Kikwete for London Family Planning summit

Kikwete for London Family Planning summit

President Jakaya Mrisho Kikwete is received at the Regency Hyatt Churchhill hotel in London today July 10, 2012 ready to attend a two-day a ground breaking International Family Planning Summit. The Summit is scheduled to launch a Global Movement to give an additional 120 million women in the World’s poorest countries, access to lifesaving family planning information, services and supplies by 2020.

The United Kingdom’s Government and the Bill & Melinda Gates Foundation, with the support of UNFPA and other partners, are hosting the summit, whose envisaged increased access will enable these women and girls to choose whether, when and how many children to have.

This Summit is a collective opportunity to generate global commitments to increase access to family planning and, in doing so, accelerate the achievement of MDGs 4 (reducing child mortality) and 5 (improving maternal health) – including MDG target 5b (reproductive health) – as well as MDG target 6a (HIV prevention).

It will build on the momentum created by the UN Secretary General's Global Strategy for Women's and Children's Health, “Every Woman, Every Child”, and the innovative public-private and civil society partnerships that are developing through the Reproductive Health Supplies Coalition (RHSC) and their Hand to Hand Campaign.

Leaders from developing and developed countries, donors, civil society groups and the private sector will come together behind a simple vision: to give women in the developing world the same access to lifesaving family planning as women in the developed world.

PHOTO BY STATE HOUSE

TUESDAY, JULY 10, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG ~ MTUMIE RAFIKI YAKO , MAONI: 0
 
JK ana watoto 7 mpango wa uzazi haumhusu!atatueleza nini juu ya kupanga uzazi!bora hata mkapa maana anao 2 wakufikia
 
Kwa kweli safari hii ilimfaa sana waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto
 
huyu dhaifu alipaswa kuwa afisa utamaduni kijijini kwetu Gamboshi..
 
tusubiri tuambiwe kwanza ni kwanini ameenda kwenye mkutano huo kabla ya kushambulia, huenda kuna marais wengi wanakwenda huko na huenda ni mkutano muhimu sana, so we better wait and see.
 
Hivi JK ni waziri wa afya au ni raisi wa nchi?......mbona huwa anadandia kazi za wizara zote......mara aende jamaica kujifunza kilimo cha mihogo......mara yuko marekani kupiga picha na boys to men khaaa.....hao mawaziri aliowateua huwa wanafanya kazi gani?
 
Posho za nje hajapata muda mrefu. Watakapoanza kumuuliza maswali kuhusu ulimboka na Meli za Iran kuvikwa bendera ya TZ atatia adabu. Hapo ameenda kupima kama je viongozi wa nje bado wanamheshimu au wamegundua utumbo anaofanya nyumbani
 
Ndio rais wetu huyu, Sijui ile timu ya ushauri pale magogoni inafanya nini! Sidhani kama kila mkutano raisi anatakiwa aende, vikao kama hivi alitakiwa amtume waziri wa afya anatosha kabisa
Huyo ndio Mkulu..Unajua kuna makabila au jamii hapa Tanzania ni malimbukeni wa kupitiliza. Moja ya hayo makabila ni huko alikotokea Mkulu. Safari za nje ya nchi kwa Mkulu ni UJIKO sana huko kwao na anaonekana ana akili na maarifa sana ndio maana anasafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo.

Siku moja nilikuwa nanyoa nywele sehemu akaja Mzee mmoja kunyoa,akawa anamuelezea kinyozi wake kuhusu Canada na jinsi kulivyo dunia nyingine. Out of curiosity nikamuuliza Kama anaishi huko! Akanijibu hapana alienda kikazi kwa Wiki moja....Aisee nilichoka kabisaaaa. Ulimbukeni ni janga la kitaifa Jamani. Mkulu anasumbuliwa na ULIMBUKENI Syndrome.
 
Rais Kiwete amedhihirisha udhaifu wake kwa mara nyingine tena baada ya kuondoka juzi kuelekea London,Uingereza eti kuhudhuria mkutano unaohusiana na Mpango wa uzazi duniani. Sioni mantiki ya Rais kuwa anasafiri kila siku kwenda nje ya nchi ilhali hapa nyumbani kuna matatizo chungu nzima na changamoto zinazohitaji maamuzi na ushauri wa rais!

