Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Waandishi undeni tume kuchunguza kwanini hawakuwaruhusu kuwepo wakati anapokea report.
 
Amen Amen Amen

Jamani jamani watanzania, mimi naona hakuna hata haja ya kusubiri kwa hamu hiyo hotuba kwa sababu: Haiwezekani kutoa kibanzi jichoni pa mwenzio wakati unalo boriti jichoni pako! ; Kama ilishindikana kuwekwa wazi gharama za kampeni ya mwaka 2005 na sources za funds hili la kuwachukulia hatua au hata kukiri uwepo wa mafisadi kwa majina yao kama tuwajuwavyo sisi, haliwezekani!
 
Labda baada ya kupokea rip[oti ya Mwanyika, amejipa siku kadhaa za kutoa boriti jichoni mwake kabla hajaenda kuuondoa kibanzi Ijumaa Bungeni
 
Expect alot on foreign affairs and more promises on the home front.It seems our presidents are usually still stuck on their old jobs for a few years remember Mkapa talking about sayansi na teknologia all the time in his first term?
 
Siku moja nilihudhuria mkutano wa mwanasiasa mmoja huko tarime. kabla ya mwanasiasa huyu kuzungumza mwananchi mmoja alinyoosha mkono kuuliza swali. alipoulizwa swali gani akajibu nataka kuuliza zwali kuhusu hayo mgeni atakayozungumzia.mfano huu ni sawa na baadhi ya wana JF tunaanza kujadili kukashifu kupinga wakati hatujajua Rais anataka kuzungumzia nini sasa nani msanii JK au wana JF

Kaka hakuna msanii hapa JF, kwani wachangaji humu ndani ni zaidi ya wananchi, maana wanawasilisha mawazo ya wananchi wengi zaidi hata ya wabunge waliowachagua kuwawakilisha kule bungeni kwa hiyo huwezi kuwaita Watanzania wasanii. Hata akija na maneno matamu kama asali, bado hayatakuwa na maana yoyote kwani maneno hayo hayatazidi yale aliyoyatoa wakati wa kuzindua Bunge.

Lakini Watanzania hawataki kusikia akihutubia Bunge au hata wajumbe wenzake wa CCM, wanataka vitendo, mafisadi wakamatwe na kufikishwa mahakamani, wafilisiwe na si kupeleka cheki hewa, wanafunzi wapatiwe mabasi kama wale wafungwa, wanafunzi wawe na madarasa na mabweni mazuri kama vile vyumba vya VIP kule Ukonga gerezani, walimu walipwe mishahara na malimbikizo yao, wanajeshi na polisi walipwe nauli ama wapewe mabasi na magari ya kutosha kuwafikisha watakapo, malumbano ya muungano na siasa zisizokwisha kule Zanzibar zimalizike na watu wachape kazi na kadhalika na kadhalika......
 
Siku moja nilihudhuria mkutano wa mwanasiasa mmoja huko tarime. kabla ya mwanasiasa huyu kuzungumza mwananchi mmoja alinyoosha mkono kuuliza swali. alipoulizwa swali gani akajibu nataka kuuliza zwali kuhusu hayo mgeni atakayozungumzia.mfano huu ni sawa na baadhi ya wana JF tunaanza kujadili kukashifu kupinga wakati hatujajua Rais anataka kuzungumzia nini sasa nani msanii JK au wana JF

Haya yanayosemwa hapa ni mambo ambayo yanasumbua vichwa vya wananchi{sisi tukiwemo} ambayo tungependa raisi wetu ayaongelee na kuyatatua.Tunachosema hapa wengi ni kua HATUTAKI maneno mengi na usanii ambavyo TUNAOGOPA vitatokea
 
Last edited by a moderator:
Katika hali isiyotarajiwa, waandishi wa habari waliokuwa wamekwisha kuingia ndani ya viwanja vya IKULU kuhudhuria uwasilishwaji wa kile kinachoitwa "Taarifa ya EPA" walijikuta wakirudishwa na kuambiwa watajulishwa ni lini au muda gani wataitwa tena.

Wakati huo Mwenyekiti wa Task Force iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa EPA, Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, alikuwa ndani ya majengo ya IKULU.

