Wakuu kuna kitu kimoja ambacho hadi leo sijaelewa na ndio maana nashindwa sana kumlaumu Kikwete na hizi safari zake..Sielewi malengo yake lakini kama kweli anajaribu kuiuza Tanzania basi bila shaka hakuna njia nzuri kama rais wetu kuwafuata makwao hawa jamaa kwa sababu hatuwezi kujiuza kama wenzetu nchi za Asia..
Nasema hivi kwa sababu navyofahamu mimi Mataifa makubwa na all big corporates hawawezi hata siku moja kuingia ktk Tender za nchi maskini hasa tunapotaka kuuza mali au kutafuta wawekezaji. Tender zetu zote toka wakati wa Mkapa zimechukuliwa na mashirika mbuzi mashirika ya kifisadi vile vile kwa sababu mara nyingi uwekezaji inatakiwa nchi host ndio ijitangaze inacho offer badala ya haya mashirika kutuma maombi.
Tanzania bado kabisa haijafikia uwezo wa kujitangaza na masirika au mataifa makubwa kugombea nafasi za uwekezaji nchini isipokuwa tunatakiwa sisi kujitangaza kwao. Na ukweli utauona ktk mashirika yote ya Umma tuliyowahi kuuza.. tumewauzia matapeli, mashiurika yasiyokuwa na record ya kazi hizo zaidi ya tungo za resume ili kupita ktk Mchekecho wa Tender.
Hata siku moja huwezi kuwaona Amtrak wakiomba kuendesha reli yetu, Hata siku moja huwezi kuwaona Bell wakijipanga ktk tender za kusambaza nyaya za simu na mawasiliano nchi maskini. Hata siku moja huwezi kuona Intel au AMD wakifikiria kuwekeza Tanzania kutengeneza PC hardware pamoja na kwamba raw za vifaa vingi zinapatikana Afrika..
Ni muhimu sana sisi Watanzania kusoma wakati, kufahamu tamaduni ya biashara ya nchi hizi.. lazima tujitangaze na tuwe mbele kutoa offer kwao kwani hawa jamaa ni kama wahindi.. Mke ndiye hutafuta mchumba na kutoa mahalai sii sawa na utamaduni wetu ambao kila siku tunatangaza tender ktk magazeti na wanaokuja kutuchumbia ni mfano wetu.. Matapeli!
Hivyo nafanya subira, sidhani kama Kikwete ni mjinga kiasi hicho cha U Vasco tuuu kivinjari dunia..Naomba Mungu isiwe hivyo, ila uwe ni mtazamo mpya wa kutafuta wawekezaji kutokana na imani ya wana CCM - Progressive. Siupendi mfumo huu na sintapendelea nchi yetu kuuzwa kwa wageni lakini sina budi kukubali ndio mbinu bora za wana Progressive kuvuta wawekezaji wenye uwezo mkubwa na kwamba naelewa nini malengo ya misafara hii badala ya kumlaumu Kikwete. Pengine yawezekana miaka mitano ijayo tutaweza kuona matunda ya kukoloniwa, ndipo tutakapo shika adabu na kuelewa tofauti ya mirengo hii.