Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Sarkozy’s jogging collapse shoots up his popularity by 12 pc

Ani
August 6th, 2009

LONDON - French President Nicolas Sarkozy’s recent jogging collapse has shot up his popularity by 12pct.

The first opinion poll since his heath scare has shown a 12 per cent increase in those who think that the 54-year-old politician is succeeding as head of state.

The survey revealed that overall 53 per cent of the French people believe Sarkozy makes “a good president”, in contrast with 41 per cent in May, reports the Telegraph.

However, just 38 per cent think the opposite, compared to 55 per cent three months ago.

The CSA poll for the Paris magazine VSD also revealed that 90 per cent of respondents believe that Sarkozy is still “dynamic”, compared to 85 per cent in May.

And 80 per cent consider him “courageous”.

Nearly 50 per cent of the respondents now consider Sarkozy “close” to the French people.

http://blog.taragana.com/n/sarkozys-jogging-collapse-shoots-up-his-popularity-by-12-pc-132466/

Ona sasa,

Unaleta habari kuwa Sarkozy ameanguka akifanya mazoezi na wala sio kuanguka tu akihutubia kama Kikwete. Ungekuwa fair kama ungemlinganisha Kikwete na Castro wa Cuba ambaye alianguka baada ya kuhutubia kwa masaa matatu na ushee (si unajua tena kama ile hotuba ya kikwete kwa kamati kuu iliyochukua nadhani siku nzima .....LoL)
 
malizia kuwa raisi gani asiye na waganga wa kienyeji (au wachawi)? Na utapata jibu zuri sana hapo.
nitamalizia vipi ukiwa unafuta posts zangu.bora nikuache useme/uandike unavyotaka nilijua nabishana na ordinary member wa jf kumbe wewe sikuwezi.
 
Kanda2 thanks kwa taarifa.

Wengi hapa hawakutaka hata kuhoji uhakika wa mleta habari...kwani ukiweza kusoma michango ya watu utajua wengi wamefurahia...the so called kuanguka kwa JK....Wengine wamekwenda mbali za zaid ya kutaka JK "afe" ....Kufa ni Jambo ambalo kila mwanadam mwenye akili Timam anafikiria kuwa ipo siku atakufa.sababu na wakati na mahali ni vitu ambavyo vipo nje ya Uwezo wa kufikiri wa Binadamu....

Haya ni mawazo yako tu yaliyopotoka. Watu wamempa ushauri Kikwete akatibiwe na wala asiogope matibabu kwa manufaa ya nchi na serikali yake.

Mwafrika..Jaribu kuwa mkweli...wahudumu wa Kike ktk Ndege wanafanya nini ktk Ndege...au wafikiri watu wote ni wajinga kama wewe...?Hata kama mtu kweli ni mpenzi wa Vimwana..upuuzi unaoufikiria hawawezi fanya ktk Ndege...!!!

Hiyo ni probable scenario inayoweza kuwa imesababisha mkulu wa nchi asipate usingizi kwenye ndege. Hayo mengine ni maneno yako tu kama kawaida yako.

Kwa Ujinga wako Hujui maana ya Madrasa...ni shule kama shule zingine...


Ninarudia tena kuwa Kanda2 apunguze muda madrasa na ushauri wangu bado ni wa bure tu kwake.


..Sijui umekusudia nini Kuhusu Aljazeera...kama ni chombo cha Habari nafikiri wewe upo mbali sana na Dunia ya Ukweli...Mshauri Mzee Mengi basi avunje partnership na Aljazeera!!!

Hata wewe unaweza kumshauri Mengi kuvunja hiyo partnership ila kwa sasa ushauri wangu kwa kanda2 ni kuwa - apunguze muda wa kuangalia suicide bombings za al jazeera na atumie muda kutazama TV zingine- mf Jerusalem news (ha h aha ha).
 
Last edited:
Endelea kujidanganya...na kuwadanga mabwe_ge wenzio...Maana Eti Rais asilale kisa Mabinti wa ktk ndege...hahahaha...!!!

Sasa ni Kipi kinachokufanya uichukie Aljazeera Int...?

Kutibiwa Ukiwa Unaumwa its OK....Kama haumwi afanyeje...Mleta Mada kasema kaaanguka...wakati Hakuanguka..then What?..Endelea na wrong assumption zako...!!!
 
Nadhani wapambe wake JK wangekuwa wanatumia busara zaidi kusisitiza kuwa Mheshimiwa apimwe afya yake na kama ikitakiwa ang'atuke mapema kabla hajajisababaishia madhara makubwa. Hapana hakuna uongo wowote, Rais wetu ni mgonjwa tena sana, na hili tatizo lake la nerve lilikuwa linajulikana hata alipokuwa waziri wa mambo ya nje, na pia alishawahi ku-collapse.

