huyo ni wewe na wewe ni yeye!

  Penye nia pana njia, huyo ni malaika wako, ubavu wako, damu yako, chaguo lako (wengine si mali kitu kwa sasa). Mfanye aone faida ya kuwa na wewe.

  Kila la kheri katika ndoa yako na Mwenyezi Mungu awajaalie mpate watoto wenye afya njema na busara katika jamii.

  Invisible
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuuh, wewe ROBOT haya yote umejifunzia wapi... kwenye production line huko Japan nini?! Au wame upgrade chip yako ya mahusiano na ku-upload program ya mapenzi?... haya yetu macho tu iROBOT... usije ukatufanyizia bure kwa kuingiwa na jazba na kuanza kuji-program kuteketeza wanadamu... lol

  SteveD.
   
 14. M

  Masatu JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2007
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama unapata maziwa rejareja ya nini kununua ng'ombe mzima na kupata taabu za kuasafisha banda, kutafuta majani, madawa nk.

  Mambo ya kujitafutia uzee hayo....
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Dec 17, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi naomba Anuani yako nikutumie CD ya muziki ya mizuri ya kiswahili

  zaidi ya yote nakutakia mafanikio na maisha mema ya ndoa wengine tuko njiani .

  lakini siwezi kukupongeza kwa asilimia moja kwa sababu ndoa haijafungwa huyo mwanadada anaweza kugauza sura wakati wa kula kiapo

  sijui nanihii atanikubali
   
 16. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  atiiii??!!!!sijakuelewa vizuri umemaanisha nini lango wa no entry??laaaahaulaaa
   
 17. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  si nikasahau jambo la msingi nililotaka kusema...nakutakia maisha mema ya Ndoa ndugu yangu na ujue kuanzia siku hiyo sio wewe tena hata katika yote ufanyayo juwa watakiwa ujali na mawazo na uwepo wa mwenzio!!
   
 18. N

  Nesindiso Sir JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2007
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 374
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kudadadeki!! Msanii una roho ngumu hadi umeamua kuoa??? Ok karibu kwenye club!.
   
 19. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2007
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Nakataa kata kata
  pole kwa mawazo hayo ilaa
  UKITAKA KUJUA UHONDO WA NGOMA INGIA UCHEZE.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...