Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Wakati mwingine napata shida kumuelewa Rais wangu

Rais bado hajaisoma ripoti hiyo, lakini ameshaanza kuishukuru Kamati kwa kazi nzuri! amejuaje wamefanya kazi nzuri?

Je majukumu ya Kamati hiyo yametimizwa?
- Je watuhumiwa wamechukuliwa hatua zozote za sheria? HAPANA
- Je fedha zilizotolewa isivyo halali zimerudishwa? HAPANA
- Mtuhumiwa namba moja Marehemu Daudi Balali alihojiwa? HAPANA

lakini bado Mh Rais anatuambia kazi iliyofanywa na Kamati ni nzuri! Tumekubali sasa tunasubiri taarifa hiyo rasmi.

Hapa ndipo kuna tatizo,wamefanya kazi nzuri sababu walishapeleka Draft na ikarudishwa ili waifanyie marekebisho aliyokuwa anayataka????
 
breeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeki!!! hold on nusura nimiss hiki:

Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.

Mimi nilidhani baada ya kutolewa maamuzi Ripoti nzima itawekwa hadharani ili kila mwananchi ajiridhishe kama ilikuwa ni "kazi ngumu na nzuri". Kwa vile hakuagiza ripoti hiyo na yeye kaikubali na kuitolea "maamuzi" ambayo hakutakiwa kuyatolea basi aiweke hadharni ili wananchi wajiridhishe kuwa ni kweli maamuzi yake hayakuweza kufanyiwa kazi na mwanasheria mkuu, IGP, na Boss wa TAKUKURU.

Ningependa vyombo vya habari vililie ripoti nzima iwekwe hadharani badala ya kuambiwa maamuzi yaliyochukuliwa. Wananchi wanahaki ya kujua msingi wa maamuzi hayo.
 
Ningependa vyombo vya habari vililie ripoti nzima iwekwe hadharani badala ya kuambiwa maamuzi yaliyochukuliwa. Wananchi wanahaki ya kujua msingi wa maamuzi hayo.
Mzee Mwanakijiji,

Kwanini siye wenyewe kama watanzania tusiamue kuifuata Ripoti pale Magogoni?na siye ndiyo tutoe maamuzi ya nini kifanywe.

Naisubiri Alhamisi
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.

Mkuu MMKJJ,
Kwangu mimi hii ni ndoto ambayo ikigeuka kuwa kweli watanzania wengi sana tutafurahi sana na kurudisha imani kwa JMK.
Lakini kwa namna ninavyolitazama hili kashfa la EPA nashindwa kuaminin kama huyu muungwana anayo jeuri ya kufanya maamuzi makubwa na mazito kama hayo unayoyatamani.
Muungwana amezidiwa, mafisadi wamembana mno na ndio waliomzunguka itakuwa muujiza kwa kweli kuyafanya hayo unayoyafikiria.
Navyojua kama kawaida yake atatumia fursa ya kulihutubia bunge kupiga porojo na maneno yake matamu, manake huyu mtu wa pwani kiswahili anakifahamu vizuri sana.
Ulishawahi kujiuliza kwanini siku hizi hakutani na waandishi wa habari "live" kama alivyokuwa anafanya hapo kabla?
Labda itokee miujiza, lakini ukweli ni kuwa muungwana kwa hili la EPA, ameshindwa vibaya.
 
a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Ka nzi kameishakufikia nini mkuu!? teh teh teh!!!!!!!!
 
Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Well An interesting anticipation. Unafikiri ni kwa misingi ipi?
 
Lakini ni kipi kinachopmfanya rais wetu aonekane ameshindwa? Ukisikiliza maneno yake na kusoma mikakati yake, inaonekana kuwa ni mizuri sana. Kwa nini utekelezaji unakwama? Ni tatizo la rais mwenyewe au wasaidizi wake? Nauliza hivi kwa sababu imefika wakati watu wengi wenye shida wanaamua kukimbilia wka rais mwenyewe kuomba msaada. kwangu mimi hii inamaanisha kuwa waliotakiwa kuyatatua matatizo hayo (wasaidizi wa rais) hawafanyi kazi yao sawasawa. Tuendelee kumlaumu kwa makosa ya wasaidizi wake pia? labda hapa kosa lake ni kutowabadilisha haraka iwezekanavyo na kuchagua timu itakayom,pa ushirikiano wa kutosha.
Lakini pia kuna uwezekano kuwa kuna kitu kinamfanya ashindwe kuyafanya hayo mabadiliko ambayo tunayatamani. Ukisikiliza maneno yake, anaonekana kuwa ni mtu anayependa kuifanyia kitu fulani nchi lakini inaonekana kuna kitu kinamkwamisha

Kama wasaidizi ndio wanamkukwamisha awaondoe.....unakumbuka maneno ya Nyerere wasaidizi wanaweza kukusaidia kuwanong'oneza tu mawaziri kuwa waachie ngazi lakini mwenye kuchukua hatua ni Rais mwenyewe. Kwa maana hiyo sasa aende hatua moja mbele zaidi.
 