Ushauri wangu kwa wapambe, do not bury your heads in the sand, but face the facts. Same advice for JK, call it quits and take off into the sunset with dignity and your health intact.

Hao wapambe wa JK wakimwambia ukweli ili a-quit unafikiri wenyewe watakula nini. Unajua wanafanya maduduz kwa mgongo wa JK. Akija prezidaa mwingine that means watafute vibarua vingine. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa anayeumia ni JK.
Utakuwa ni uamuzi wa busara jamaa kuachia siasa kwa sababu za kiafya, everyone will understand that. Bila ya kuwa na afya nzuri unawezaje kufanya kazi kwa ufasaha?
 
nitamalizia vipi ukiwa unafuta posts zangu.bora nikuache useme/uandike unavyotaka nilijua nabishana na ordinary member wa jf kumbe wewe sikuwezi.

Punguza basi vilio visivyo na mwisho. Ni lini utakua ili uanze kuandika bila kulia lia kama kitoto kichanga? Inaonekana hauko tayari kabisa kujitoa muhanga kwa kujilipua kama maisha ndiyo haya ya kulia lia.

Mimi sijawahi na sitawahi kufuta maandishi ya member yoyote hapa jamvini. Hiyo ni kazi ya mods na ya wamiliki wa JF. Kama hujagundua, maandishi yangu kibao tu yanafutwa hapa na au kuhamishwa ila huwezi kuniona nikilia lia kaa kitoto kichanga.
 
Endelea kujidanganya...na kuwadanga mabwe_ge wenzio...Maana Eti Rais asilale kisa Mabinti wa ktk ndege...hahahaha...!!!

Hao hapo ni pamoja na wewe? Hilo la Raisi kutolala muulize pacha wako kanda2 aliyedai kuwa Kikwete alichoka baada ya kusafiri kwa masaa 19 toka marekani.

Sasa ni Kipi kinachokufanya uichukie Aljazeera Int...?

Kushabikia suicide bombers - si unajua wale mujahidini waoga wasioingia jeshini ili kupambana bali wanakimbilia kujiua wenyewe kwenye mabasi yaliyojaa wanawake, wazee na watoto.

Kutibiwa Ukiwa Unaumwa its OK....Kama haumwi afanyeje...Mleta Mada kasema kaaanguka...wakati Hakuanguka..then What?..Endelea na wrong assumption zako...!!!

Hakuna sehemu yoyote mleta mada amesema kuwa Kikwete kaanguka. Hizo ni fantasy zako tu mkuu.
 
Unaleta habari kuwa Sarkozy ameanguka akifanya mazoezi na wala sio kuanguka tu akihutubia kama Kikwete. Ungekuwa fair kama ungemlinganisha Kikwete na Castro wa Cuba ambaye alianguka baada ya kuhutubia kwa masaa matatu na ushee


Mwafrika,

Castro alianguka baada ya kupigwa kichwa na Zidane.

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=tAa1vDW2NGk[/ame]
 
Mbogela,

I have an immense interest in US presidents and their biographies and so far the only documented alcohol abuse issue that was clearly documented is that of President General Ulysses S. Grant (the one on the 50 dollar bill). Grant came to the White House after winning the Civil War, so you can imagine how long ago that was, he was the 18th President of the United States from 1869 to 1877.

There is no record of wifebeating, maybe you may be able to educate us on this new piece of info, one never knows with the secret lives of US Presidents.

http://en.wikipedia.org/wiki/Ulysses_S._Grant
.

Asante mkuu, lakini naamini sio Rais wa zamani kiasi hicho ngoja nitaitafuta hii story, I am sure mkuu nimeioona sehemu. Siiamini sana wikipedia lakini kama hatuna authentic source mbadala basi hatuna budi kuitumia, lakini mkuu ngoja nifanye asignment upande wangu I will come back to you in case i get something tangible
 
jk hakuanguka mwanza alipumzika kwa dakika kadhaa.ubnaposema kila siku ni kukuza jambo na kuleta uongo.amesafiri kwa masaa kama 19 toka marekani akafika saa saba usiku.alfajiri akaenda arusha kwenye mkutano wa jumuiya ya madola.ataunganisha mwanza.lazima atazidiwa na uchovu.

kama kuanguka rais bush wa marekani alikuwa anaanguka na alifanya kazi term mbili.rais wa ufaransa nicolas sacorzy anaanguka mara kwa mara lakini anafanya kazi za urais .mwacheni jk yeye ni binadamu kama mimi na wewe.

pole jk tupo pamoja nawe na mwenyezi mungu atakulinda.

