Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Jamani Someni Marko 9:19-25 mtaona jinsi mapepo wanavyo mwogopa Yesu.
 
i think watu wameikuza kupitiliza habari hii, nimeangalia habari asubuhi si kama watu wanvyotaka tuamini.hivi hatuwezi kutoa taarifa kama ilivyotokea hadi tuongezee na uongo?
Tupe ukweli...
 
Kazi ni kubwa .. Ni jana tu kakiri jinsi alivyo mbishi anaposhauriwa na watu.

Naamini kuwa wanamshauri sana amweke lupango RA na EL lakini yeye mbishi sasa naamini.
 
Naomba kupata maelezo ya mtu anaelewa madhara gani anaweza kuya pata kama angekubali/atakubali kwenda kufanyiwa upasuaji wa nerve oblangata kama Ndanda to Lomwe alivyo tueleza hapo chini na je kwenye jamii ataeleweka kama atagundulika/akifanyiwa upasuaji wa sehemu muhimu kama hiyo...nahisi maamuzi yake yatakuwa hayaaminiki vile maana atakuwa unfit...
Ni kweli muungwana ni mgonjwa anasumbuliwa na ninadhani ni tatizo la NERVE katika sehemu za medula oblangata kwa lugha ya kitaalam, na kwa taarifa nilizonazo baada ya kuanguka pale jangwani wakati anamalizia kampeni zake za Urais 2005 alipata kutibiwa na Daktari mmoja huko ufaransa na alishauri afanyiwe upasuaji lakini muungwana hakukubaliana na hilo. Baadae akapata Daktari mmarekani nadhani wa Boston ambaye anamtibu mara zote kwa kumpatia dawa, na huyu Daktari kamshauri aachane na kazi za siasa baada ya 2010 kwani ndizo zinampatia stress na tatizo alilonalo halihitaji stress, lakini madaraka matamu hataki kufuata masharti ya Dr.

Huyu Dr wa marekani ndo yule alimleta akampeleka mbuga za wanyama na baadae alitoa misaada pale MOI. Tatizo hili la kupoteza fahamu na ku collapse limekuwa likimtokea mara kwa mara hata akiwa IKULU tu, nakumbuka ile ziara ya mkoani Mbeya aliopopolewa mawe alipata kuanguka pia katika moja ya shughuli zake za ndani ikulu ndogo ya huko.

Mimi nawashauri wasaidizi wa Rais wawaambie watanzania ukweli, waache kutupamba kwa maneno kuwa anafanya kazi nyingi ndo maana ananguka, wawaeleze watanzania tatizo la msingi la afya ya Rais wao. Hizi safari za Marekani kila kukicha ni danganya toto, kinachompeleka huko ni matibabu tu.
 
Naamini kuwa wanamshauri sana amweke lupango RA na EL lakini yeye mbishi sasa naamini.
Bunge linakaribia na moja ya hoja watakazo zijadili ni pamoja na RAEL a.k.a Richmond au wataifunika?
 
Huyu Bwana siyo mzururaji bali ni mchapa kazi anayewajali wananchi. Hivi mlitaka akae Ikulu huku wakuu wa wilaya na mikoa wakidanganya hakuna njaa ingali watu wanakula mizizi? Tumwombea apate afya njema.
Afukuze wote lakini tatizo lake anaweka washikaji zake ndiyo maana anawaonea haya..
 
By the way is there any chance kwamba RAIS JK anapitapita hapa JF? Is there any chance? I am trying to THINK LOUDLY! Hivi inawezekana kweli humu hakanyaji....
Nahisi huwa anapita...
 
By the way is there any chance kwamba RAIS JK anapitapita hapa JF? Is there any chance? I am trying to THINK LOUDLY! Hivi inawezekana kweli humu hakanyaji....
Nahisi huwa anapita...

lazima mheshimiwa anapita hii ndo web yetu wabongo akiwa room kwake nina hakika ana laptop full network ...habari anaipata
 
Nerve problem is something very serious. But I believe he has not closed all the doors for advise. He could turn to people whom he trusts for what should be done next. Nature ya operations za kichwa ni ngumu, na hilo sio suala la kukimbilia haraka maana unajua mambo ya kupasua kichwa bwana yana athari zake.hata hivyo kama option zote hazifanyi kazi basi utafanyaje bwana itabidi tu.
Well, mimi namuombea afya njema ili aweze kuendelea na kazi zake.
 
Last edited:
lazima mheshimiwa anapita hii ndo web yetu wabongo akiwa room kwake nina hakika ana laptop full network ...habari anaipata

kupata habari hakusaidii kama habari inazopatikana inachukuliwa kama soga la kijiweni.

Nimeipenda avatar yako.
 
Si ngoma kama wengi wanavyoweza kufikiri, lakini hao watu wa Raia Mwema hapo juu wanajua, maana katika hadithi yao wamemwandika Kikwete ila kwa kificho, kwa sababu Kikwete ndiye anayekataa upasuaji na anayependa kuendekeza mambo ya waganga wa kienyeji.

Uzuri au ubaya ni kwamba wenye kuujua ugonjwa hawasemi, wenye kusema hawaujui.