Watanzania tulivyowajinga, bado tutamrudisha JK mwaka 2010 kuwa rais wetu.

Unaona kabisa jamaa analinda wezi wa mali zako, bado unaendelea kumchagua tena kwa kura yako huru kwamba aendelee kuwa mlinzi wa hizo mali. Kweli Waafrika ndivyo tulivyo, nakubaliana na Nyani!
 
huo wote ni mchezo wa kuigiza,
lazima mkuu alishaisoma draft yote kabla ya kutoa go ahead ya kuchapwa kwa hiyo report,
lets wait and see their next move
 
Wakati mwingine napata shida kumuelewa Rais wangu

Rais bado hajaisoma ripoti hiyo, lakini ameshaanza kuishukuru Kamati kwa kazi nzuri! amejuaje wamefanya kazi nzuri?

Je majukumu ya Kamati hiyo yametimizwa?
- Je watuhumiwa wamechukuliwa hatua zozote za sheria? HAPANA
- Je fedha zilizotolewa isivyo halali zimerudishwa? HAPANA
- Mtuhumiwa namba moja Marehemu Daudi Balali alihojiwa? HAPANA

lakini bado Mh Rais anatuambia kazi iliyofanywa na Kamati ni nzuri! Tumekubali sasa tunasubiri taarifa hiyo rasmi.

Mimi nawauliza hebu hizi kelele zetu nini hatma yake? ni lini tutakuwa na mikakati bora ili kupata viongozi tunaowataka? kila kukicha Kikwete....Kikwete.

Nataka tujiandae, hizi hadithi za ripoti...., mafisadi... mara EPA, tuzitafutie dawa, dawa hiyo ni kujiandaa 2010 angalau tuwe na wabunge wengi wa upinzani, hataweza kuwanya lolote kwa maneno, tuwe na dhamira ya kweli jamani.
 
Tayari Mkuu ameomba mawaziri wote wawepo dodoma siku ya Alhamisi,sijui kuna agizo gani la serikali..

Mie nilitaka Ikulu watoe Ripoti ambayo ilikuwa haijafanyiwa editinng na CAG inayohusu EPa sababu ndiyo ina kila kitu

Nahisi kama anaweza akavunjwa serikali yote na kuamua kuunda upya tena......Tusubiri tusikie.
 
Hakuna jipya hapo, tusipoangalia hapa tutapigwa changa la macho. Msishangae ikaundwa kamati nyingine ndogo kuipitia hiyo ripoti. Maana siku hizi hakuna jambo linalofanyika bila kamati au tume. Nyie wana JF subirini mtashangaa tutakachoambiwa. Kwa kweli hakutakuwa na jipya zaidi ya kuambiwa fedha zinarudishwa na zitarudishwa.
 
Watanzania tulivyowajinga, bado tutamrudisha JK mwaka 2010 kuwa rais wetu.

Unaona kabisa jamaa analinda wezi wa mali zako, bado unaendelea kumchagua tena kwa kura yako huru kwamba aendelee kuwa mlinzi wa hizo mali. Kweli Waafrika ndivyo tulivyo, nakubaliana na Nyani!

Mkuu,

Tatizo si Kikwete peke yake bali ni wale waliokuwa na walio nyuma na mambo yoote yanayotendeka katika "system".

Kwamba wao walitoa pesa nzuri na ya kutosha tu kufanyia kampeni lakini walikuwa na ahadi ya Kikwete kwamba pesa ile ingerudishwa kutoka ndani ya "strong room" ya BOT, si zipo nyingi tu?

Kwa hio tusishangae hata RA akifanya kampeni ya uraisi na mgombea mwenza akawa EL au ikawa vice versa.

Ni uleule mzunguko, wa walewale.
 
Watanzania tulivyowajinga, bado tutamrudisha JK mwaka 2010 kuwa rais wetu.

