Kikwete awadanganya watanzania - TENA

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
58
Kwa wale ambao wanafuatilia siasa za marekani watakumbuka kuwa miaka ya 90, serikali ya Clinton ilifanikiwa kuweka makubaliano na Korea kaskazini ili wamarekani wawapatie wakorea mafuta na chakula kwa uhakikisho kuwa wakorea wataachana na mipango ya kujenga nyuklia.

Joji Kichaka (ambaye alipondea sana alichofanya Clinton na democrats) alivyoingia madarakani alitishia kuwa angetumia nguvu ili wakorea waache nyuklia na vitisho vingine kibao. Haya, hata miaka haijapita, kichaka amedhihirisha kuwa mtu wa vitisho tu kwani wakorea wamejaribu kwa mafanikio nyuklia yao na pia Kichaka imebidi tu atume watu wakafanye mazungumzo na wakorea.

Mfano huu wa Kichaka na vitisho vya maneno ya democrats ni kitu ambacho Kikwete amejifunza toka kwa rafiki yake joji kichaka na sasa anakitumia Tanzania. Nilifuatilia sana maneno na ahadi za Kikwete wakati wa kampeni za kugombea uraisi. Maneno mengine sio tu yalikuwa kama ahadi za Joji Kichaka bali yalikuwa kama ahadi za mama anayebembeleza na kuhadaa mwanaye ili anyamaze na kulala.

Kikwete aliahidi ajira milioni moja, aliahidi kupitia mikataba upya, aliahidi kuboresha maisha, aliahidi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu, aliahidi ujenzi wa miundo mbinu, aliahidi kusaidia michezo nchini, aliahidi kufanya vingi sana...

Baada ya kuwa raisi, akaomba apelekewe majina wa mafisadi na wauzaji wa madawa ya kulevya, akaanzisha website ili kupokea maoni ya wananchi, akatoa namba za simu ili kupokea maoni ya watu na ahadi kibao.

Wakati watu wakisubiria sera zitekelezwe, waziri wake akasaini mkataba wa Richmonduli, buzwagi, mikataba kibao ya uchunguzi wa madini, nakadhalika. Wakati huo huo ikajulikana kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa pesa BOT, akiba kubwa ya pesa za kigeni iliyoachwa na Mkapa ilikuwa ikipotea, nk.

Wakati haya yakiendelea, Kikwete akaanza safari za nje ambazo zimetumia mabilioni ya shilingi za watanzania, ukaguzi wa fedha ukaonyesha kuwa kuna matumizi zaidi ya bilioni moja ambayo hayana uthibitisho wowote huko ikulu, nk.

Hali ya wananchi ikazidi kuwa mbaya, mfumuko wa bei zaidi ya asilimia mia mbili kwa bidhaa muhimu, nk wakati serikali na viongozi wakitumbua mabilioni kwa ufahari wa magari na serikali yenye watu wengi sana (moja ya baraza la mawaziri kubwa kabisa barani Afrika).

Wakati wananchi wakisubiri vitendo, Kikwete anaendeleza trik ya Joji Kichaka (ndio maana hawa ni marafiki) ya kutoa maneno tu ambayo hayana vitendo. Hotuba yake ya Dodoma imejaa ahadi nyingi kuliko hata zile alizotoa wakati wa kampeni.

Kwa mara nyingine tena Kikwete amewadanganya watanzani. Swali ni kwamba, mpaka lini ataendelea kuwahadaa watanzania?
 
Maneno yako yana msingi wa kujilinda lakini naona kipindi cha kumpima hakijafika wala hajatimiza nusu ya awamu ya kwanza,huyu mtu ndio kwanza ameanza kujenga si kweli hakuna mabadiliko katika uwajibikaji wa ahadi zake.lakini waswahili wanasema akutukanae hakuchagulii tusi,mnavyotaka nyinyi kuwa mkisema tu basi achukue hatua za kuwakamata na kuwapeleka jela,hilo halipo isipokuwa kwenye nchi za kidikiteta.Muungwana ni kiongozi muadilifu na ni binadamu kama binadamu wengine ,hakuna asiekosea na kila unapokosea ndipo unapojifunza mbinu mpya za kukabiliana na matatizo Tanzania mkae mkijua si kisiwa kama kama kisiwa cha Shelisheli,hivyo kinachotakiwa ni subira ya miaka mitano,hapo Watanzania ndio watampima uwezo wake wapi aliahidi na wapi amefikia na kipi kimekamilika.Haraka haraka haina baraka.
 
kimsingi tunakubaliana, Kikwete naye siyo safi.. and this time u said it! Nadhani ataendelea na maneno hayo hadi ifike 2010 ambapo atawaomba Watanzania samahani kwa kushindwa kutimiza ahadi fulani na akipewa ngwe nyingine atahakikisha anamaliza. sura yake itawekwa kwenye mabango, viongozi wa dini watasema ndio chaguo la Mungu, na nyimbo zitatungwa huku picha za kuonesha yeye ni mtu wa watu zikisambazwa.. bahati mbaya it won't work... Atakuwa ni Rais wa Kwanza katika Tanzania kutawala kwa kipindi kimoja.
 
