Katika hali isiyotarajiwa, waandishi wa habari waliokuwa wamekwisha kuingia ndani ya viwanja vya IKULU kuhudhuria uwasilishwaji wa kile kinachoitwa "Taarifa ya EPA" walijikuta wakirudishwa na kuambiwa watajulishwa ni lini au muda gani wataitwa tena.
Wakati huo Mwenyekiti wa Task Force iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa EPA, Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika, alikuwa ndani ya majengo ya IKULU.
MASWALI YAMEIBUKA:
1. Je, Rais alipata dharura ya kukosa muda wa kuipokea?
2.Je, Rais hakuridhishwa na maelezo ya kina Mwanyika kuhusu taarifa yao?
3. Je, Rais ameshitushwa na taarifa hiyo kutokana na kugusa wengi?
4. Je, Rais aliona ni bora aisome kwanza ili akiipokea awe na cha kusema?
5. Je, Rais ameona hakuna sababu ya kupokea mbele ya waandishi?
6.Je, Rais aliona ni bora wahusika wachukuliwe hatua badala ya taarifa?
7. Je, Kina Mwanyika wamemwambia kazi bado nzito?
Na mengine mengi waandishi wamejiuliza na wananchi watajiuliza pia, JF munasemaje?
Kama wa Pakistani nae ameachia ngazi asubuhi ya leo.Na ikiwezekana atueleze kwamba kazi imemshinda na yuko tayari kujiuzuru.
Kama wa Pakistani nae ameachia ngazi asubuhi ya leo.

tutatikisika