Unaona kabisa jamaa analinda wezi wa mali zako, bado unaendelea kumchagua tena kwa kura yako huru kwamba aendelee kuwa mlinzi wa hizo mali. Kweli Waafrika ndivyo tulivyo, nakubaliana na Nyani!

Mkuu labda nikukumbushe kidogo, CCM ni kiboko kwa wizi, ni wezi kila angle, ni wezi kusi kaskazi mwa africa, marangapi wanamtuma komba kwenda nchi jirani kuelimisha wizi wa kura abmao wao wameufuzu... hivi unataka kuniambia kweli kabisa kikwete atashinda tena kw akishindo bila kura kuibiwa?????? walipofikia sasa hivi ni pabaya sana na wao wanajua na mpaka sasa hiviv hawajajipanga kujadili jinsi ya kuiba kura maana bado wako bize kuziba wizi wa epa na mengineyo.... ni wachache sana watakao wapa kura ila nyingi sana wataiba.. na safari hii wataiba kiasi kikubwa toka historia ya wizi wa kura kwao ulipoanza
 
Hakuna jipya hapo, tusipoangalia hapa tutapigwa changa la macho. Msishangae ikaundwa kamati nyingine ndogo kuipitia hiyo ripoti. Maana siku hizi hakuna jambo linalofanyika bila kamati au tume. Nyie wana JF subirini mtashangaa tutakachoambiwa. Kwa kweli hakutakuwa na jipya zaidi ya kuambiwa fedha zinarudishwa na zitarudishwa.

hahahhaaaaaa.... kwikwi kwi kwi kwi......... mbavu zangu uwii.... yani nimecheka sana, mbali na kucheka unalolisema ni kweli kabisa , si unakumbuka Pinda alishaanza kutulainisha siku zanyuma kuwa hawezi kujibu maswali ya epa na anachodhani hiyo kamati itaomba kuongezewa muda???
 
Hakuna jipya na la maana tutakaloambiwa. Hapa ni hadithi njoo uongo kolea mpaka asubuhi.
Raisi hatoongelea suala la EPA, RICHOMND wala MADINI. Anaweza kuongelea masuala hayo bila hata ya kulihutubia bunge. Vasco Da Gama anataka kuongelea masuala ya vifo vya wabunge, mimba za wanafunzi, timu ya taifa ya mpira wa miguu, migogoro ya Darful - Sudan, na jinsi Serikali ilivyomchukulia hatua muhasibu wa shule moja ya sekondari kule Songea kwa kuiba pesa.

Suala la EPA ni zito sana kwake na kwa chama Tawala. Mapesa ya EPA ndiyo yalimpeleka Ikulu, ataanzia wapi kujikana yeye mwenyewe?.

Hata kama akiongelea suala la EPA kuna nini kipya ambacho wananchi hatukijui toka mwanzo?, suala kubwa na muhimu lilikuwa ni kuwakamata wahusika na kurudisha mapesa yetu, sasa story tena za nini?.

SERIKALI 2 - WANANCHI 0 na mpira umekwisha.
 
my good piiiiiiiips.... another changa la macho on the way, kaeni mkao wa kula bye for now..........
 
Mkuu labda nikukumbushe kidogo, CCM ni kiboko kwa wizi, ni wezi kila angle, ni wezi kusi kaskazi mwa africa, marangapi wanamtuma komba kwenda nchi jirani kuelimisha wizi wa kura abmao wao wameufuzu... hivi unataka kuniambia kweli kabisa kikwete atashinda tena kw akishindo bila kura kuibiwa?????? walipofikia sasa hivi ni pabaya sana na wao wanajua na mpaka sasa hiviv hawajajipanga kujadili jinsi ya kuiba kura maana bado wako bize kuziba wizi wa epa na mengineyo.... ni wachache sana watakao wapa kura ila nyingi sana wataiba.. na safari hii wataiba kiasi kikubwa toka historia ya wizi wa kura kwao ulipoanza

Mbona hawakuiba Kigoma kwa Zitto? Mbona hawakuiba kwa Dr. Slaa? Vipi kule Moshi mjini mbona hawaibi?

Sidhani kama wizi ndio ulikuwa sababu ya JK kushinda kwa asilimia zaidi ya 70.
 
Habari za uhakika ni kwamba taarifa hiyo imekabidhiwa bila ya kuwapo waandishi wa habari leo hii IKULU, kutokana na Rais kukabiliwa na majukumu mengine muhimu ndipo akalazimika kupokea kwa haraka taarifa hiyo bila kuwapo waandishi.
mhh!mhh!mhh!
 
Back
Top Bottom