Mara kwa mara Watanzania wamekuwa wakilalamikia safari za Rais nje ya nchi ambazo aghalabu hazina tija kwa nchi yetu. Rais Kiwete tangu aingie madarakani amekuwa akishtumiwa kwa safari za mara kwa mara ambazo Rais huandamana na ujumbe wa watu wengi na hivyo basi kuliingiza taifa kwenye gharama kubwa za mabilioni ambayo ni fedha ya walipa kodi wa nchi hii.

Kwanini Rais Kiwete huwa hawezi kuchagua mwakilishi kwenye safari kama hizo? Tunajua kuna Waziri wa Mambo ya nje na kuna Mawaziri husika kwenye maeneo mbalimbali,k.m.afya,elimu,mawasiliano n.k. Safari kama hii ya London Kiwete alitakiwa amwachie Waziri wa Afya ili aiwakilishe Tanzania kwenye mkutano huu unaohusu mambo ya mpango wa uzazi na siyo Rais Kikwete kwenda huko. Hii ni aibu kwa Rais Kiwete na Serikali yake. Huyu tunaweza kumwita kuwa ni RAIS WA NCHI ZA NJE na siyo Rais wa Watanzania. Inasikitisha kuwa Rais badala ya kukaa Ikulu na kujaribu kutatua kero na changamoto zinazoikabili Serikali yake yeye amekuwa ni mtu wa kukwepa na kukimbia changa moto hizo kama vile migomo ya Wafanyakazi,hali ngumu za kiuchumi kwa wananchi na serikali na tishio la kuuawa kwa raia wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa!

Tumeshuhudia mara nyingi kunapotokea migomo au jambo baya la kitaifa Rais Kiwete kwanza yeye ndiyo anakimbilia nje ya nchi kama vile hana habari na matukio hayo. Kuna mifano kama ya Miripuko ya Mabomu ya Mbagala na Migomo ya Madaktari mara 2 mfululizo na wakti wote katika matukio haya Rais Kiwete aliamua kusafiri kwenda nje bila kukaa Ikulu na kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo. Hii maana yake nini? Jibu liko wazi kabisa kuwa Kiwete hawezi kuhimili migogoro ya kitaifa. Kwa maana nyingine ni kudhihirisha udhaifu wake! Hii ni sawa na kusema Baba nyumbani anapoona familia haina chakula,watoto wanaumwa, nyumba ya kulala inavuja basi anaamua kukimbilia mjini au kutokomea porini kusikojulikana ili kukwepa lawama. Huyo ni Baba dhaifu na ambaye hastahili kuitwa baba mwema hata kidogo.

Wito wangu kwa Rais Kikwete ni kwamba apunguze safari zake za nje maana hazina tija kwa Taifa na watanzania wote kwa ujumla wao. Safari ambazo hazina ulazima awapeleke mawaziri husika ili wamwakilishe na yeye akae Ikulu kutatua kero na matatizo ya Watanzania. Haiwezekani wewe ni baba nyumbani na una watoto wakubwa badala ya kuwatuma kwenda kwenye kazi mbalimbali za shamba,biashara au vikao vya kifamilia wewe baba unataka kila jambo ufanye mwenyewe. Hapo utaonekana ni baba mbambaishaji na ambaye umeshindwa kuisimamia nyumba na familia yako.

Nawasilisha.
 
Uenda kaenda kuwaombea watanzania msaada wa madaktari........Tusubiri atatuambia katika ngonjera zake za mwisho wa mwezi wa saba maana huwa hana hoja zaidi ya kutuambia hadithi zake za abunuasi
 
Absolutely NO NO NO, he should have asked his minister for health and social welfare to attend on his behalf. It is disgraceful for Mr. President to attend such a minute conference! hah hah hah perhaps gay marriage is another contemporary method of family planning Mr Kikwete, please discuss it with Mr. Cameron hah hah
 
Kuna viongozi wengine huwa wanaacha nchi na kukimbia ,inawezekaana ndio ameishatuwacha kwenye mataa!! Huwezi kujua !
 
Akiulizwa atajibu "SIDHANI KAMA KULIKUA NA ULAZIMA KIUTENDAJI ILA KWA UTALII WA NJE ILINIBIDI NIENDE".....
Vasco da Gama in another discovery....
 
Back
Top Bottom