... Atakuwa ni Rais wa Kwanza katika Tanzania kutawala kwa kipindi kimoja.

Pamoja na jitihada mahususi anazozifanya kupitia mtandao wake kuna kila dalili wafuasi wake na wanachama wakagawanyika, wakapoteza uelekeo,utii na uaminifu kwa mwenyekiti wao, ambaye anazidi kutomboa mtumbwi na yeye angali yumo. Atapata upinzani mkubwa toka kwa watu alionao karibu. Hii itapelekea kushindwa vibaya 2010, kama hatua madhubuti za kupapambana na ufisadi na rushwa hazitachukuliwa. Muungwana amekuwa na maneno mengi kuliko utekelezaji, 2010 wananchi watakuwa na vitabu vyake sera ya CCM na ahadi wakati wakiomba kura 2005, wananchi watahoji, maisha bora yako wapi? Ajira? Maji? bara bara? mbona rushwa inazidi kuongezeka? hapo ndipo watakapo chinjiwa baharini.....hata damu yao tusiione tena.
 
kimsingi tunakubaliana, Kikwete naye siyo safi.. and this time u said it! Nadhani ataendelea na maneno hayo hadi ifike 2010 ambapo atawaomba Watanzania samahani kwa kushindwa kutimiza ahadi fulani na akipewa ngwe nyingine atahakikisha anamaliza. sura yake itawekwa kwenye mabango, viongozi wa dini watasema ndio chaguo la Mungu, na nyimbo zitatungwa huku picha za kuonesha yeye ni mtu wa watu zikisambazwa.. bahati mbaya it won't work... Atakuwa ni Rais wa Kwanza katika Tanzania kutawala kwa kipindi kimoja.

Naomba kuunga mkono hoja....
 
....Muungwana ni kiongozi muadilifu..... Tanzania mkae mkijua si kisiwa kama kama kisiwa cha Shelisheli, hivyo kinachotakiwa ni subira ya miaka mitano,.....

Unasema kuwa muungwana ni muadilifu wakati richmonduli, buzwagi, bot, ubadhirifu ikulu anahusika moja kwa moja na mtandao wake wa EL na mkoloni Rostam Azizi.

Na hayo mambo ya shelisheli yanahusiana nini hapa na subira ya miaka mitano. Watanzania wakisubiri miaka mitano ipite, mikoa yote ya kanda ya ziwa na kati itakuwa imeuzwa kwa wakoloni.

Wewe inaonekana huitakii mema Tanzania. Nusu ya population ya Tz iko kanda ya ziwa na kati, hiyo fujo itakayotokea baada ya ardhi yao kuchukuliwa na Barrick (kipengele kwenye mkataba wa Buzwagi kinaruhusu Barrick kuchukua ardhi yoyote itakayosaidia kazi yao) utaizima vipi?
 
Siombi kuunga mkono hoja bali nathibitisha hoja ya Mwafrika wa kike ni kweli tupu na ninaikubali kabisa.

Ukombozi huanzia ktk nafsi na watanzania wakishafahamu ukweli ndani ya nafsi zao patakuwa hapakaliki hapa. Cha msingi ni kuwatoa kafara mifisimaji yote serikalini na kuanza A. yaanu kuanza upya.

Naithibitisha pia hoja ya Mzee mwanakijiji kuwa atakuwa rais wa kwanza kuongoza nusu term na hapo jua litakapokuchwa ndipo wenye macho wataona....
 
jamani lazima tuwe wa kweli. Hadi hivi sasa Kikwete hajaonesha uwezo wa kupambana ulingoni, ila ameonesha umahiri mkubwa wa kutoa vitisho vya kupigana. Binafsi ninaamini kama akiamua kuvaa gulovu zake na kuanza kupigana anaweza kupigana kwa ufundi mkubwa. Tatizo, watu anaotakiwa kupigana nao ndio waliompatia ulingo huo na baadhi ya opponents wake ni rafiki zake. Je ataweza kuwapiga ngumi ulingoni na jioni kuwakaribisha chai nyumbani? akiweza kusolve that dilemma then and only then ataingia ulingoni na kupigana vinginevyo itakuwa ni kujirusha rusha na kurusha ngumi hewani kama maandalizi yasiyokoma huku akitumia muda mwingine kupiga ngumi gunia la mchanga huku watu wakimsifia jinsi anavyotoka jasho na kuhema...
 