Mwandishi wa mwananchi communication anasimulia hivi

Rais Kikwete, ambaye alifika mkoani hapa akitokea Arusha ambako alifungua mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, ikiwa ni siku chache tangu atoke Marekani kuhudhuria mkutano wa Baraza la Umoja wa Mataifa, alikumbwa na mkasa huo majira ya saa 6:29 mchana.

Rais Kikwete alikatisha hotuba yake wakati akianza kuelezea suala la kudumisha amani upendo na mshikamano, akisema:"Wakati nilipokuwa nikipita kuomba ridhaa yenu kuongoza nchi hii, kote nilikopita niliomba kudumishwa kwa amani upendo na mshikamano…" Ghafla alinyamaza na baadaye ikasikika sauti kutoka kwenye kipaza sauti chake ambayo inaonekana kuwa ya mlinzi wake, iliyosema "Kakae". Baadaye Rais Kikwete aliuliza kwa sauti akisema "naweza kuhutubia nikiwa nimekaa"na kujibiwa na mwenyeji wake, Askoku Mkuu wa AICT, Daniel Nungwana kuwa "unaweza kukaa", jibu ambalo lilifanya aondoke kwenye eneo ambalo alikuwa akitumia kuhutubia jukwaani na kwenda kukaa meza kuu ambayo ilikuwa umbali wa takriban mita mbili.

Mara baada ya kukaa na vipaza sauti kurekebishwa ili aendelee na hotuba, Rais Kikwete alitamka kwa sauti ya juu iliyoonyesha kuwa afya yake si nzuri wakati alipoeleza kuwa “nimechoka sana kwa sababu ya safari” na kisha kuendelea na hotuba yake, lakini sauti yake ilizidi kubadilika na kuwa inayokwaruza na akakatisha hotuba yake, akiacha waumini wakinong’ona.

Baadaye Rais Kikwete, ambaye aliwahi kupoteza nguvu jukwaani wakati akihitimisha kampeni zake za uchaguzi kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam,
alinyamaza na kutulia huku akiwa anaangalia upande wa mashariki, shingo yake ikilalia bega la kushoto na kichwa kuegemea kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro.

Dakika chache baadaye (saa 6: 35), mlinzi wake ambaye alisimama nyuma ya kiti chake, alimtikisa kwa muda, lakini rais hakuonekana kujibu kitu na ndipo walinzi wake na maofisa wengine wa usalama walipomzunguka kumkinga kuzuia watu wasimuone na baadaye kumbeba juu na kumpeleka kwenye chumba maalumu kilicho eneo la jukwaa kubwa la Uwanja wa CCM Kirumba.

Wakati akiingizwa chumbani humo, magari yote ya msafara wake yalielekea nje ya uwanja huo na kuegeshwa nje ambako kuna mlango, jambo lililoashiria kuwa iwapo afya yake isingetengemaa, angetolewa kupitia mlango huo na kukimbizwa hospitali.

Wakati harakati hizo zikiendelea, Kandoro alirejea jukwaani na kuelekea kwenye kipaza sauti. Kandoro aliwataka wananchi kutulia kwa maelezo kuwa hali ya rais ni nzuri na kwamba amepumzika kwa muda kutokana na uchovu.

"Nawaomba mtulie, Rais wetu amepumzika tu kwa muda kutokana na uchovu wa safari na yuko salama. Nawahakikishia kuwa yuko salama na huu ni uchovu tu kwani amesafiri sana kutoka nje ya nchi hadi Arusha na baadaye kuja hapa Mwanza. Hivi sasa amepumzika na atarudi hapa," alieleza Kandoro.

Kikwete alirejea jukwaani majira ya saa 6: 45 akitembea bila ya msaada wa walinzi ambao walikuwa nyuma yake na kwenda kukaa kwenye meza kuu ambako aliomba kipaza sauti na kusema maneno machache. "Ndugu wachungaji na waumini, nguvu imerudi; nataka kutumia fursa hii kuzindua mfuko wenu maalumu; nami nachangia shilingi milioni moja,"alisema Kikwete na kuamsha kelele za shangwe na vigelegele.

Baadaye ratiba ya sherehe hizo iliendelea kwa harambee ya kuchangia mfuko maalumu wa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao aliombwa na Askofu Nungwana kuchangia kwa kuuzindua kabla ya hotuba yake. Askofu Musa Mwagwesela aliwatangazia wananchi kuwataka wajitokeze kuchangia mfuko huo kwa kipindi cha dakika tano, ili wamruhusu rais aondoke uwanjani hapo. Alisema ameombwa kufanya hivyo na watu wa usalama.

