Penzi la mwana wa Bosi

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
PENZI LA MWANA WA BOSI
1

Nipomaliza la saba, litorokea mjini,
Mguuni nina raba, na kibegi mgongoni,
Nauli ninayo haba, nimeweka mfukoni,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

2

Gari zuri tukapanda, kuelekea mjini,
Shauku ilinipanda, kuondoka kijijini,
Nauli nikailinda, nisiibiwe mjini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

3

Hatimaye tukafika, usiku huko mjini,
Hofu mie linishika, kiwa pale stendini,
Kule sikuwa na kaka, wala ndugu wa mjini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

4

Niliishi stendini, karibia wiki zima,
Ni siku moja jioni, akaja mama mzima,
Shida nikamwelezeni, kanionea huruma,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

5

Kwake akanipeleka, gari lake zuri Sana,
Lipofika tukashuka, getini pakaachana,
Wandani walishituka, nguo zangu paukana,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

6

Yule mama sasa bosi, kazi amenipangia,
Kazi kushika mikasi, kusawazisha maua,
Kuni nakata vipisi, jikoni navitupia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

7

Bosi na mabinti tatu, kiume hakujaliwa,
Mkubwa aitwa Atu, sura nzuri amepewa,
Avaa virefu vyatu, vinang'aa kwenye juwa,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

8

Kwa bosi pale nyumbani, bosi mtu wa safari,
Na mwaka jana mwishoni, alisafiri safari,
Atu nami libakini, nyumba tulinde vizuri,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

9

Toka kiwa kijijini, mapenzi kwangu ni Shari,
Sijawahi lifanyeni, natoboa hii Siri,
Atu kanizindueni, kuvunja hiyo amri ,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

10

Nakumbuka siku moja, Atu likuja chumbani,
Kwangu likuwa kioja, usiku meingieni,
Amevaa kanga moja, imemchora mwilini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

11

Atu nikamuuliza, kwanini aje chumbani,
Akadai hatoweza, amepandwa na majini,
Mambo mengi linijuza, moja ni kuhusu chini,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

12

Pasipo kutarajia, kanga kule litupia,
Chuchu nikajionea, zimesimama sawia,
Akili ikazubaa, macho kodo nakodoa,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

13

Mhogo litutumuka, sijui umeanzia,
Atu nikamrukia, mwili nikiukagua,
Mwili wote melegea, sina budi kujilia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

14

Nilimwendesha kwa kasi, karibia nusu saa,
Nikatupia risasi, ndani mule naachia,
Kweli nilikuwa fisi, minofu menitupia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

15

kawa sasa desturi, Atu wangu nami wake,
Akinipa penzi heri, liloshiba Kama suke,
Atu nimembikri, kwangu ni wa kwanza mke,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

16

Bosi aliporejea, chochote hakugundua,
Sisi tukiendelea, dabwada kifurahia,
Tunda nikimung'unyua, usiku tukiibia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

17

Mwaka ulipotimia, Atu mejinenepea,
Mimba kwangu amekwaa, mamaye limfokea,
Nani mimba memtia, jibu akitarajia,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

18

Bosi wangu lipojua, kuwa Mimi na hatia,
Bastola lichukua, risasi akafyatua,
Kichwani nikaumia, damu zikijitokea,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

19

Nilikurupuka Sana, ukuta nikarukia,
Atu nikampa lana, ovuni amenitia,
Liingia mtaani, maisha kipigania,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

20

Atu tulipotezana, kwa sasa tisa miaka,
Namshukuru Rabana, nami nimetajirika,
Naishi vizuri Sana, hapa mjini mefika,
Penzi la mwana wa bosi, menitia matatani.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa Mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi TANZANIA 23/2/2022

1710781135551.jpg
 
Pole bwana Jerremia, Dennis mwakitumbuka,
Iweje we kuumia, siyo kichwa kufumuka?!
Risasi kuizuia, we una roho.ya paka??
Kwamba tunda ulikula, hiyo ni kimasikhara!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom