Kikwete apokea Ripoti ya EPA ajiandaa kuhutubia Taifa!

Kufanya kweli inayoongelewa hapa kwa JK ni ngumu, nionalo mimi kama imebidi kuhutubia bunge wakiwemo mawaziri huenda wanataka kumtoa sadaka mmoja wao (ambaye washaongea naye wakapatana) ili imani irudi kwa wananchi kuwa JK bado yumo

Kama kweli JK yumo mfano rahisi amweke pingu Lowassa au Rostam, upo ushahidi mwingi sana kuhusu hawa "mapapa" kwahiyo hakuna haja ya kuwaundia tume ingine. Ikitokea hiyo nitajua kweli JK yumo, hata wakifungiwa kwenye hoteli zilizojengwa juzi huko magereza ingawa italeta balaa kubwa kwa kuonyesha matabaka waziwazi.

Naamini kama ana akili hakutakuwa na nafasi ya kuunda chombo kingine chochote kumshughulikia yeyote, nadhani sasa kama imetokea kuwa akina Mwanyika walishindwa kuyafanya aliyoyaagiza basi natamani kumwona akiyatamka kwa mdomo wake kwenye hiyo hotuba ambayo kwa hakika lazima atavaa "bukta tatu" ili awe imara kwa matamshi yake.

Naamini, kama kuna kubwa aendalo kulifanya tungeshaona dalili zake maana halitakuwa jambo la kawaida kwenye uongozi wake. Sio siri pia kwamba hao wahusika watakaoshughulikiwa washazipata taarifa hizo na tayari weshafanya lolote kuhakikisha hakitatokea hicho tukionacho sisi kwamba kitaandika historia kwenye utawala wa msanii wetu wa komedi, JK - kiazi kizee akilini ila kionekanacho bado kibichi kwa nje. Nasema kizee kwasababu tukijidhania prezidaa ni mtu mzuri na safi...! basi akili yake inafaa kutibiwa maana imeoza kwa sasa...! vinginevyo tukikubali kuwa prezidaa ni mzima, basi tukubali ni mwizi mkubwa anayesimamia wenzake kuiba na kutumia mbinu zozote ziwezekanazo kuhakikisha wananchi hawashtukii mbinu zao.
 
Nahisi kama anaweza akavunjwa serikali yote na kuamua kuunda upya tena......Tusubiri tusikie.

Hawezi, huo ubavu wa kufanya hivyo atautoa wapi. Kwa kutizama utendaji wake toka achaguliwe, ni wazi anayo mapungufu makubwa ya kiutendaji wacha kuchukua maamuzi mazito, yangu macho. The man is just senile and incompetent, full stop.
 
Habari za uhakika ni kwamba taarifa hiyo imekabidhiwa bila ya kuwapo waandishi wa habari leo hii IKULU, kutokana na Rais kukabiliwa na majukumu mengine muhimu ndipo akalazimika kupokea kwa haraka taarifa hiyo bila kuwapo waandishi.

Wakati wa kuunda tume vifijo na vigelegele lakini kwa sababu report inawahusu wezi walio karibu yake inakuwa siri. S...... huyu sizitaki mbichi hizi.
 
Naungana na wanaobashiri kuwa hakuna jipya. Kama kungekuwa na jipya tungekwisha ona MATENDO, jamani MaTENDO.
Rais mwema ni hutenda na si kuishia kwenye hotuba.
Tujikumbushe wimbo wa Mwaitega anaosema kuwa tutakujua kama wewe ni mshika dini kwa kuona MATENDO.
Na tutajua tu rais amekasirishwa na ripoti ya wizi wa epa kwa kuona MATENDO na si maneno.
Jamani MaTENDO...
 
Nadhani sasa hivi hana ujanja isipokuwa kuchukua hatua kwa sababu gia ya kwanza ya "
Ripoti ya EPA" tumeichomoa mapema na tumeshamwambia Rais wetu kuwa hiyo haingii aje na nyingine. Anachoweza kufanya ni kusimama kuongoza.

a. Wakati Rais anazungumza na kuelezea hatua zilizochukuliwa kuhusu EPA vikosi vya Polisi vitakuwa kwenye nyumba na maofisa watakaotajwa na watu kutiwa mbaroni kufikishwa mahakamani. Miongoni mwao ni Mramba na Yona

b. Kiwira itatangazwa kurudishwa serikali baadaya kuwepo "irregularities" katika mchakato wa upatikanaji wote.

c. Rais atakubali kujiuzulu kwa Mwanyika kama Mwanasheria Mkuu na atatumia nafasi hiyo kutangaja jina la Mwanasheria Mkuu mpya ambaye ataapishwa pia kama Mbunge. Edward Hosea kuondolewa kutoka nafasi yake ya sasa na kuhamishiwa idara nyingine (kusubiri kupangiwa kazi nyingine).

Kimsingi, my instincts zinanilazimisha kuamini kuwa Kikwete atakachofanya ni kwenda to the other extreme ambayo itakuwa ni Over Kill. Ile Ijumaa na mwishoni mwa Jumaa kutakuwa na shamrashamra za watu kufurahia "Kikwete afanya Kweli".

Lakini kubwa zaidi atakalofanya ambalo naamini linaweza kuwa na alama kubwa zaidi ya Urais wake ni suala la Zanzibar kujitangaza kuwa ni nchi nje ya Jamhuri ya Muungano. Nimeandika kwa kirefu kwenye gazeti moja la Jumatano na nitaandika pia kwenye jingine kufafanua uzito wa hili. Katika kushughulikia hili, Watakuwa wamepitia hukumu ya Mahakama ya Rufaa na kujua tatizo lilipo na hivyo sitoshangaa kabisa kama Rais Kikwete atafanya kile ambacho kingefanywa miaka mingi iliyopita, nayo ni kuanzisha Mjadala wa Katiba ili mara moja na daima kuondoa kasoro za Muungano.

Nje ya hapa; I dare say itakuwa ni kuundwa kwa Kamati nyingine kushughulikia jambo jingine.

Utakuwa mwanzo mzuri, tusubiri tuone atasema nini ila nimeonya kuwa akianza kuchekacheka jua ni shoka na mpini kwenye shamba la miti, TUTAKUWA TUMEKWISHA
 
Itabidi nikae kwenye luninga kumshudia my Presdaa akishusha tabasamu, I like this
 
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu zana,
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Tazama Tanznia, ninapokwenda safarini,
Kutazamaa maajabu, biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi
Mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Tanzama Tanzania watu wako ni wema sana,
Wenye shida na taabu, kukimzwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Nchi nzuri Tanzania, karibu wasio kwao,
Nchi nyingi za kutoa, nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia, Ngome yako imara kweli wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
 
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
Nchi yangu Tanzania, Jina lako ni tamu zana,
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Tazama Tanznia, ninapokwenda safarini,
Kutazamaa maajabu, biashara nayo makazi
Sitaweza kusahau mimi
Mambo mema ya kwetu kabisa
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Tanzama Tanzania watu wako ni wema sana,
Wenye shida na taabu, kukimzwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote

Nchi nzuri Tanzania, karibu wasio kwao,
Nchi nyingi za kutoa, nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia, Ngome yako imara kweli wee,
Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote
Good old days! Sasa ni historia tu!
 
Good old days! Sasa ni historia tu!

Sidhani kama watoto wa zama za CCM wanaujua huo wimbo. Miaka ya zamani wanachi walikuwa na uzalendo na mapenzi ya kweli kwa mama yao Tanzania. Siku hizi tumebaki na mafisadi ambao hawana uzalendo wala uchungu na mama yetu Tanzania.

Iko wapi Tanzania ambayo ilikuwa ikisifika kwa kukaribisha wageni, Tanzania yenye nuru na mapenzi kwa wageni, Tanzania yenye amani na upendo wa kweli, Tanzania iliyojaa wapigania Uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika kuanzia Zimbabwe, Namibia, Msumbiji, Angola mpaka Afrika ya Kusini.

Tanzania ya sasa imebaki ni ya mafisadi na isiyo na amani tena! Je, ina maana kwamba wazalendo ndiyo wameisha? Na kama generation ya mafisadi itaendelea kuzaliana kwa kasi kubwa, nini hatima ya mama yetu Tanzania?

Mungu ibariki Tanzania na wazalendo na walaani mafisadi wote wasio na mapenzi na mama yetu Tanzania!
 
Siku moja nilihudhuria mkutano wa mwanasiasa mmoja huko tarime. kabla ya mwanasiasa huyu kuzungumza mwananchi mmoja alinyoosha mkono kuuliza swali. alipoulizwa swali gani akajibu nataka kuuliza zwali kuhusu hayo mgeni atakayozungumzia.mfano huu ni sawa na baadhi ya wana JF tunaanza kujadili kukashifu kupinga wakati hatujajua Rais anataka kuzungumzia nini sasa nani msanii JK au wana JF
 
Utamaduni gani huo
Utamaduni wetu ulikuwa wa kuwagawa watanzania kati ya wenye nacho na wasio nacho

Kuichukua tanzania na kuibinafsisha kwa mafisadi na waganga wa kienyeji na kufanya watakavyo

Utamaduni gani huo unaouzungumzia wewe ??

BabaH!!

haujamuelewa mwenzako anaposema "kama utamaduni wetu" anamaanisha utamaduni wa kuifisadi nchi na si vinginevyo, lakini ole wake
 
14. Suala la mahakama ya KADHI: nini msimamo wa serikali?. Mbona linachukua mjadala mrefu bungeni??!!!

Ahh..... nimesahau... maalbino!!!
 
Habari za uhakika ni kwamba taarifa hiyo imekabidhiwa bila ya kuwapo waandishi wa habari leo hii IKULU, kutokana na Rais kukabiliwa na majukumu mengine muhimu ndipo akalazimika kupokea kwa haraka taarifa hiyo bila kuwapo waandishi.

Hii itakuja kuwa sawasawa na kuangalia movie kutoka kwenye channel ya tv ambayo iko kwenye family mode....kila tusi au neno lisilofaa watoto kusikia linawekewa beep,mwishowe hata movie yenyewe inakuwa haileweki kutokana na beeps kuwa nyingi.
 
asilete mchezo mambo yanabadilika kwa kasi atakuja kuipata ajali ya kisiasa kama ya brother wake lo wasa
 
Na waigizaji wengine wa Zecomedy wanaounda kundi hilo pamoja na Kikwete watakuwepo? maana hatujaona Commedy siku nyingi jamani, nataraji mambo yakuchekeshana yatakuwa kwa wingi siku hiyo
Mheshimiwa RAis haundi na siyo mmoja wao wa kundi la ze comedy.tusifike huko na hajafikia usanii wa nanma hiyo,usanii ano ila siyo huo..
 
Back
Top Bottom