Mwkjj,

Kikwete anabet kuwa uamskini wa wa-Tanzania utakuwa umeongezeka mara mbili mwaka 2010 kwa hiyo pesa kidogo ya chumvi na sukari toka kwa Rostam Azizi itamrudisha Ikulu kwa kishindo kingine!
 
Its a wish stated as a fact once some conditions are met.

hehehehehehe, I can't laugh louder than this.....you know MMKJJ you can make a good politician or Mbowe's spokesman. For you will be able to provide a cocktail-type of answer that fits any imaginable question...hehehehehe. Smart.
 
Maneno yako yana msingi wa kujilinda lakini naona kipindi cha kumpima hakijafika wala hajatimiza nusu ya awamu ya kwanza,huyu mtu ndio kwanza ameanza kujenga si kweli hakuna mabadiliko katika uwajibikaji wa ahadi zake.lakini waswahili wanasema akutukanae hakuchagulii tusi,mnavyotaka nyinyi kuwa mkisema tu basi achukue hatua za kuwakamata na kuwapeleka jela,hilo halipo isipokuwa kwenye nchi za kidikiteta.Muungwana ni kiongozi muadilifu na ni binadamu kama binadamu wengine ,hakuna asiekosea na kila unapokosea ndipo unapojifunza mbinu mpya za kukabiliana na matatizo Tanzania mkae mkijua si kisiwa kama kama kisiwa cha Shelisheli,hivyo kinachotakiwa ni subira ya miaka mitano,hapo Watanzania ndio watampima uwezo wake wapi aliahidi na wapi amefikia na kipi kimekamilika.Haraka haraka haina baraka.

Umerejea kwa jina jipya ee? Karibu tena ulingoni.
 
...

Hali ya wananchi ikazidi kuwa mbaya, mfumuko wa bei zaidi ya asilimia mia mbili kwa bidhaa muhimu, nk /quote]

Zipi? Acha kamba za kitoto!

Insurgent hivi unaishi Bongo kweli??

Mifano michache toka 2006 hadi sasa
mkate from 300-1000 tsh
mche wa sabuni 500-1200
Maharage from 400-1200
Unga wa ngano kilo 1 from 300- 1000
Mafuta ya kupikia 3 lt from 2500-9000

Hii siyo kwamba nimegushi ni kweli kabisa nimekutana nayo maduka ya survey last friday!

Hapa nakwambia bei za DSM what about mtu aliyeko Kasulu? Ukerewe?Nanyamba? Bugomora? Mbamba bay Sumbawanga na Mpanda?

Usisahau mashahara ni 84 alfu tu!
 
kwa bei hizo hapo juu, sidhani kama dar-es-salaam watu wangebaki hadi hivi sasa ! kwa ufahamu wangu mie ni kwamba wengi wao hawana kazi, hata kama wana kitu cha kufanya to earn a living, sidhani kama hata elfu 70 zinafika ! nadhani wote wangekimbilia nachingwea, mporipori, ukerewe, na kwingineko wakale mpunga !
 
hehehehehehe, I can't laugh louder than this.....you know MMKJJ you can make a good politician or Mbowe's spokesman. For you will be able to provide a cocktail-type of answer that fits any imaginable question...hehehehehe. Smart.

no.. I think I can be very useful kwa CCM kuliko wapinzani.. if a perfect offer is made.. LMAO...
 
Insurgent hivi unaishi Bongo kweli??

Mifano michache toka 2006 hadi sasa
mkate from 300-1000 tsh
mche wa sabuni 500-1200
Maharage from 400-1200
Unga wa ngano kilo 1 from 300- 1000
Mafuta ya kupikia 3 lt from 2500-9000

Hii siyo kwamba nimegushi ni kweli kabisa nimekutana nayo maduka ya survey last friday!

Hapa nakwambia bei za DSM what about mtu aliyeko Kasulu? Ukerewe?Nanyamba? Bugomora? Mbamba bay Sumbawanga na Mpanda?

Usisahau mashahara ni 84 alfu tu!

Rwabugiri waambie maana inaonekana baadhi ya watu wanahitaji kuchukua darasa la hesabu hapa kidogo.

bei imepanda kwa baadhi ya vitu zaidi ya asilimia mia 300.
 
Back
Top Bottom