Zoezi hilo la wananchi na watu mbalimbali kuchangia mfuko huo liliendelea na majira ya
saa 7:08 mchana Rais Kikwete aliombwa na mwenyeji wake Askofu Daniel Nungwana kuwashukuru wananchi kabla ya kuondoka. Aliposimama Rais Kikwete alisema: "Kwanza nawaombeni radhi kwa mshtuko niliopata. Lakini umenitokea kwa ubishi wangu; ni kwa ajili ya uchovu wa safari."

Kikwete aliendelea kusema: "Nimerudi juzi saa 7:00 usiku. Nilikuwa Arusha kwenye mkutano wa bunge, walinishauri nipumzike nikasema ahaa hawa nao ngoja niende tu; waliniambia tunaona uchovu mwingi, nikasema hawa nao ahaa… nitaweza tu; nimekuja hapa… siku nyingine nitawasikiliza wanaonishauri."

Kabla ya kuzidiwa na kukatisha hotuba yake jana, Rais Kikwete alilipongeza kanisa hilo kwa kutimiza miaka 100 na kwa kutoa huduma mbalimbali katika sekta ya afya na elimu.

mchango wa mashirika ya dini na kusisitiza kuwa unapotaja maendeleo ya nchi hii, huwezi kukwepa mchango huu wa mashirika ya dini.

Hali haikuwa shwari kwa wananchi waliokuwa kwenye uwanja huo licha ya matangazo ya Kandoro kuwa afya ya rais ni nzuri. Kulikuwa na minong'ono mingi kutokana na kila mmoja kuuliza nini kimetokea kabla ya
Askofu Mussa Magwesela kuwaambia waumini kuanza maombi maalumu kumuombea rais kutokana na hali iliyomkumba ghafla. "Waumini wote naomba tumuombee mpendwa rais wetu; tumuombee Mungu amrejeshee afya yake,"alisema na mara moja waumini wakaanza maombi ya mmoja mmoja.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa baadaye na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ilidai kuwa Rais Kikwete alilazimika kupumzika kwa dakika chache "baada ya kumaliza hotuba yake” katika sherehe hizo kutokana na kuzidiwa na uchovu. "Nguvu imerudi…napenda sasa kuchukua nafasi hii kuzindua rasmi uchangiaji wa shughuli za kanisa lenu na mimi naanza na mchango wa Sh 1,000,000," taarifa hiyo ya Ikulu ilimkariri Rais Kikwete ikieleza kuwa baada y
a mapumziko mafupi alirejea na kuendelea kushiriki shughuli hiyo. Ilieleza kuwa Kikwete alianza kusikia uchovu wakati akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya waumini wa Kanisa hilo.

Taarifa hiyo inaeleza: "Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Oktoba 4, 2009, amelazimika kupumzika kwa dakika chache katika chumba cha mapumziko kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza mara tu baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa sherehe za miaka 100 tokea kuanzishwa kwa Kanisa la African Inland (AICT) nchini Tanzania.
"Mhe. Rais amelazimika kupumzika kutokana na kuzidiwa na uchovu kufuatia shughuli nyingi mfululizo katika siku za karibuni. Baada ya mapumziko hayo, Mhe. Rais aliendelea kushiriki katika shughuli hizo hadi mwisho wa shughuli hiyo ya AICT."

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kikwete alikiri kupata matatizo hayo, akisema kuwa yalitokana na kutofuata ushauri wa wasaidizi wake waliomtaka apumzike baada ya kurejea kutoka Marekani. Taarifa hiyo imeeleza kuwa washauri walimtaka asiende Arusha kufungua mkutano huo wa mabunge na baadaye kumzuia asiende Mwanza.

Taarifa hiyo ya Ikulu inasema: "Kwa kweli mshtuko huu wa leo ni
matokeo ya ubishi wangu. Nilishauriwa na wasaidizi wangu nipumzike baada ya kurejea nyumbani kutoka Marekani. Niliambiwa nisiende Arusha ama kuja hapa. Lakini nikakataa. Siku nyingine nitawasikiliza zaidi."
 
Wakati haya yanaendelea na blogosphere inazidi kuwaka moto...


