KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
Kwanza kabisa mtu akinipa heshima ya ukada mimi naipokea kwa taadhima kabisa sina noma wala nini, enzi za Nyerere jamaa mmoja alisema Nampendekeza Julius kuwa Raisi wa jamhuri anayepinga anyooshe mkono, hakuna aliyenyoosha mkono basi Nyerere akawa raisi wa jamuhuri
Aisee kwamba jua ndio limewachosha mimi sikubaliani kabisa, mbona wanene wa CCM hawajachoka?wakati wao wapo kwenye nchi hii pia na jua si linawamulika wao pia? mbona California jua linapiga mwaka mzima lakini watu hawajachoka? mwenye njaa huchoka, mwenye shibe hunawiri.
hao watu wa california wana rangi gani ?
watu wa nyumbani bana sio wengi wanaojua/hata kama wanajua hawatilii maanani mambo ya manukato na uturi bobu, sasa utakuta mtu anaamka asubuhi mswaki jiti, hapaki mafuta, nywele hachani, unategemea aonekane sawa na wewe unayepaka uturi kila siku, deodorant ya nguvu, unanyeshewa na maji ya mvua kila siku bafuni ! wakati nyumbani mtu anatumia ndoo na maji utakuta sana sana mtu yanamwagikia kichwani, lakini kwenye magoti husahau njia na yakifika hadi kwenye magoti basi ujue mvua siku hiyo imenyesha tena ya nguvu ! bana wee, manukato, na joto kali hufanya watu wachoke ! Nadhani hapa tutaende mbali na hii mada kama tutaendelea kuzungumza kuhusu hali ya hewa !