Upasuaji unaweza kuhusu gonjwa la aina tofauti tofauti -jipu, busha etc
 
Wakuu mimi hadi nisikie maelezo wa watalaam wanaojua kilichotokea.. Na nadhani sisi wananchi tuna kila haki ya kufahamu kilichotokea na kimesababishwa na nini..Kujua afya ya rais ni right ya wananchi na sii personal issue hata kidogo...JK ana maradhi gani?..Tunaposhindwa kutamka hadharani matatizo yetu ni sawa kabisa na maradhi ya uchumi wetu kwa sababu leo hii ukiniuliza kwa nini JK anaanguka kila siku nitajibu - sifahamu kwa nini JK anaanguka kila siku!.. yale yale majibu ya Umaskini wa Tanzania yakitanguliwa na usiri mkubwa.
Nimesubiri sana kusikia toka vyombo vya Taifa lakini baada ya siku mbili ndio imetoka hiyo, inaonyesha wazi kuna usiri fulani..
 
lazima mheshimiwa anapita hii ndo web yetu wabongo akiwa room kwake nina hakika ana laptop full network ...habari anaipata
Kama angekuwa anapita humu angesha wafunga mafisadi wote bila kuwaacha RA na EL, asingejaza washikaji zake kwenye serikali yake na sijui kama angehitaji washauri au niule ubishi wake....
 
kwanza nafikiri Kikwete awaeke watanzania uwazi ikiwa ana matataizo ya Afya kwani nafikiri is un fit to rule our country if he is unfit lazima awatangazie Watanzania na weke wazi kabla ya kuchukua fomu kugombea tena urais kwa kipindi kijacho.
 
Rais wetu ni kama Vasco Da Gama! kikla kukicha ni USA na akisharudi Bagamoyo , Msata! hivi huo muda wote aliokaa US kulikuwa na kipi kikubwa alichokuwa akifanya?
Rais wetu anatupa shida sana watu wanaoishi maeneo ya kuanzia Mbezi beach hadi Bagamoyo! Kama akiwepo Dar es salaam basi ujue kama si Jumamosi basi Jumapili ataenda Bagomoyo au Msata na barabara zitafungwa masaa kadhaa! Hivi haoni vibaya watu wanavyoteseke na folelini zinzao sababishwa na miosafara yake mirefu yenye mbembwe na msururu wa magari ya kifahari katika nchi fukara(UMASKINI WA KUJITAKIA)?
 
hakuna tatizo...That is AICT Africa inland church!!
thanks Mr President that was Great let us work hard Cause we dont know Bla bla bla
 
Akuna cha ugonjwa waulizeni waliokuwepo...wapendwa walikuwa wanakemea mapepo sasa hawakujua rais nae ndio anaanza kuhutubia...rais akiwa anaendelea jamaa huku wanaongeza moto..//loh!!!!!!rais akaona iswe tabu ikabidi kala chapa huyoo....sio wa kwanza ,rais kamuzu banda aliwahi kudondka pale chuo kikuu wakati vijana wako nje wanakemea na kusali....

Ha ha ha ha,

Hii ya wapendwa kukemea mapepo imenimaliza mbavu jamani.

Ohh mai mai mai gademu it .... JF haina mfano Tanzania nzima.
 
Jamani Someni Marko 9:19-25 mtaona jinsi mapepo wanavyo mwogopa Yesu.


UNAJUA VIONGOZI WEU WENGI WANACHEZA NA MUNGU;;UKIANGALIA ASILIMIA 50-80 YA VIONGOZI WAMEUA WATOTO AMA NDUGU ZAO KAMA SI WAKE ZAO ILI WAPATE UBUNGE/UWAZIRI UDIWANI NA HATA SERIKALI ZA MITAA BAYA ZAIDI WAPO WANAOINGIA WENYEWE PALE BAGAMOYO ;;NA KUAMUA KUVUA NGUO KUKAA U%&&&I HATA SIKU KUMI TENA HUKU WAMELALA CHALI WAKIFANYIWA UGANGA...HATARI TUPU..ILA KWA JINA LA YESU BWANA WA BWANA MUNGU WA MIUNGU ALFA NA OMEGA HATA ACHUKULIWE NA USALAMA WA TAIFA TUNARUSHA MAKOMBORA HUKO HUKO ALIPO........HUU MWAKA WAKIAMBIWA JAMANI WATANZANIA TUCHAGUE CHAGUO LA MUNGU CCM HAWAAMINI MOTO UMESHAANZA KUONEKANA SERIKALI ZA MITAA....KAZI WANAZO
 
Laiti haya maombi yangefanyika kwenye ofisi ya bunge basi viti vingebaki vitupu,
 
Rais wetu anatupa shida sana watu wanaoishi maeneo ya kuanzia Mbezi beach hadi Bagamoyo! Kama akiwepo Dar es salaam basi ujue kama si Jumamosi basi Jumapili ataenda Bagomoyo au Msata na barabara zitafungwa masaa kadhaa! Hivi haoni vibaya watu wanavyoteseke na folelini zinzao sababishwa na miosafara yake mirefu yenye mbembwe na msururu wa magari ya kifahari katika nchi fukara(UMASKINI WA KUJITAKIA)?

Mkuu unashauri awe anatumia Helicopter?
 
Back
Top Bottom