RALVA RWEYEMAMU hajui namna ya kujibu mapigo na wameshindwa hata kufanya PR ya kumwonyesha rais yuko Gym au rais ana fanya jogging ili kuuzima huu moto

this doesnt look good na unless kuje kitu kingine kuondoa hii from the front pages
 
Mbogela.
HAKUNA SEHEMU INAELEZA KUWA ALIANGUKA.KUKAUKWA KWA SAUTI NI JAMBO LA KAWAIDA.NDIO MAANA WAKATI WA HOTUBA LAZIMA KUWE NA CHUPA YA MAJI KUZUIA MAMBO KAMA HAYA.
RAIS MUSAA YARDUA WA NIGERIA MARA NYINGI AMEKUWA AKIPATA HALI YA KUUGUA KIKAO CHA UN HAKUHUDHURIA ALIKUWA SAUDIA ARABIA AKITIBIWA.
 
Mbogela.
HAKUNA SEHEMU INAELEZA KUWA ALIANGUKA.KUKAUKWA KWA SAUTI NI JAMBO LA KAWAIDA.NDIO MAANA WAKATI WA HOTUBA LAZIMA KUWE NA CHUPA YA MAJI KUZUIA MAMBO KAMA HAYA.
RAIS MUSAA YARDUA WA NIGERIA MARA NYINGI AMEKUWA AKIPATA HALI YA KUUGUA KIKAO CHA UN HAKUHUDHURIA ALIKUWA SAUDIA ARABIA AKITIBIWA.
Kanda2,
Ile tu kwamba shingo ilielekea mashariki ina maana kwamba alilose body control for sometime. Angekuwa bado amesimama uwezekano ni mkubwa kwamba angeanguka.
 
Kikwete anaumwa, tena seriously.Watu hawataki kusema tu.

Hii incident wala ile ya 2005 si habari za uchovu wa safari

I support you 1000%.Tatizo letu Watanzania ni kukwepa kuita koleo ni koleo (calling a spade a spade).Na kingine ni kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.Hivi uchovu wa Kikwete (anayetembea kwa ndege huku akikohoa tu wapambe wanahaha kumtimizia) unaweza kulinganishwa na walalahoi wanadamkia mashambani na kukesha hadi machweo?Msiwatukane babu na bibi zetu,au baba na mama zetu,au kaka na dada zetu,au wadogo na ndugu zetu wengine wanaoshinda juani kutwa nzima kutafuta ridhiki lakini wanarejea nyumbani na uchovu wao huku wakiwa hawana uhakika kesho watakula nini!

Huyu mtu mgonjwa,lakini kwa vile katika tawala za kiimla kusema rais mgonjwa ni sawa na kosa la uhaini basi tunakimbilia majibu rahisi ya uchovu.Dr Slaa hachoki katika mapambano yake dhidi ya mafisadi?Mbona hajaanguka jukwaani mara 2?Vipi kuhusu wamachinga wanaokesha juani kutwa nzima?Kikwete hajakulia mazingira ambayo ukizunguka na ndege mara 2-3 basi uchovu unakuzidia hadi aanguke jukwaani.

I repeat,huyu mgonjwa,na wengi tunajua hilo lakini kwa vile kusema kiongozi mgonjwa ni sawa na kuvunja katiba,basi tutakubali kuwa KACHOKA,which brings us to another important point kwamba KIONGOZI MCHOVU HATUFAI especially as tumeshika nafasi ya 150+ kwenye human development report ya 2009.

He should go before it''s too late.
 
Mbogela.
HAKUNA SEHEMU INAELEZA KUWA ALIANGUKA.KUKAUKWA KWA SAUTI NI JAMBO LA KAWAIDA.NDIO MAANA WAKATI WA HOTUBA LAZIMA KUWE NA CHUPA YA MAJI KUZUIA MAMBO KAMA HAYA.
RAIS MUSAA YARDUA WA NIGERIA MARA NYINGI AMEKUWA AKIPATA HALI YA KUUGUA KIKAO CHA UN HAKUHUDHURIA ALIKUWA SAUDIA ARABIA AKITIBIWA.

Kanda nakubalina na wewe nimeweka hicho kipande kukubaliana na wewe kuwa hakuanguka ila aliomba akae, kisha akakimbizwa chumba cha kupumzika, mpaka hapo tutasema kuwa alipumzika.

lakini sijaona picha zinazoonyesha
1. akitikiswa,
2. akiwa amezungukwa na wapambe,
3. amebebwa kupelekwa chumba cha kupumzika
4.anaporudi tena.

Inamaana mapaparazi wetu ni wale wa kusema semeni cheese ndio wapige picha??? Picha za hili tukio kama zingepigwa kwa utaalam na kwa ukaaribu mzuri tungeweza kuasses hata uso wake ulionekanaje na macho, midogo na hapo tungesema kitu. Wapiga picha mnapewa home matukio kama haya picha zenu zingemaliza ubishi
 
Back
Top Bottom