Support ya msanii Soggy Doggy kwa wasanii kutoka jijini Mwanza

Feb 6, 2024
40
50
SUPPORT YA MSANII
SOGGY DOGGY ANTER KWA WASANII WA MUZIKI WA BONGO FLEVA MKOANI MWANZA..
____________________

✍🏾 Bila shaka jina la Msanii Anselm Tryphone Ngaiza a.k.a soggy doggy anter sio jina jipya masikioni mwa watu Hasa Kwa wadau na mashabiki wa Muziki wa Bongo fleva Nchini Tanzania...

✍🏾 Mchango wa soggy doggy Anter ndani ya Game ya Bongo fleva ni mkubwa mno..

Kirefu cha neno " Anter "

Ni
A-Anselm
N-Ngaiza
T-Tryphone
E-Evarist
R-Rumanyika

Harakati hizo zilipelekea kufanyika kwa mapinduzi makubwa sana ya kimaendeleo Mkoa wa Mwanza Baada ya Msanii huyo kuamia mkoani Humo akitokea jijini Dar es salaam...

🔥🔥🔥🔥🔥🔥

"KUNDI LA MUZIKI LA "B.W.V" ( BOYS WITH VOICE ) NA SOGGY DOGGY ANTER AMBAYE NDIYE ALIYEKUWA MTUNZI WA NYIMBO ZA KUNDI HILO.
______________

✍🏾 Kama waijua vyema Historia ya Muziki wa Bongo fleva Mkoa wa Mwanza

Utakuwa una wafahamu Vijana Hawa, vijana Ambao walijikita zaidi katika Masuala Ya Burudani..

1.jontwa jokeli
2. Jose kashushura.
3. Phantom lanks
4. Shija rweymam
5. Jingo man
6. Jet man
7. Jita man
8. Kind bway
9. Dk. Kb

Lakini pia kilikuwepo kizazi kingine cha millennium mkoani Mwanza kwenye upande wa Muziki wa Rap ( HIP HOP )..

Ambao wao walivuka mipaka mapema nakwenda Ng'ambo ya pili ( hapa na maanisha mkoani Dar es salaam walikwenda kutafuta ridhiki mkoani humo kupitia Sana'a ya muziki )

Na wengine Wengi walikuwa wanatisha sana hasa likija suala la utoaji Burudani ya Muziki Kwa upande wa wasanii wanaotokea mkoani Mwanza bila kusahau kundi la " B.W.V" (BOYS WITH VOICE).

B.W.V au BOYS WITH VOICE Lilikuwa ni kundi LA muziki kutoka Mkoani Mwanza .

Kundi lililoundwa na wasanii wawili Philbert kabago na Hamad salehe , kundi hili lilipata umaarufu mkubwa sana kupitia Album yao iliyotoka Mwaka 2003.

Album ambayo ilikuwa ikizungumzia changamoto mbalimbali za kijamii . lakini kubwa zaidi ni Mwanza kuitwa jiji ile hali miundombinu ikiwa bado ni mibovu Kwa mahandaki na Tope kibao . tunashukuru Mungu Barabara zilirekebishwa na sasa Barabara za mkoani Mwanza ni full mkeka tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma...

🔥🔥🔥🔥🔥

Kubwa zaidi wapenzi na mashabiki wa Muziki wa Bongo fleva ningependa kuwapa Taarifa kwamba mtunzi wa Baadhi ya nyimbo za kundi la " B.W.V" ( BOYS WITH VOICE)

Alikuwa ni Msanii soggy doggy anter.

Soggy doggy anter aliwaandikia nyimbo Baadhi nazo ni kama ifuatavyo :-

1. Bosss nipe mshahara Wangu " Boys with voice wakiwa wamemshikisha Msanii Maua ( Msanii wa nyimbo za asili kutoka mkoani kagera , Msanii ambaye alipata umaarufu kupitia nyimbo yake ya kihaya ikijulikana Kwa jina la " akatambala ")

Nyimbo hii ya " BOSS NIPE MSHAHARA WANGU " ili wataka / kuwakumbusha ma boss kuwalipa mshahara wafanyakazi wao Kwa wakati sahihi..

2.barabara zimerekebishwa

"Nyimbo ambayo walitoa maalumu
ili Kutoa shukurani kwa serikali baada ya marekebisho ya miundombinu ya Barabara kukamilika ..

3. Mzee mchana, usiku kijana

" Nyimbo ambayo ilikuwa ikizungumzia mwenendo mbaya wa kitambia wa mzeee mmoja katika jamiii .

4. Barabara zirekebishwe ft miss sarah.

Miss Sarah
Mwana Dada ambaye alipata umaarufu mkubwa sana kupitia kushirikishwa katika nyimbo na Msanii mwenzie Caz tee. Lakini hasa ni katika wimbo "nakuhitaji"

Nyimbo zote hizi mtunzi alikuwa ni soggy doggy baada ya kuingia jijini Mwanza na kukutana na changamoto zinazoikabili Jamii.