MASWALI YAMEIBUKA:
1. Je, Rais alipata dharura ya kukosa muda wa kuipokea?
2.Je, Rais hakuridhishwa na maelezo ya kina Mwanyika kuhusu taarifa yao?
3. Je, Rais ameshitushwa na taarifa hiyo kutokana na kugusa wengi?
4. Je, Rais aliona ni bora aisome kwanza ili akiipokea awe na cha kusema?
5. Je, Rais ameona hakuna sababu ya kupokea mbele ya waandishi?
6.Je, Rais aliona ni bora wahusika wachukuliwe hatua badala ya taarifa?
7. Je, Kina Mwanyika wamemwambia kazi bado nzito?

Na mengine mengi waandishi wamejiuliza na wananchi watajiuliza pia, JF munasemaje?

Option namba sita ni mojawapo kati ya options kuu tatu za Mh Rais....Hiyo ni ya kwanza....Ya pili ni wanaweza wasichukuliwe hatua zozote...Na ya tatu inaendana na highlight ya mwisho hapo juu...Ambapo hapa jf nimekubaliana na Akili Mtindi kama alivyo ainisha hapo chini...

Kufanya kweli inayoongelewa hapa kwa JK ni ngumu, nionalo mimi kama imebidi kuhutubia bunge wakiwemo mawaziri huenda wanataka kumtoa sadaka mmoja wao (ambaye washaongea naye wakapatana) ili imani irudi kwa wananchi kuwa JK bado yumo

Kama kweli JK yumo mfano rahisi amweke pingu Lowassa au Rostam, upo ushahidi mwingi sana kuhusu hawa "mapapa" kwahiyo hakuna haja ya kuwaundia tume ingine. Ikitokea hiyo nitajua kweli JK yumo, hata wakifungiwa kwenye hoteli zilizojengwa juzi huko magereza ingawa italeta balaa kubwa kwa kuonyesha matabaka waziwazi.

Naamini kama ana akili hakutakuwa na nafasi ya kuunda chombo kingine chochote kumshughulikia yeyote, nadhani sasa kama imetokea kuwa akina Mwanyika walishindwa kuyafanya aliyoyaagiza basi natamani kumwona akiyatamka kwa mdomo wake kwenye hiyo hotuba ambayo kwa hakika lazima atavaa "bukta tatu" ili awe imara kwa matamshi yake.
 
HABARI zilizonifikia hivi punde, zinaeleza kwamba sehemu ya hotuba ya RAIS inasema;

"Mheshimiwa Spika, nimepokea ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za EPA na tayari nimekwisha vikabidhi vyombo husika kwa ajili ya utekelezaji." mwisho wa kunukuu, na baada ya hapo ataendelea na mambo mengine muhimu ya Kitaifa na suala hilo hapo ndio utakuwa mwisho wake kujadiliwa kwani, "liko mikononi mwa vyombo husika".

Hapa kuna maswali, vyombo husika ni vipi? Si ndio alivyovipa kazi, na badala ya kufanya kazi, vikaja na RIPOTI, kwa hiyo sasa tutegemee na kusubiri RIPOTI nyingine kutoka "VYOMBO HUSIKA"..... Hii inawezekana Tanzania pekee
 
Vyombo HUSIKA ni kina MWEMA...Sasa Polisi yenyewe imegawanyika kama MILITIAS...Hata hao mafisadi wana VIKOSI VYAO vinavyowasikiliza...Na hadi sasa nadhani wahusika wote wa EPA wanachungulia madirishani ama kuwapigia simu Wanasheria,makamanda wao wa polisi na wanasiasa wengine wenye ushawishi ili wanuse nuse yatakayojiri...Na labda wapo hapa jf pia kama watanzania wengine ili kunusa nusa kama viji nzis.

Hapo my take ni kuwa...Mafisadi wanaweza wakawa wamezungukwa kwa sasa na wanaliwa MINGO....Na labda kama Mwema yalimshinda basi JK ndiye wa kusema...Akijidai kuwa lisizungumziwe kwasababu keshakabidhi kazi basi hapo ni usanii kwani hata yeye alikataa wazi wazi kuwa asikabidhiwe ripoti hiyo wazi....Na kwahiyo kama EPA ni issue MOTO...Then huo MOTO kama unamchoma Mkuu mwenyewe wa nchi...Then kina Mwanyika na Mwema si wa kulaumu....Mkuu wa nchi na jemedari ndiye kiongozi aliyeko mbele...Yeye ndiye atakayetuongoza kwenye kufikia maamuzi haya na si vinginevyo.

