Leokweli,
Binafsi sii mtu wa upande wa kushoto na sipendi kabisa mbinu zao ktk maendeleo ya mtu maskini kwani siku zote tunawajaza matapeli nchini.. Strong leadership kwa nchi maskini hutokana na msimamo unaowekeza kwa wananchi wake kuunda jamii ambayo itaendesha uchumi wetu kwa karne zijazo na sii kutegemea wageni wasiweza hata kupata uraia wa nchi mbili..meaning at one point ni lazima wajikate!
Ukisoma kwa makini mawazo ya Jasusi ni mawazo ya kila Conservative, kwamba siku zote kizuri hujiuza na mwanamke anayejipenda mara nyingi hupata wachumba lakini sio umalaya kama huu unaofanyika.
Na siamini kabisa kazi ya rais kutembea na wafanyabiashara kwa sababu rais ni mtu anakwenda kufunga mkataba wa kibiashara na kukaribisha uwekezaji ktk sekta ambazo ni muhimu kwetu ktk kupata soko la nje..
Mara nyingi tunasahau kwamba Wageni wanapokuwa nchini iwe Saudia kulima mpunga nchini kinachohesabika ni kwamba mchele huo ni made in Tanzania na tunasafirisha nje.. Kodi yetu haiwezi kubadilika kama atakuwa Mtanzania au Mgeni na uwezo wa serikali kukusanya zaidi utatokana na soko tutakalo pata nje..Lakini kama Watanzania wenyewe wana uwezo wa kulima na kinachowashinda ni zana za kilimo nashindwa kabisa kuelewa kwa nini serikali ipo radhi kununua mashangingi na misafara kama hii kutafuta waarabu kuja kulima mpunga ktk eneo ambalo sisi wenyewe tunaweza kabisa kulima na kutosheleza soko la Saudia..
Kwa nini JK asiweke mkataba na Saudia ktk ununuzi wa mchele toka Tanzania na sisi tukajipanga kuweza ku supply demand yao!..Navyofahamu mimi ktk ubepari viongozi wa nchi huweka mikataba kama hakika ya mwanzo ya mauzo ushirikiano wa Kibiashara na sio kutembea na wafanyabiashara wadogo wanaotembea na sample mikononi kutafuta soko nje..Kwa mfano Prime minister wetu alikwenda UK, China na US kuweka mkataba wa kuuza mbao zetu huko jambo ambalo limekuwa likipigwa vita sana na wananchi wa nchi hizo..Lakini sikuona Priminister wetu akiandamana na wanamisitu au wwenyeji kujipanga na wanunuzi ktk zikao vyote.. Prime Minister alijua uwezo wetu ktk kusupply na wao walijua ni kiasi gani cha mbao zetu wanazihitaji ukiondoa supplier wengine..
Hivyo kazi inabakia kwa wakulima (wanamisitu) kuweza kuzalisha kiwango kinachotakiwa na kama ikitokea wamezalisha Zaidi au Pungufu serikali huwapa wakulima subsidy kutokana na hesabu zinavyo fahamika lakini sii kwetu..
Zamani enzi za mwalimu Tanzania ilijulikana duniani kwa mass production ya Sisal, Cotton, Coffee beans, Korosho na kadhalika hivyo hapakuwa na haja kabisa yetu sisi kujitangaza isipokuwa tulipeleka mali zetu sokoni. Utamaduni huo ulikufa baada tu ya Ujamaa kufa na hasa pale bei za bidhaa hizo ilipoporomoka.. Leo hii hatuna bidhaa yoyote ambayo tunaweza kujivunia au kuitangaza nje.. na sidhani kama JK anaweza kutafuta soko la kitu chochote wakati hana uhakika wa uzalishaji wake nchini.
Mimi nashindwa kuelewa kwa nini tumeacha Kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wetu. Sioni ndani kabisa kama alivyosema Jasusi..Unless Muungwana anataka kunambia hata kufua umeme, kusambaza gas yetu tunahitaji msaada au mwekezaji toka nje. Ni kitu gani hasa anacho shop nashindwa kuelewa kwani hao kina Johnson ni wababishaji tu biashara zao za Kariakoo - zinafanyika South East ya miji mingi ya US..
Til now, can't stop wondering kuna kitu gani ambacho sikifahamu kitatokana na misafara hii!..