Nyangumi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2007
- 507
- 17
Maneno yako yana msingi wa kujilinda lakini naona kipindi cha kumpima hakijafika wala hajatimiza nusu ya awamu ya kwanza,huyu mtu ndio kwanza ameanza kujenga si kweli hakuna mabadiliko katika uwajibikaji wa ahadi zake.QUOTE]
Yaani kweli ukipenda kitu huoni kasoro zake. Watanzania wa sasa sio wajinga.Hii gari imeshaacha barabara inaelekea kwenye korongo. Hatuhitaji kuingia kwenye korongo ndo tumwambie dereva. Watanzania wanamtahadharisha JK kuwa gari yake imeshaacha barabara.
Hiyo miaka miwili na nusu yote ya nini?Si yeye ndo alituambia NGUVU MPYA NA KASI MPYA? Au hiyo kasi mpya na nguvu mpya iko kwenye kuiba na kusafiri nje.Imebakia miezi nane tu,itafika utamtetea tena kuwa "hata kipindi chake cha miaka 5 hajamaliza"
Watanzania hapa tumeliwa. Hakuna kitu kibaya kama kufanya mapenzi ya siasa sawa na ushabiki wa mpira.