Na kwahiyo option ya Mwanyika kudai ni kazi ngumu bado ipo...Na option ya tume juu ya tume je?
 
Wakuu sijui JK amepanga kuwaambia nini watanzania kwa sababu pesa ya EPA ilipita mtandao wa Serikali yake na ile ya BEN na uliwaweka wao pazuri. Kweli nasubir atamke bayana ya Kagoda (Rostam), Jeet Patel, Vilman mwenye Serengeti Breweries (financier wa Michezo), kina Mramba, Yona na wengine wengi. Ameshapoteza dira JK wetu. Afuate nyayo za Musharaf. Then tunataka sisiemu ihalalishe makundi mawili na lenye nguvu lijiunge na upinzani iongoze nchi. Nimechoka wajameni ee.
 
Hizo pesa za EPA hazikujitoa zenyewe kutoka BOT.....Waanze na wale walio FACILITATE HIYO IDEA...Then wale walio i carry through na KUITEKELEZA!
Hata kama ni kweli pesa hizo zilimsaidia kushinda Uchaguzi..Haina maana kuwa wale waliofanikisha matumizi ya pesa hizo na wale walio initiate na ku implement hiyo idea hawako responsible.

Hao watu na watendaji wengine wa serikali ni lazima wawajibike kwasababu siamini kabisa kama wangemwambia JK toka mwanzo kuwa wamechukuwa pesa za EPA halafu na yeye akubali tu.

Pia labda utata mwingine bado upo kuwa hizo pesa zilitoka wapi.

Tusisahahu kuwa mara ya kwanza mgogoro huu ulipoanza viongozi wa mataifa ya magharibi badala ya kuuliza kuwa nani alikwiba...WAO SWALI LAO LA KWANZA LILIKUWA NI....PESA HIZO NI ZA NANI?

Na kabla hata ya blah blah za kina Membe....Viongozi wa mataifa ya Scandnavia walimbana sana JK na serikali yake...Na kuna yule aliyefanya ziara ya kuja bongo na mwandishi mmoja kutoka huko aliuliza wazi wazi kuwa pesa zilikuwa za nani...JK ALIWEKA WAZI KABISA KUWA PESA ZILE ZILIKUWA NI ZA WANANCHI...Baadae kukaja kauli nyingi sana za tofauti na kanganyifu zaidi kuhusu pesa zilikuwa ni za nani haswa!

Tena kuna wakati serikali ilisema pesa hizo ni za wafanyabiashara wa zamani zilizokuwa NBC...Na wakati mwingine kuna kauli zilizotoka kuwa HAZIKUWA NA MWENYEWE!

Inasikitisha sana kuona kuwa eti wafadhili wana uchugu tu na pesa zao...Sasa hata kama ni zao si waliwapa wananchi wa Tz?

Na kama si zao...Then ni za URANIUM? AMA KODI ZA WANANCHI?

Na vyovyote vile itakavyokuwa...Zilikuwa tayari kwenye taasisi ya umma na benki ya serikali(BOT) Na kwahiyo ni pesa za serikali...Na serikali ni ya wananchi...Serikali inahifadhi pesa za Taifa letu kwa kutumia taasisi ya benki kuu...BENKI KUU NI YA WANANCHI....Hivyo basi ni lazima waliowaibia wananchi kutoka kwenye benki ya taifa lao wawajibishwe...Then baada ya hapo tuangalie kuwa pesa hizo za wananchi zilifika vipi kwenye akaunti hiyo ya EPA.
 
Ktk hali yoyote ile iliyopelekea JK kuwa Rais wetu haimaanishi kuwa Tz haina rais kama tunavyoaminshwa humu ndani especially thread hii, tukubali na kuheshimu baraka na maamuzi ya waTZ na kwamba ndg.Jakaya Mrisho Kikwete ndie rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tz wa awamu ya nne.

Nasisitiza wakuu, presidency iko pale , Institution iko full occupied kila idara, tukishafahamu hilo ni vema sasa tutambue uwezo wa ki-Mamlaka alionao Rais , Taasisi anayoiongoza na uzito wa mambo yenyewe kwa wakati husika.

Uamuzi wa kuongea na Bunge ni uamuzi wa Taasisi yake baada ya yeye kwa utashi wake kuona kuna umuhimu wa kuongea na Bunge kama taasisi mdau ktk serikali yake.

Tusijipe wasifu wa Sheikh Yahya au Majimarefu bali Jf iruhusu wenye nyeti wazianike ingawaje bado naamini kuwa institution na mkuu wake wako ktk hali njema kiutendaji,uwasilishaji na utatuzi.

Tuwe na subira maana huleta heri wakuu
 
Jamani msitegemee chochote cha maana kuhusu EPA. Kama mmesoma Thisday na Kulikoni ya leo zinasema kwamba Yusuf Manji aliingizwa EPA kwa maelekezo ya JK. Biblia inasema kwamba wakati Yesu anapelekwa Golghota kusulubiwa alilemewa na msalaba mzito na baada ya kuanguka mara tatu wale askari walimshika mpita njia kwa jina anaitwa Simoni akabebeshwa msalaba wa Yesu! Katika ili Yusuf Manji ni "Simoni" wa EPA. Anabebeshwa msalaba ili "mwenyewe" apumue, tena inasemekana kwa maagizo ya JK. Kuna kitu hapo?
 
JK HAWEZI kusema Manji aingizwe kwenye EPA kwasabau EPA ilianza kabla hata JK hajapata URAIS...EPA imeanza kitambo tu kama ilivyo kwa Manji.....EPA ILIANZA WAKATI MKAPA NI RAIS na pia akiwa mwenye kiti wa ccm.

Manji na Mkapa walikuwa KITU MOJA kwasababu ya R.Mengi....Mtandao waliamuwa kutumia UKABILA NA UDINI...Na kama mnavyojuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea chuki ili tu wasiweze kuchukuliwa hatua ama kuulizwa lolote kuhusu ujambazi wao.

Kwa mantiki hiyo JK yuko kwenye wakati ambao ni yeye mwenyewe alijitakia.

Suala la Manji kuwamo humo si la ajabu...La ajabu lingekuwa kama Manji angekuwa hayumo.
 
Lakini ni kipi kinachopmfanya rais wetu aonekane ameshindwa? Ukisikiliza maneno yake na kusoma mikakati yake, inaonekana kuwa ni mizuri sana. Kwa nini utekelezaji unakwama? Ni tatizo la rais mwenyewe au wasaidizi wake? Nauliza hivi kwa sababu imefika wakati watu wengi wenye shida wanaamua kukimbilia wka rais mwenyewe kuomba msaada. kwangu mimi hii inamaanisha kuwa waliotakiwa kuyatatua matatizo hayo (wasaidizi wa rais) hawafanyi kazi yao sawasawa. Tuendelee kumlaumu kwa makosa ya wasaidizi wake pia? labda hapa kosa lake ni kutowabadilisha haraka iwezekanavyo na kuchagua timu itakayom,pa ushirikiano wa kutosha.
Lakini pia kuna uwezekano kuwa kuna kitu kinamfanya ashindwe kuyafanya hayo mabadiliko ambayo tunayatamani. Ukisikiliza maneno yake, anaonekana kuwa ni mtu anayependa kuifanyia kitu fulani nchi lakini inaonekana kuna kitu kinamkwamisha
Mpita Njia........waliomuweka madarakani na wanaomuweka mjini ndio wanaoharibu...hana jinsi ya kufanya.....hata ungekuwa wewe inabidi uchague kama noma iwe noma kwa kuwageuka washkaji au ukauke matatizo yaendelee...kuhusu ishu ya MAFISADI wa EPA nk watakubaliana kuwatoa kafara wawili watatu...lakini hakuna kesi ya maana....wadanganyika mtarajie hayo!!!!
 
Jana kwenye taarifa ya kina Rweyemamu wanasema Rais aliwapongeza kwa kazi nzito na ngumu lakini nzuri.... kilichonishangaza ni kuwa hata kusoma ripoti yenyewe hakusoma ndio amekabidhiwa tu... sasa alijuaje ni nzuri?
 
Mazingaombwe?
 
Back
Top Bottom