Sogggy Doggy:

Nilipopata kazi RFA nilimshawishi Enrico ahamie Mwanza na ikawa

Producer Enrico alikaa Mwanza kama miezi 6 au mwaka hivi kama sikosei . Baadae Alimua kuondoka jijini Mwanza Kwa sababu wasanii wengi walikuwa hawawezi kulipa gharama za studio

Wasanii kama FID Q Alisepa dar es Salaam, mapema sana , ujue Fid Q , Farida, Hardmad ni wasanii wa mwanza lakini walihit kutokea dar tofauti na Hawa "BWV" ( BOYS WITH VOICE )
harakati Nyingi za Muziki walifanya wakiwa nyumbani" mwanza.

Wasanii wengi wa Mwanza niliwasaidia kwa kugonga ngoma zao kwenye show zangu pale RFA ( enzi hizo nikiwa Bado ni radio prisenter radio free africa ) lakini pia na concerts nilizokuwa naandaa niliwapa nafasi katika jukwaa.Ila Kwa kifupi Wasanii wengi wa Mwanza walikuwa wana sana..

Lakin Kwa Bahati mbaya mmoja wa member wa kundi la " boys with voice "

Msanii " Salehe Hamad " alizaliwa maeno ya nyakalilo wilayani sengerema June 23 1982 na Alitangulia mbele za haki December 13 Mwaka 2010.

Lakini safari yake ya Maisha katika Muziki ilianzia katika shule ya msingi " Victoria internation " akiwa na umri wa miaka 14.

Salehe hamad aliacha mke na mtoto mmoja wa kiume.

Safari Swaiba ake Philbert kabago haikuwa rahisi katika Game ya Bongo fleva Baada ya kumpoteza rafiki yake kipenzi " Salehe Hamad " ..

Ambaye walikuwa wakiunda kundi moja " boys with voice "

Na kuamau kusimama kama solo na kubahatika kutoa wimbo wake mwenyewe nje ya kundi, wimbo uliojulikana Kwa jina la " wivu " Akiwa amemshirikisha Mwana Dada farida.

Farida nae alikuwa ana nyimbo kadaa zilizompa umaarufu
Kazi nyingi zikiwa chini ya usimamizi wa kidbway studio za Tetemesha Mwanza ..

1. Oh ! Pesa org. Akiwa pekeake

2. Oh ! Pesa rmx . akiwa amemshirikisha Mkoloni kutoka kundi la " wagosi wa kaya " .. Kundi la muziki kutoka Mkoa " Tanga "

3. Upendo wa Mama

4. Honey akiwa amemshirikisha fid Q .

Collabo
________

1. Roho 7 ft farida - crazy

2. Yaki ft farida - wangu

3. Joe Makini ft farida - sintokuacha

Wasanii Wengine kutokea Mkoani Mwanza ni

1. Coyo

" huyu jamaa ana hit song kama mbili hivi moja inaitwa njoo badae.

2. Mchama the best

" mchama the best huyu dogo alisumbua sana fiesta ilikua mwaka 2016.

3. Barada Da price

" baraka the prince huyu ndo alianza vizuri sana anavokuja na siachani nawe 2015.

4. Gheto ambassador

" Ghetto ambassador kwa wale wapenda harakati huyu jamaa watakua wanamfahamu alikua kundi la TAMADUNI MUZIKI tangia 2011 mpaka kundi lilipovunjika 2015.

5 . Cool James a.k.a Mtoto wa
Dandu(R.I.P).

6. Dudubaya

7 . H .baba.

8. Rado

9. PNC

10. Young killer

11. Dataz

12. Sajina

13. Mo music

(Picha na 1 )

"Ni marehemu Hamad salehe " B.W.V" ( BOYS WITH VOICE ), kwenye Uzinduzi wa Album yao .

KATIKA KIWANJA CHA CCM KIRUMBA MWANZA SEPTEMBER 14 MWAKA 2003 . TAMASHA LILILOANDALIWA NA " ZIZOU FASHION ( TIPPO ) .

KWA NYUMA ANAONEKANA H. BABA ENZI HIZO AKIWA BADO NI DENSA .

( picha no. 2 )

Kuanzia kushoto "chini"

Ni Msanii Bavoni, Ay & Philbert kabago.

Waliosimama kuanzia kushoto ni.

Hamad salehe , Dk. Life & saimoni sayi " complex "
..🎤🎤🎤🎤

( picha no. 3)

" katika studio za Mwanza records " Kwa Producer Enrico Fegwerado ,

Kutoka kushoto ni Msanii Soggy doggy anter , Philbert kabago & sister p a.k.a snaper ama chemical..
" pale kati"
 

Attachments

  • FB_IMG_1709975895987.jpg
    FB_IMG_1709975895987.jpg
    11.1 KB · Views: 7
  • FB_IMG_1709975888042.jpg
    FB_IMG_1709975888042.jpg
    19.2 KB · Views: 5
  • FB_IMG_1709975881233.jpg
    FB_IMG_1709975881233.jpg
    18.7 KB · Views: 5
Umeandika vitu vizuri, Ila mtiririko ilikuwa mhovu.
Anyway umenikumbusha mbali sana enzi hizo nikuwa sekondari nilipenda kusikiliza sana wimbo wa Soggy Doggy wa Asu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom