Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete azidiwa jukwaani, akimbizwa mapumziko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamanda, Oct 4, 2009.

  1. Kamanda

    Kamanda Senior Member

    #1
    Oct 4, 2009
    Joined: Dec 5, 2007
    Messages: 135
    Likes Received: 110
    Trophy Points: 60
    Rais Jakaya Kikwete leo amepatwa tena maswaibu yaliyomkuta Mwanza wakati wa kampeni 2005 akiwania kura za Watanzania huko Mwanza, safari hii siyo kwa kukabwa na Msukuma, bali afya kutetereka.

    Afya ya Rais Kikwete ilitetereka akiwa jukwaani akihutubia waumini wa Kanisa la AICT na wananchi katika Kiwanja cha Kirumba ambapo iijisikia vibaya na kubebwa na watu wa usalama kutoka jukwani hadi chumba cha watu maarufu katika uwanja huo kwa mapumziko.

    Rais Kikwete baada ya kuwa huko kwa mapumziko mafupi alirejea na kuendelea na hotuba yake.

    Inawezeana ni uchovu wa safari kama alivyosema na safari hii amesema hatarudia 'mchezo' wa kuunganisha safari ili apate muda wa kupumzika.

    Pole Rais Kikwete
     
  2. n

    nzala Member

    #2
    Oct 4, 2009
    Joined: Dec 24, 2008
    Messages: 43
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 15
    je, baada ya kurudi jukwaani, amemaliza salama kuhutubia wakazi wa mwanza?
     
  3. Junius

    Junius JF-Expert Member

    #3
    Oct 4, 2009
    Joined: Mar 11, 2009
    Messages: 3,183
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 133
    the guy is tired kwa kuzurura tuuuu.
     
  4. Mshiiri

    Mshiiri JF-Expert Member

    #4
    Oct 4, 2009
    Joined: Jun 16, 2008
    Messages: 1,893
    Likes Received: 66
    Trophy Points: 145
    Hapana this excellence is doing hard to make sure things run. He could have just stayed in Dar and nothing happens BUT seeing and saying and deciding here and there. It is not a joke. He deserves to rest a while BUT he sees no chance to rest as the country is POVERTY STRICKEN in all sectors. Jamani hazururi ni majukumu. Fikirini outside the box. Msiingie kwenye dirty politics all the time.
     
  5. Josh Michael

    Josh Michael JF-Expert Member

    #5
    Oct 4, 2009
    Joined: Jun 12, 2009
    Messages: 2,525
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 135
    Hapa kitu cha msingi kwa Rais wetu ni kupumzika maana amechoka sana kwa ajili ya safari nyingi sana, Pole Jk
     
  6. b

    bnhai JF-Expert Member

    #6
    Oct 4, 2009
    Joined: Jul 12, 2009
    Messages: 2,208
    Likes Received: 1,373
    Trophy Points: 280
    Mungu ampe afya njema. Anajitahidi kuona kila jambo linakwenda lakini na mwili unahitaji mapumziko. Hana anachofaidi katika hizo safari zaidi ya tuhuma lukuki zisizo na msingi. Maana akitaka kwenda anaweza na watu asijue. Anaweza kusema nipo mapumziko. Anaponzwa na uwazi zaidi na uwajibikaji.
     
  7. MwanaFalsafa1

    MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

    #7
    Oct 4, 2009
    Joined: Feb 26, 2008
    Messages: 5,566
    Likes Received: 28
    Trophy Points: 135
    Nchi nyingi sana afya za viongozi wakuu zinakua "state secret". Hata kama ana maradha yanayo msumbua lazima kuta fanyiwa cover ups. Anyway pole sana mheshimiwa raisi.
     
  8. Invisible

    Invisible Admin Staff Member

    #8
    Oct 4, 2009
    Joined: Feb 11, 2006
    Messages: 9,091
    Likes Received: 237
    Trophy Points: 160
    Nasikia hata Press Conference alokuwa aifanye saa 12 jioni ya leo badala yake anatoa Press Release tu.

    Pole Mheshimiwa
     
  9. K

    Keil JF-Expert Member

    #9
    Oct 4, 2009
    Joined: Jul 2, 2007
    Messages: 2,214
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 135
    Kwenda kuwahutubia AICT nayo ni sehemu ya kuondoa matatizo ya umasikini?

    Alikuwa Arusha kufungua Mkutano wa CPA, na akaunganisha kwenda Mwanza. Yote hayo ni mambo yanayohusu politics, he can easily send a representative kufanya hizo kazi, kwani lazima yeye ahudhurie shughuli zote?

    Akialikwa kwenda Mby anaweza kutuma mwakilishi lakini akialikwa kwenda Mwanza lazima aende mwenyewe. Ni sawa na jinsi anavyoenda US kila kukicha na hajawahi kutuma mwakilishi.

    Hayo ni matatizo ya kujitakia mwenyewe na wala hayahusiani na mikakati ya kuleta maendeleo ama kuondoa umasikini.

    Aliwahi kuulizwa kwanini Tanzania ni masikini, alijibu kwamba hata yeye hajui kwanini Tanzania ni masikini. Kama hajui kwanini Tanzania ni masikini atawezaje kuondoa umasikini? Kwa kusafiri kila siku?

    Hivi Mwanza kuna nini? Maana haiwezi kupita miezi kadhaa bila ya JK kutia timu Mwanza na kuna mikoa mingine alionekana mara moja tu tangu achaguliwe kuwa Rais miaka 4 iliyopita.
     
  10. Belo

    Belo JF-Expert Member

    #10
    Oct 4, 2009
    Joined: Jun 11, 2007
    Messages: 11,281
    Likes Received: 4,286
    Trophy Points: 280
    Bado yuko Mwanza au kisharudi Bagamoyo
     
  11. Crashwise

    Crashwise JF-Expert Member

    #11
    Oct 4, 2009
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 22,172
    Likes Received: 862
    Trophy Points: 280
    kazi anayo maana hata kampeni zimekaribia...au wasukuma nije nije..
     
  12. b

    bnhai JF-Expert Member

    #12
    Oct 4, 2009
    Joined: Jul 12, 2009
    Messages: 2,208
    Likes Received: 1,373
    Trophy Points: 280
    Yapo maeneno ambayo ni rahisi saana kutuma mwakilishi. Katika kipindi hiki ambacho nchi ipo kwenye malumbano ya kidini ni lazima rahisi aende akaseme na akaeleze matarajio ya serikali na serikali inafanya nini. Wale jamaa wanafikisha miaka 100, ni tukio muhim kwao, sasa kama wakitumiwa mwakilishi, nadhani itakuwa haitoshi, maana pia wanatengeza asilimia kubwa ya Taifa hili.
     
  13. Ng'wanza Madaso

    Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

    #13
    Oct 4, 2009
    Joined: Oct 21, 2008
    Messages: 2,278
    Likes Received: 60
    Trophy Points: 145
    Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla ndiko alikopata kura nyingi zaidi 2005.
     
  14. Crashwise

    Crashwise JF-Expert Member

    #14
    Oct 4, 2009
    Joined: Oct 23, 2007
    Messages: 22,172
    Likes Received: 862
    Trophy Points: 280
    kasharudi dar..
     
  15. Oxlade-Chamberlain

    Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

    #15
    Oct 4, 2009
    Joined: May 26, 2009
    Messages: 7,928
    Likes Received: 103
    Trophy Points: 160
    hio yote inatokana pia na kutokokuwa na washauri wazuri wa afya.daktari gani anashindwa kumshauri raisi apumzike baada safari ndefu kama hizo anazofanya.
     
  16. Babylon

    Babylon JF-Expert Member

    #16
    Oct 4, 2009
    Joined: Feb 5, 2009
    Messages: 1,338
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Au Waraka wa makanisa umegeuka Halal Badir ?
     
  17. Kamanda

    Kamanda Senior Member

    #17
    Oct 4, 2009
    Joined: Dec 5, 2007
    Messages: 135
    Likes Received: 110
    Trophy Points: 60
    Nashukuru kwamba Rais Kikwete mwenyewe amekiri kuwa amekuwa mbishi wa kuwasikiliza wasaidizi wake, kumbe walimshauri kupumzika, asiende Arusha wala Mwanza, lakini akawapuuza.

    Ni vyema sasa akapunguza safari na kuwasikiliza wasaidizi wake wanapomshauri kupumzika ili awe na nguvu na mawazo chanya kwa siku inayofuata, niliwahi kuelezwa na madaktari kuwa mapumziko ya mwili na akili ni muhimu kwa kujenga upya mawazo mapya.

    Kinachomchosha sana JK siyo hotuba zake ndani ya nchi, bali safari za nje, jamani wengi wetu tunajua namna ndege zinavyochocha, ukiwa angani unaipata fresh hata kama ni dege kubwa.

    Pole JK, lakini anza kupumzika sasa, ingawa hiyo nayo isipitilize saaana ikwa ni kupumziiiika tu na kupumziiiika.
     
  18. Kamanda

    Kamanda Senior Member

    #18
    Oct 4, 2009
    Joined: Dec 5, 2007
    Messages: 135
    Likes Received: 110
    Trophy Points: 60
    Nadhani mbali na hilo, ana mapenzi makubwa na Mwanza. Yupo mtu alimsaidia sana kwenye mambo yake, hivyo anaona kuwa Wasukuma wote (wengi kwao Mwanza) ni roho safi na wakarimu
     
  19. Mwazange

    Mwazange JF-Expert Member

    #19
    Oct 4, 2009
    Joined: Nov 16, 2007
    Messages: 1,051
    Likes Received: 8
    Trophy Points: 135
    Mheshimiwa anatakiwa apumzike......
     
  20. K

    Keil JF-Expert Member

    #20
    Oct 4, 2009
    Joined: Jul 2, 2007
    Messages: 2,214
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 135
    Aeleze kwamba serikali inafanya nini kuhusu kumaliza malumbano ya kidini? Hapo huwezi kumsikia akisema chochote, jamaa ni opportunist. Ndiyo maana swala la Mahakama ya Kadhi alianza kwa kuruka kiunzi kwamba hakuandika Ilani ya Uchaguzi, bali iliandaliwa na Chama.

    Alipoona mambo yamekuwa moto kule Bungeni baada ya waislam kusema watainyima CCM kura, akamtuma Pinda aseme na masheikh, yeye hakwenda.

    Nasubiri kwa hamu sana magazeti ya kesho ili nijue kasema nini huko Mwanza. Kwa kifupi ni kwamba hana maamuzi na hana msimamo unaoeleweka. Kitu chochote ambacho kinaonekana ni sensitive huwa anakwepa kukabiliana nacho anasubiri kwanza apime upepo ndipo utamuona anakuja na kuongelea na siyo kutoa tamko rasmi.

    Ilikuwaje wabunge wakashindwa kujadili hotuba yake mwaka jana? Walidanganywa weeeee mpaka ikafika mahali wakaacha hata kuuliza. Maana ingejadiliwa wangeichambua kama karanga na yeye hakutaka hayo yafanyike.

    Kwa hiyo kwenda Mwanza ama kutokwenda hakuna tofauti yoyote kwa kuwa hana kitu firm anachoweza kuongelea ama kukitolea msimamo yeye kama Rais wa nchi ama Mwenyekiti wa CCM. Ndiyo maana kila kukicha watu wanalalamika kwamba uongozi umepwaya, kwa sababu mtu anayetakiwa kuongoza ni mwoga, yuko nyuma nyuma anasubiri kwanza apime kina cha maji ndiyo apite ama aingie.
     
Loading...